Nguvu ya umma ya Waarabu ilianzaje mnajua...!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya umma ya Waarabu ilianzaje mnajua...!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Papa Mopao, Nov 15, 2011.

 1. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kuna thread moja inazungumzia kuhusu Escape from Sobibor, mtoa mada kazungumzia kuhusu nguvu ya umma ambayo hiyo film ndani yake kafananisha na nguvu ya umma, wachangiaji wengi wametoa maoni yao kwamba havifanani na nguvu ya umma.

  Sasa, katika hili limenikumbushia kuhusu Nguvu ya Umma katika nchi za kiarabu, nilitazama Documentary inayozungumzia Arab's movements aljazeera ndo walionesha na nilibahatika kuiona.

  Nikianzia Tunisia japo nitaeleza tukio lilivyotokea:

  Kule Tunisia, kulikuwa na kikundi kidogo tu ambacho kilianzisha movement ya kuupinga utawala wa wakati huo, sasa kwa mbele ya hao watu(waandamanaji) kulikuwa kundi kubwa la polisi (kama FFU) nao walizuia watu kupita kuelekea sehemu walizokusudia kupita tena ilikuwa mjini kabisa huko Tunis, sasa kulitokea lile gari la maji na kuwamwagia watu na watu walikimbia, kitu cha ajabu kabisa alibaki kijana mmoja na wala hakukimbia kabisa na lile gari la maji lilimsogelea karibu kabisa mithili kama vile anataka kugongwa lkn hakugongwa wala kukamatwa na polisi wa Tunisia, yule jamaa akageuka nyuma na kuwaambia watu wasogee wasiogope kitu, ule ujasiri wa yule kijana ndo iliamsha watu na watu wakasogea kabisa, magari ya maji yaliongezeka na kuwamwagia watu lkn watu hawakutoka na yule kijana akalala chini kama ishara kwamba "hatutoki hapo" na nguvu ya umma ililala chini, polisi walizidiwa na kurudi nyuma na watu wakazidi kuongezeka na kuongezeka mpaka wakafanikiwa kufikia malengo yao.

  Chanzo cha Nguvu ya Umma kusimama barabarani kwa Tunisia ni yule kijana na waandishi wengi walisema yule kijana ndo alikuwa chachu kabisa na watu wengi walivyoshuhudia kupitia vyombo vya habari ndo walipata moyo wa kwenda barabarani na kuenda kusimama na kuupinga utawala uliopo.

  Nikija kwa Misri:

  Misri, kulikuwa na waandishi wa habari waliokuwa juu ya hotel fulani, wale waandishi walikuwa wanapiga tu stori pale juu ghorofani hotelini mida ya asubuhi asubuhi kama saa mbili hivi, ghafla walishuhudia kikundi cha watu upande wa ng'ambo ya mto Nile unaopita pale mjini, wakapiga picha lile tukio na kuweka mtandaoni, kumbe wananchi wa misri walibahatika kuiona picha ya lile tukio, wale waandishi wakashuka haraka kutaka kujua kulikoni pale, walipowauliza wale watu wakasema hatumtaki Mubarak na tunataka kuuziba njia hapo darajani, waandishi wakachukua picha na pia kuna waandishi waliobaki kule juu ghorofani nao wakachukua video, kumbe wakati huo wananchi walifuatilia lile tukio la laivu kupitia kituo cha tv na mtandaoni, hicho ndicho kilikuwa chachu ya nguvu ya umma kuongezeka pale darajani na watu wakazidi kujaa, polisi waliwajaribu kuvuruga maandamano lkn wapi na baadae nguvu ya umma iliwafukuza polisi na kufanikiwa kusogea hadi eneo walilokusudia kufika.

  Kwa ufupi ni haya...!
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Ya Tanzania yanategemewa kusisimua dunia na haitaamini kama hawa ndiyo watanzania kweli!!!!
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  wanaume, kina kaka na kina baba, wanawake tuko tayari kulala barabarani, hata kupata mateso ya kupakwa pilipili huku chini. Je kina baba mko tayari kutupa support kwa kulala barabarani? Msiyaogope maji ya upupu. Tuungeni mkono. Huo mwezi ujao mtaona jinsi wanawake tutakavyo onyesha dunia kuwa tunaweza kuleta mabadiliko.
   
Loading...