Nguvu ya Umma isiyoratibiwa imeanza kufanya kazi nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya Umma isiyoratibiwa imeanza kufanya kazi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  [​IMG]

  KILA kona nchini Tanzania yanasikika malalamiko ambayo msingi wake ni ugumu wa maisha ambao unasababishwa na mambo kadhaa wa kadhaa. Wanasiasa nao wanahaha kutafuta kuungwa mkono na wananchi kwa lengo la kushika au kuendelea kuwa madarakani.
  Harakati hizo za kisiasa zinafanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na semi na mitindo anuai, mathalani kujivua gamba, operesheni sangara, operesheni zinduka na nyinginezo. Lengo la kila Chama ni kuufikia na kuuhamasisha umma ili ukiunge mkono.
  Harakati hizo hivi karibuni zimeibua dhana kwamba nchi inaweza kupoteza amani kutokana na baadhi ya mbinu zinazotumiwa na wanasiasa. Inadhaniwa kuwa nguvu ya umma inaweza kuchochewa kwa lengo la kuuondoa uongozi uliopo madarakani.

  Hata Rais Jakaya Kikwete, akihutubia taifa mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu, alikishutumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba maandamano na mikutano ya hadhara ya nchi nzima kinayofanya ambayo ilianzia mikoa ya Kanda ya Ziwa ina ajenda ya siri ya kutaka kuuondoa uongozi wa nchi madarakani isivyo halali.Mtaalamu wa siasa ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, anabainisha kuwa nguvu ya umma siyo dhana hamasishi bali huleta maana inapohalalisha mapambano dhidi ya mfumo unaothibitika kuumiza umma. Anasema nguvu ya umma hailengi mtu, chama wala kundi fulani la watu.
  Ally anasema nguvu ya umma kabla haijafikia hatua ya kuleta mabadiliko, hutafakari na kubaini kuwa madhara yanayoipata kutoka kwa kundi, mtu au chama fulani yanatokana na mfumo, hapo ndipo nguvu ya umma huratibiwa kukabiliana na mfumo huo na kwamba siyo lazima uongozi ulio madarakani uondolewe, ingawa hutokea mabadiliko makubwa ndani yake.
  Vuguvugu la nguvu ya umma nchini linaweza kuleta mabadiliko ya kiuongozi?
  Ally anasema Tanzania ni sawa na Chuo Kikuu cha nguvu ya umma kwa sababu hata uhuru wake ulipatikana kwa nguvu hiyo, nembo ya chama tawala (CCM) yaani ni jembe na nyundo inamaanisha nguvu ya umma (wakulima na wafanyakazi).
  “CCM kipo kwa nguvu ya umma. Asili ya Tanzania ni kuongozwa kwa nguvu ya umma bila shaka unakumbuka enzi za Hayati Mwalimu Nyerere…, matatizo yalianza miaka ya 80 baada ya serikali kuingia kwenye mtego uliovishwa vazi la biashara huria…, ambao unalazimisha serikali kulinda maslahi ya mwekezaji badala ya maslahi ya umma,” Ally anaeleza.
  Anasema ili nguvu ya umma isababishe mabadiliko yenye kuleta manufaa, lazima iratibiwe ingawa yeyote anayejipa jukumu hilo lazima akumbane na kigingi cha kuitwa mchochezi.
  Hata hivyo iwe isiwe, pale nguvu ya umma inapohitajika inatokea tu kwa sababu hakuna mwenye uwezo wa kuzuia matakwa ya umma.
  “ Yeyote anayejitolea kuunganisha umma ili ukabiliane na mfumo kandamizi ni lazima adhibitiwe kwa kuitwa mchochezi lakini nguvu ya umma haidhibitiki, wakati unapowadia umewadia,” Ally anabainisha.
  Katika hali ya kawaida nguvu ya umma huratibiwa kupitia makundi maalumu katika jamii, kama vile vikundi vya wanawake, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima; Ushirika, vyama vya vijana na vile vya kiraia kwa lengo la kupinga mfumo ambao umethibitika kukandamiza jamii.
  Awali kila kikundi hufanya mapambano peke yake kwa namna inavyoonekana inafaa, lakini malengo yanaposhindikana kufikiwa, ndipo umuhimu wa kuungana unapoonekana na hatua za makundi hayo kuunganisha nguvu dhidi ya mfumo husika inapotekelezwa.
  Hatua hiyo ya kuunganisha nguvu ya vyama na vikundi vyote ndiyo inayoonekana kuwa ngumu hapa nchini na hivyo kuashiria hatari ya kuibuka nguvu ya umma isiyoratibiwa. Hatari hiyo inatokana na makundi hayo ambayo kwa kujua au kutojua, kugawanyika, jambo linaloleta ugumu katika kuwezesha uratibu wa nguvu ya umma.
  Kwa mfano vyama vya wafanyazi, vimegawanyika na kila kukicha vinashambuliana kwa namna tofauti. Kadhalika vile vya wakulima, wafanya biashara, wanawake na hata vyama vya vijana.
  Ally anasema ili nguvu ya umma ilete matunda bora kwa jamii ni lazima vikundi hivyo viungane kwa nia moja tu ya kukabiliana na mfumo bila tofauti za kisiasa, kidini wala kabila.
  Mtazamo wa Ally kuhusu vyama vya siasa kusababisha nguvu ya umma kuleta mabadiliko ya kiuongozi nchini ni kwamba hilo haliwezekani kwa sababu wanasiasa karibu wote hawaumizwi moja kwa moja na ubovu wa mifumo ya huduma kwa jamii.
  Aidha jamii ya Watanzania imeng’amua kuwa dhana wakilishi haina uwezo wa kuikomboa dhidi ya mifumo kandamizi hivyo linalotarajiwa ni jamii yenyewe kuondoa tofauti zake na kuungana kwa lengo la kujiletea mabadiliko, kwa maslahi yake yenyewe.
  “Jukumu la kuwa na uongozi bora ni la umma wenyewe, umma wenyewe hutekeleza jukumu lake la ama kuuondoa madarakani uongozi uliopo au kushinikiza yafanyike mabadiliko makubwa,” Ally anaeleza.
  Hata sasa nchi inapitia kipindi cha mabadiliko yanayotokana na nguvu ya umma isiyoratibiwa. Ally anatoa mfano mmoja wapo kuwa ni matibabu yanayotolewa na aliyewahi kuwa Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT), Ambikile Mwaisapile, Loliondo mkoani Arusha.
  Mwaisapile almaarufu Babu, alianza kutoa tiba ya magonjwa yote sugu ukiwamo UKIMWI siku nyingi lakini tiba hiyo imepata umaarufu mkubwa baada ya vyombo mbalimbali vya habari kutangaza shuhuda za baadhi ya waliokunywa na kuponywa na tiba hiyo ambayo hutolewa kwa kipimo cha kikombe kimoja tu.
  Kufuatia shuhuda hizo kutiwa nguvu na baadhi ya madaktari baada ya vipimo kuonyesha maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua hayapo tena, idadi ya watu kuelekea kwa babu kunywa kikombe cha dawa iliongezeka kwa kasi kubwa. Katika kinachosadikiwa kuwa ni serikali kutekeleza jukumu lake la kulinda raia dhidi ya hatari au ashirio la hatari, ilitangaza kuzuia tiba hiyo.
  Hata hivyo Serikali ya Mkoa wa Arusha ilitamka wazi kuwa ni vigumu kutekeleza uamuzi huo kwa sababu ya wingi wa watu wanaoamini na kufuata tiba hiyo. Baadaye Uamuzi huo ulilegezwa na mpaka leo matibabu yanaendelea. Ingawa tiba inatolewa kwa imani, wanaotibiwa hawabaguliwi kwa imani zao.
  Kilichozuia Serikali kushindwa kutekeleza jukumu lake hilo ni umoja wa watu ambao haujali tofauti zao za dini, siasa, umri, jinsia, elimu wala kabila bali unaoashiria kukosa imani na mfumo wa kisayansi duniani katika kutibu magonjwa sugu badala yake kuamini tiba inayotolewa na babu Mwaisapile. Ally anasema huo ni mfano halisi wa jinsi nguvu ya umma inavyofanya kazi.
   
