Uchaguzi 2020 "Nguvu ya umma" itaamua uchaguzi huru na haki mwaka huu

Wewe Mataga nani aliyekupa mamlaka ya kutusemea sisi Watanzania? Kwani nyinyi Ccm mna faida gani kwenye nchi hii zaidi tu ya kuendekeza vitendo vya rushwa, ufisadi, upendeleo, wizi wa mali za umma, kununua wanasiasa uchwara kwa kodi zetu na kujilimbikizia mali?
Nani kakuambia nakusemea? Mimi nazungumzia uhalisia wa kisiasa Chadema ni matapeli wa kisiasa. Kama Ccm ni mafisadi ingefanya maendeleo makubwa kama haya! Au unaleta hoja za hisia tu? Waliohama Chadema waliunga juhudi kwa dhamira zao wenyewe baada ya kumkubali JPM na Ccm.
 
Sina tatizo na kuitisha nguvu ya umma, naona cdm kama chama hamshiki hoja na kuimalizia. Kabla ya baa la Corona na kuzuiliwa mikusanyiko, ilikuwa kuna vuguvugu la kudai tume huru ya uchaguzi, na hoja ya kwanza ambayo tungeanza nayo baada ya kusema kutakuwa na mikutano, ni hiyo ya kudai tume huru.

Lakini baada ya bunge kuvunjwa naona kama hoja ya kudai tume huru ya uchaguzi imekufa midomoni mwenu, na sasa mnaongelea nguvu ya umma. Kwa tafsiri ya haraka ya ccm na vyombo vya dola, nguvu ya umma ni uvunjifu wa amani. Mimi nilitarajia kila kiongozi anayesimama aseme tunahitaji tume huru ya uchaguzi, neno hilo litumike mpaka liwe kero kwa kila mtu. Halafu mtangaze kutumia nguvu ya umma tena kwa herufi kubwa, kuwa mtatumia nguvu ya umma kwakuwa tume ya uchaguzi sio huru. Tunatakiwa tuingie kwenye uchaguzi huku tukiifanya tume iwe haiaminiki, na hata matokeo itakayotoa yasiaminike kabisa. Kwasababu iwe isiwe lazima tume hii iibebe ccm, namna pekee ni kuinyima uhalali wa kusimamia uchaguzi, na kuitangaza kwenye kila platform kuwa sio huru.

NB: tarehe 7/7/20 tuhakikishe tunavaa nguo nyeupe, ili kupandisha hamasa ya kudai tume huru vya uchaguzi. Madai ya tume huru ya uchaguzi ni ya halali na hayana muda. Kwahiyo hakuna kisingizio cha kuwa muda umeisha.
Upinzani nchii hii mathalan CHADEMA hawana nia ya dhati ya kutwaa madaraka kwenye nafasi yoyote ya Uongozi hasa nafasi ya Urais wa nchii hii , Period.. Wanachofanya ni kubweka tu kama m.bw.a koko asiye na meno ! Kazi kulia lia tu.

USHAURI ulioutoa hapo juu huwezi kuona wakiufuata hata chembe
 
Upinzani wangekua wanafanya utafiti kabla ya uchaguzi wangeshayajua matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Mnyika anawaanda nyumbu kisaikolojia tu
Hayo maneno sio mapya,huyo mbunge hata akitangazwa na nguvu ya umma ataingia bunge gani bila ya kupewa cheti na mkurugenzi?
Wameshagundua hawapati hata jimbo moja,wanaanda watu kufanya fujo
 
Upinzani nchii hii mathalan CHADEMA hawana nia ya dhati ya kutwaa madaraka kwenye nafasi yoyote ya Uongozi hasa nafasi ya Urais wa nchii hii , Period.. Wanachofanya ni kubweka tu kama m.bw.a koko asiye na meno ! Kazi kulia lia tu.
Mkuu, ulikuwepo pale Kinondoni alipouliwa Binti Akwilina?

Sawa, shukrani zako nyingi kama ulichangia kuwatoa viongozi wa CHADEMA gerezani Segerea.

Samahani sana, kama hukunielewa hapa.
 
CDM msikimbilie kuwa na maamuzi kama hayo, huu ni uamuzi mgumu ambao mnapaswa kuufanya hatua kwa hatua, ili nguvu ya umma iwe ni "the last resort" kwa ushirika wa vyama vyote vya upinzani. Kwepeni kuwa nyie ndiyo wenye "ownership of civil violance" kwa kuwa mtakabiliana na maovu mengi kutoka kwa watesi wenu.
 
Nani kakuambia nakusemea? Mimi nazungumzia uhalisia wa kisiasa Chadema ni matapeli wa kisiasa. Kama Ccm ni mafisadi ingefanya maendeleo makubwa kama haya! Au unaleta hoja za hisia tu? Waliohama Chadema waliunga juhudi kwa dhamira zao wenyewe baada ya kumkubali JPM na Ccm.

Basi sawa.
 
Mkuu, ulikuwepo pale Kinondoni alipouliwa Binti Akwilina?

Sawa, shukrani zako nyingi kama ulichangia kuwatoa viongozi wa CHADEMA gerezani Segerea.

Samahani sana, kama hukunielewa hapa.
mkuu naona unajaribu kuingiza mada mpya. hivi kwa mazingira ya kisiasa ya Sasa nchini kweli Upinzani wanajitapa kwenda kushinda Uchaguzi? Bila Tume huru ya Uchaguzi kweli???
 
mkuu naona unajaribu kuingiza mada mpya. hivi kwa mazingira ya kisiasa ya Sasa nchini kweli Upinzani wanajitapa kwenda kushinda Uchaguzi? Bila Tume huru ya Uchaguzi kweli???
Kuna kutoelewana.

Hapa hujanielewa kabisa nilichoandika.

Nashangaa pia kwa kueleza mambo ya "kushinda uchaguzi bila ya tume..." kwa sababu sijaelezea jambo hilo katika hiyo mistari niliyoweka hapo na wewe kuijibu kivyako.
 
Back
Top Bottom