Nguvu ya Umma is synonymous to mob justice, ipigwe vita Haraka sana.

Nguvu ya uma inafanyika pale ambapo viongozi au vyombo vya kutoa haki kwa jamii visipofanya kazi basi wananchi huchoka na kuamua kuchukua maamuzi yao. Au unasemaje bwana sixgate. Sipendi walichofanya wananchi ila wangefanyaje maana huyo jamaa anauwezo wa kuwaweka Polisi pamoja na mahakimu mfukoni,
 
Hizi ajira za njaa kwamba kila siku ni lazima uonekane umeandika kitu ni mbaya sana!

Embu jaribu KU-RELATE KICHWA CHA UZI NA TUKIO LA MABINA. Two different things.

Kuna uzi uliwekwa humu uki-analyse uelewa wa watu aina yako Conclusion of which was pathetic!

Sijausoma, weka link
 
Unaitafsiri namna gani kitendo cha huyu mwenyekiti wa chama kumpiga raia risasi???!
Leo mchana tumepokea shocking news kuwa aliyekuwa cadre na ccm chairperson kwa mkoa wa mwanza ndg Mabina Clement amepijwa mawe mpaka kufa kutokana na land conflicts. (Hii taarifa ipo sitaizungumzia sana naomba nizungumzia tabia ya kujichukulia sheria mikononi in the name of nguvu ya umma/mob justice)

Kwanza nianze kwa kusema nalaani mauaji ya Mabina yaliyotekelezwa na wananchi wa kisesa mwanza, naomba niwakumbushe kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kuhukumu mtu nje ya mfumo tuliojiwekea,ambapo hukumu hutolewa na mahakama.

Nakemea kwa sababu Mob Justice ni tabia ambayo inakuwa kwa kasi, pengine is due to weakness in Judicial System which does not work properly and people continue to organize their trial and judge their suspect on street kwa kuwaumiza au kuwauwa kama ilivyotokea leo mwanza. Hii tabia inahitaji immediate attention kuhakikisha maisha ya watu wenye/wasio na hatia hayaendelei kupotea mikononi mwa wanaojiita "wananchi wenye hasira kali"

I would like also to remind political party's leaders especially hawa wa chadema ambao at some point ni catalyst katika kuvuruga mfumo tuliojiwekea wa "utawala wa sheria" kuwa there is no one who is above the law lakini wao wamekuwa wakitembea in up countries preaching the so called "nguvu ya umma" which means "wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho katika taifa" but its very unfortunately kwa kutokusudia,au kwa kukusudia watu kwanzia level za chini hawaambiliki, wanagoma, wamefundishwa na chadema kuwa police hawafanyi kazi kwa ajili ya wananchi wote bali ni "PoLice CCM" refer Dr slaa na baadhi ya makada wa chadema". Dhana ya nguvu ya umma imekuwa mob justice ndio maana hata hapa JF, mashabiki na makada wa chadema wamefurahishwa na mauaji ya ndugu Mabina.

Naendelea kulaani, watu, vikundi ambavyo badala ya kupinga tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi wanaunga mkono na kuiita hiyo ndiyo nguvu ya umma.

Wito wangu kwa jeshi la police ni kufanya kazi kwa umakini bila upendeleo, na ihakikishe watu wote waliohusika katika tukio la leo wanakamatwa na wanapelekwa mbele ya vyombo vya sheria.

Mob justice ni jambo la hatari,linashababisha vurugu,mauaji linahitaji ufumbuzi wa haraka sana.

Sixgates
Dsm
 
Mbona yeye mabina kajichulia sheris mkononi ya kumuua mtoto wa watu...safi sana wananchi...anayeua kwa upanga naye atauawa hivyo hivyo..angeachwa hai asingefanywa lolote zaidi wangemtetea kuwa hajakusudia..Rest in hell mabina
 
Mbona yeye mabina kajichulia sheris mkononi ya kumuua mtoto wa watu...safi sana wananchi...anayeua kwa upanga naye atauawa hivyo hivyo..angeachwa hai asingefanywa lolote zaidi wangemtetea kuwa hajakusudia..Rest in hell mabina

Mkuu hilo tukio pia nalilaani. Lakini nimekuwa specific kuhusu mob justice. Kwamba mabima kaua haininyimi mimi pia kupinga kujichukulia sheria mkonon
 
Nimesema hapo juu kuwa wananchi hawaoni kama haki zinatolewa kwa haki. Mfumo wa mahakama ni dhaifu, haki hazionekani zikitolewa.


Wananchi masikini ndio wengi nchi hii ,mahakamani wanyonge/masikini hawana haki.Viongozi wa kiserikali nao wamewatelekeza na hujinasibisha kwa kauli za mbaya na zilizojaa kejeli .

1-Na mimi nnasema wapigwe tu maana tumechoka-Waziri mkuu Pinda Bungeni

2-Siongei na mbwa nnaongea na mwenye mbwa-Juma Nkhamia Bungeni

3-Liwalo na liwe -Waziri mkuu Pinda ktk mgogoro wa Madaktari

4-Kama bei ya umeme ni ghali basi tumieni vibatari-Agrei Mwandri naibu waziri nishati na madini.