 2. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ni mpotoshaji mwingine anayetafuta ulaji serikalini fasta fasta.
  Nguvu ya UMA ndani ya Tanzania inaratibiwa vizuri sana katika misingi ya kisiasa, siasa inaleta makundi yote pamoja, Wafanyakazi, Wakulima, Wanafunzi,Vijana, wakina mama,waamini wa dini tofauti tofauti, wanaunganishwa pamoja katika uratibu wa kisiasa na sasa kwa pamoja wanataka madaliko.

  Watanzania wamegundua kwamba tatizo sio vijana hawathaminiwi katika taifa, wala tatizo sio mfumo dume, tatizo sio imani za kidini, wala tatizo sio mifumo ya kiuchumi.

  Watanzania wameng'amua kwamba matatizo yetu yanasababiswa na ombwe katika uongozi wa kisiasa unaosimamia uendeshaji wa serikali, na sasa wanataka kuuondoa uongozi wa kisiasa uliopo, wameamua kukipiga chini chama cha mapinduzi.

  Kwa utaratibu mzuri kabisa, wanatambua kwamba namna ya kuondoa uongozi wa kisiasa kama tunavyoongozwa na katika yetu ni kupitia sanduku la kura, wamefanya namna hiyo katika uchaguzi mkuu 2010, lakini wamedhurumiwa, maamuzi yao yamechakachuliwa na sasa katika mpangilio safi, unaofuata taratibu safi kabisa wanapush kupata katika mpya, wakiamini kwamba hili ni jibu la maatatizo mengi
  ikiwemo fursa iliyotumiaka kuchakachua maamuzi yao kwenye uchaguzi mkuu.

  na zaidi, kwa sababu siku hazigandi, wanaisukuma serikali ifanye kazi yake, na wanaiongoza ifanye
  kazi kama ambavyo UMA unaitegemea ufanye, maandamano tunayoyaona na yatakayokuja na sauti za kelele kwa serikali iliyo madarakani kutekeleza yale inayopaswa kutekeleza.

  Serikali inayoratibiwa vizuri, itafuata maelekezo ya UMA, ikikaidi ni kweli machafuko yatatokea.

  Huyu bashiru nimemsikiliza dakika chache za mwisho kwenye kipindi cha je tutafika channel ten wiki
  hii, alikuwa anaongea upuuzi wa kiwango cha juu sana.

  Huyu sio msomi, ni mwana CCM.
   
Loading...