Nguvu ya wananchi: Yamkumba mkuu wa wilaya Magu

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
Wananchi wagomea mkutano wa DC

Source: Tanzania Daima


na Ahmed Makongo, MaguWANANCHI wa Kijiji cha Yichobela, Kata ya Nyigogo, wilayani Magu, Mwanza, mwishoni mwa wiki waligoma kuhudhuria mkutano uliokuwa umeitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo (DC), Mathow Nasei, kwa ajili ya kuzungumzia matukio ya ujambazi hadi mwenyekiti wao ajiuzulu.
Kwa mujibu wa mtendaji wa kata hiyo, Mary Ng’ wandu, alisema kuwa mkutano huo uliokuwa na agenda tatu, ikiwemo ya kuzungumzia matukio ya ujambazi kijijini hapo, kuhamasisha maendeleo ya ujenzi wa sekondari ya kata hiyo, pamoja na ufujwaji wa fedha za michango ya wananchi kwa ajili ya ujenzi wa sekondari, ambazo ni sh 544,000.

Mkuu huyo wa wilaya, Nasei alifika kijijini hapo saa 5:30 asubuhi, kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao, lakini hakukuta watu kama alivyotarajia zaidi ya kukuta watu wasiozidi sita akiwemo, Diwani wa kata hiyo, Kulwa L. Nyawayi, Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, pamoja na wajumbe wawili wa serikali ya kijiji hicho.

Kutokana na hali hiyo, mkuu huyo wa wilaya (DC), alilazimika kuahirisha mkutano huku wakiulaumu uongozi wa kijiji hicho kwa kushindwa kuhamasisha wananchi kuhudhuria mkutano huo muhimu.

“Inawezekana hapa kuna tatizo kubwa sana, sasa tunakuja kuwasikiliza ili tupate ufumbuzi, tunakuta hali hii. Hivi kwa nini uongozi wa kijiji umeniaibisha kiasi hiki? Nafikiri mheshimiwa diwani uniruhusu niondoke,” alisema.

Baada ya DC huyo kuondoka, Diwani wa kata hiyo, Kulwa Nyawayi, pamoja na baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji hicho waliokuwapo walimtaka mwenyekiti huyo wa serikali ya kijiji, Shija Ntubi, kujiuzulu.
 
Back
Top Bottom