Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 14,522
- 17,153
Katika nchi za ukanda wa maziwa makuu, inaelekea kuwa nchi ya Tanzania imepoteza kabisa nguvu za kijeshi ilizokuwa nazo miaka ya sabini; inawezekana ni kwa sababu ya ufisadi wa wanasiasa wetu. Leo hii nchi inayoongoza kijeshi ni Rwanda, ikifuatiwa na Uganda, na kumalizia na Burundi. Tanzania na Kenya zinafuatia kutoka kwa mbali sana. Nimewahi kufuatilia kwa karibu sana data za kijeshi za nchi hizi ikiwa ni pamoja na aina ya silaha zilizopo, mafunzo na nidhamu ya askari, nikaona wazi kuwa Rwanda wako mbali sana. Ikitokea kuwa tumekorofishana nao kwa kweli sijui tutakimbilia wapi. Data hafifu zilizoko pale Wikipedia zinaonyesha kuwa Tanzania tunahitaji kujipanga upya kijeshi kwa kasi sana. Dunia ya maziwa matatu ina utata sana tusijejikuta tumeburuzwa na Rwanda kama wanavyofanya huko Kongo kutokana na raslimali nyingi tulizonazo.