Nguvu ya Umma: Tofauti yetu na Kenya sisi tumeliwa kichwa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
Kauli ya umma ni kauli ya Mungu. Haijawahi kushindwa popote chini ya jua.

Aungurumapo Simba mcheza nani?

Ni kupata katiba mpya, kuondokana na longo longo za mamlaka, ni kuwawajibisha wabadhirifu, nk?

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir

Sisi tuko hapa:

FuzzZy9akAEOIva.jpeg

Bipartisan talks must end in 30 days, Raila says as Azimio suspends protests, again

Anasema Odinga:

"We have instructed our delegates to make it clear that we want these talks concluded in 30 days from the date of commencement. We have also made it clear that our youths, who have been arrested and arraigned, on trumped-up charges, must be released unconditionally ahead of the talks."

IMG_20230505_051536.jpg

Anaendelea Odinga:

"We have instructed our delegates to raise this. We wish to make it absolutely clear that we are not interested in power-sharing with Kenya Kwanza. In fact, our position remains that Kenya Kwanza is an illegitimate regime that is in power through a civilian coup. We have instructed our team to make this clear. We are not interested in any deals other than open public talks on issues we have made public,"

Kipi ni wazi kuliko hiki?

"We will not hesitate to resort to alternative measures at the slightest indication of lack of good will and honesty on the Kenya Kwanza side. If, through intransigence, delay tactics and other aspects of stonewalling Kenya Kwanza forces us to abandon the talks, there shall be no turning back,"

Ushauri wa bure tunahitaji utaratibu mzuri vyamani kuwapata kina Raila. Hili ni ni jambo la dharura sana. Kina Raila wapo wengi vyamani.

Hatuwezi kuendelea kuwaweka hao benchi kama ni nia yeti ya dhati kuupata ushindi tunaoutaka.
 
Ndugai: Nilitaka kumkutanisha Mbowe na Shujaa Maguful lakini akakataa akiwahofia Wenzake!

Odinga hana cha kuwahofia wenzake. Odinga anaongea kauli za watu. Kwenye kauli za watu nani atamhofia nani?

Waitara aanza kuongea lugha ya watu

Kauli za watu (language of the people) huvutia, hufurahisha, huburudisha nyoyo na kunenepesha mifupa.

Hofu na iwepo kwenye maridhiano ya siri. Kama nongwa na iwe nongwa.

Tangu lini sera za chama zikawa siri? --- JKN

Kwani Erythrocyte anasema je? Au naye ni mwendo wa kupita juu kwa juu kama wale wenzetu wengine?
 
Raila anaelewa maana ya Dola. Sasa amebaki na porojo na mineno mirefu kana mifupa ya kamongo huku akibweka bweka kana wainjilisti wa CHADEMA

Kwamba porojo au maana ya Dola? Kwani Ruto, Gachagua au lile genge lao umewasikia wanasema je?

FutD12pWIAEjDDU.jpeg

Kulinganisha CHADEMA ya leo na Odinga huyu, labda kama ni kuamua kujitoa ufahamu tu ndugu.
 
Zawadini kuna wito wako hapa:

IMG_20230505_051536.jpg

Hapo ni muunganiko wa vyama kadhaa. Sisi ubinafsi uliopitiliza kwa maslahi ya nani?
 
Odinga yupo very clear, amenifunza yafuatayo na kuyalinganisha na hapa kwetu, ambapo sadly hali imekuwa complete opposite..

- Anataka mazungumzo yaishe ndani ya siku 30, hapa ameshagundua kuyaacha muda mrefu ni kuwapa mamlaka nafasi ya kuleta utani.

- Amewazungumzia delegates, hili linaonesha jamaa wana watu kwenye mazungumzo yao sitting room, na wala sio ya watu wawili chumbani kama kwetu.

- Amemtaka Ruto kuhakikisha anawaachia huru wote walioshtakiwa kwa makosa ya kubambika, hapa kwetu bado Sanga yupo ndani sijui siku zimefika ngapi sasa, naona siku hizi kazi yetu ni kuzihesabu tu..

- Zaidi anasema they are not interested in power sharing, anamuona Ruto muhuni aliyeingia madarakani kwa civilian coup, hawa wa kwetu wanavyopenda pesa kupitia ubunge nk wakipewa hii chance sidhani kama wataiacha..

- Lakini pia, uwezo wa Odinga kuyasema wazi yale yote anayohitaji kwenye mazungumzo yake na Ruto, hajaficha chochote, ameyaita ni mambo public na kwasababu hiyo anaamini public lazima iyajue, vipi hapa kwetu, ni yupi kati yetu anayezijua agenda za kwenye maridhiano?!.
 
Hapa ndipo ilipo tofauti yetu na Kenya ambapo kina Yonda, Waterleo, na wa namna hiyo ni kina Magonjwa Mtambuka tu, walio janjaruka.

Au nasema uongo ndugu zangu.
 
Tatizo SIYO nguvu ya Umma tatizo ni hoja yenye mashiko ya kuifanya nguvu ya Umma ufanye KAZI yenye maslahi mapana Kwa umma.

Siyo kila nguvu ya Umma ina tija! Isije ikatokea mawazo ya mtu mmoja mwenye Nia ovu au ambaye hajafanya utafiti wa kutosha lakini akatumia ushawishi wake Kwa Jamii na kujifanya hiyo ndiyo nguvu ya Umma mifano ni mingi hata hawa wakina Mackenzie wanaweza kutumia nguvu ya Umma kutimiza matakwa Yao binafsi.

Tuwe makini kufuata mkumbo bila kufanya utafiti.
 
Back
Top Bottom