5-Pigeni mbizi -Magufuli akiwaambia wakazi wa Kigamboni

Zipo nyingi wengine wanaweza kuziongezea hapa,tatizo la mfumo huu uliopo sasa yaani chama cha mapinduzi ccm wanafikiri bado wanishi na wananchi wa miaka ya 1960..Tutawahukumu kadiri ya mnavyotuhukumu.
 
Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe (a.k.a too local) alitangaza siku ya civil disobedience. Wafuasi wengi wa Bavicha wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi.

Hata kile kitendo cha Chadema Arusha kuichoma moto ofisi yao kwa lengo la kupata umaarufu wa kisiasa pia ni sehemu ya madhara ya utamaduni huu mpya ulioletwa na Chadema.
 
Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm alifika katika eneo hilo majira ya asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika eneo la milima ya Kanyama ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na wananchi.



Baada ya kufika katika eneo hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na kumhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana baina yake na wananchi.



Baada ya majibishano ya muda mrefu na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina aliamua kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo zilimpiga mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kupoteza maisha.



Taarifa hizo toka katika eneo hilo la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe, mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo.
 
Kumbuka huyo Diwani baada ya kufyatulia watu risasi na hatimaye kuua ndipo hasira zikwawaka wananchi, nayeye akapata haki yake...

Rest in Hell Diwani..


mleta mada angekuja na suluhu badala ya kulaani pekee. Post yako inaonesha kiburi cha marehemu kama walivyo watawala na wenye uwezo wengi. Mimi naamin tatizo hili linaweza kumalizwa kwa wao walio juu kuwa watu wa haki na kuhakikisha mifumo ya utoaji haki inafanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi. Lakini si kwa kutegemea wananchi waache bila mabadiliko toka ngazi za utawala.
 
Mob Justice si sawa.

Lakini pia ubabe na matumizi mabaya ya Silaha za moto sio sawa vile vile.

Sixgates ungekuwa fair na kuhoji "Kilichowasukuma Wanakisesa ni nini"

Justice System ilifanya kazi yake fairly na kwa wakati?

Marehemu na yeye Role yake kwenye hili ni nini??


Japo moshi wa kibatari ni Hatari kwa Afya ya binadam na ni dhana duni ya mwanga, Umeme ukikosekana wiki nzima hauna budi kuwasha Kibatari.


Simtetei yeyote.
 
Mkuu, leo nahibiri habari ya kutojichukulia sheria mkononi. Hiyo ya kuacha dhulma hata wewe mbona unaweza kuifanya.

Hivi kwa nini usiwe unajipa muda mpaka ukiwa na vivid info ndio uanzishe thread?

Yani mtu ameuwa kwa risasi halafu ni diwani bado wananchi wamwache? Mimi nadhani walipaswa kumchoma moto kabisa.
 
hakuna mwenye mamlaka kutwaa uhai wa mtu nadhani wananchi wamechukizwa na mambo mawili kama si zaidi ya hayo; kwanza kitendo cha kujihami na silaha ya moto kasha kuua mtu limechochea hasira mbaya
Pili wananchi tunaona wazi kuna watu watu wako juu ya sheria hasa unapokua na nafasi ndan ya cha ccm,
mtoa uzi amesau kama marehem kajieka juu ya sheria ndo mana kesi iko mahakan yy kaamua kujenga akijua mahakama itakua upande wake
 
Wenye Akili na wanao angalia mbali watakuunga mkono vice versa utatukanwa na kupuuzwa na lile kundi lingine.
 
umeandika vizuri sana lakini umekuja kuharibu ulipoingiza cdm kwenye andiko lako , cdm hawajawahi na wala siyo lengo lao kuhamasisha mauaji , hata wewe unajua , bali kilichomsibu Mabina ni dhuluma , rejea kauli ya kapuya kwenye sakata lake ! Labda nikupe angalizo tu kwamba hiyo lugha yao ' SISI NDIYO WENYE NCHI ' itawateketeza wengi sana .

Mkuu hata nikiangalia historia, hakuna wakati ambao pamekuwa na kujichukulia sheria mkononi kwingi kama kuanzia miaka ya 2000 na kuendelea. Hawa wananchi wamekuwa wakiaminishwa kuwa vyombo vya sheria havifanyi kazi but sio kweli mkuu. Chadema wapo responsible kw kuwa sehem ya upotoshaji.
 
Nyabafuuu kabisa yaani unamtete mhalifu aliye kuwa amea jiandaa kufanya mauaji ya halaiki?
wee unafikiri hao wananchi wa kisesa hawana akili?
Uliona wapi mkulima anaenda shambani kulima na silaha ya moto mkononi?

Kama ni njaa ndo imekufikisha uko ilikofika, sasa umepotoka na pole sana!
 
Hata wewe nguvu ya umma itakufikia hapo ulipo. Ukitaka isi kufikie tenda haki tu. Vinginevyo mtaisoma namba.

Mkuu huko tunakoelekea kama mtaendelea kumsikiliza dkt slaa na mbowe atawapoteza, hizo sumu anazomwaga na kuwaambia policcm,mara mufanye civil disobedience itakuja kuwagharimu
 
Back
Top Bottom