Nguvu ya Umma ilivyookoa majimbo, naomba busara itumike Nchi ibaki salama

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
2,896
2,000
Mwaka 2010 Kama sikosei Wapinzani hasa CHADEMA walidhulumiwa majimbo mengi Sana ya ubunge na pengine udiwani.

Lakini sehemu zote ambazo nguvu ya Umma ilitumika majimbo yaliokolewa
Nitayataja ninayoyakumbuka:

Nyamagana - bila nguvu ya Umma Ezekia Wenje asingekua mbunge

Arusha Mjini- bila nguvu ya Umma God bless Lema asingetangazwa Mshindi.

Ubungo - bila nguvu ya Umma Myika asingetangazwa Mshindi.

Mbeya - bila nguvu ya Umma Sugu asingetangazwa Mshindi.

Iringa Mjini - bila nguvu ya Umma Msigwa asingetangazwa Mshindi.

Kwa uchache na ninayoyakumbuka Ni hayo, Kama Kuna mtu anakumbuka zaidi atuwekee hapa.

Mfano mdogo tu Nyamagana, watu walishaanza kuharibu Mali za serikali ikabidi kwa Busara za RPC wa Mwanza amuamuru mkurugenzi wa Uchaguzi Mwanza kwa kumpa saa moja awe ametangaza matokeo saa moja ikipita ataondoa Polisi wake.

Mkurugenzi kwa kuona hivyo akamtangaza Mshindi halali Bwana Ezekia Wenje wa CHADEMA.
Sehemu nyingine vijana walishaingia mitaani na happy ikawa tete.

Wito wangu kwa watawala na Watu wa Tume,
Tunakwenda kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wenye tensheni kuliko Uchaguzi wowote uliowahi kutokea hapa nchini,
Wagombea wakubwa wawili Wana tabia za kufanana,
Mmoja Ana nguvu ya dola na hakubali kushidwa,na mwingine Ana nguvu ya Umma na hakubali kushindwa,

Hivyo nawaomba watu wa Tume tumieni busara kumtangaza Mshindi alieshinda kihali kwani mtalindwa na Dunia,kuliko kushinikizwa kumtangaza alieshindwa kihalali na nguvu ya Umma ikachukua nafasi yake na dola ikaingilia matokeo yake Ni kuharibu.Na mkishaharibu dunia itawaadhibu.

Enyi watu wa Tume wekeni Haki na mazingira mazuri ya Uchaguzi
Na kutenda Hali,kinyume na hivyo Ni nyinyi wenyewe mtalazimisha matumizi ya nguvu ya Umma,

Msilazimishe matumizi ya nguvu ya Umma kwa kuonea upande mmoja
Ninavyoona safari hi nguvu ya Umma inaenda kuwa nchi nzima
na sio majimbo machache.

Napenda
Amani na ninaipenda Tanzania,Sina mahali pengine pa kuishi zaidi ya Tanzania.
 

Mzee Chayai

Senior Member
Aug 20, 2018
196
500
Ilemela- bila nguvu ya umma Highness Kiwia asingekuwa mbunge 2010
Singida Mashariki - bila nguvu ya umma Tundu Lissu asingeukwaa ubunge
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom