Nguvu ya mwanamke

Japo maisha ni ya thamani kwa kuyakatisha kwa staili hio japo inauma lakin alikosea angevumilia tu waachane tu mwanamke wa hvyo hafai...
ANA ROHO YA KINYAMA SANA HUYO MWANAMKE. NAMWEKA KUNDI MOJA NA WAUAJI. AKAISHI PORINI HUYO MWANAMKE
Duuuuh!!!
 
Habari zenu wapendwa.

Leo kuna jambo limenigusa nikatamani sana kushare nanyi, haswa wanawake wenzangu(haswa wale midomo chuchunge)

Kuna baba ni jirani yangu amejiua baada ya kuhitilafiana na mkewe ( ilani tatizo la kipindi kirefu sana), kwakweli mwanamke ana kelele yule, akianza kumtusi mumewe majirani wooote mtasikia.

Sasa ikatokea mumewe akayumba kidogo kiuchumi, lakini mkewe hakutaka kuelewa na kumtuhumu kuwa ana michepuko(sina hakika kama kweli alikuwa nayo au la), hapo ndipo balaa lilipoanzia.

Mume akaamua kumshirikisha mkewe katika mapato yake, na wakafungua account ya pamoja, mke ndio mara nyingi alikwenda kudeposit pesa, ikatokea mume akapatwa na dharura ya kifamilia(kwao) akahitaji pesa, akamueleza mkewe kuwa anahitaji kiasi fulani cha pesa ili aende kwao, mke akaanza kelele.

Mume akaamua kwenda bank,cha ajabu akakuta account alotegemea ina zaidi ya milioni6 ina laki tu, akarudi kwa hasira na kumuuliza mkewe, akamjibu simple 'usinulize maswali ya kipuuzi',( haya ni maelezo ya rafiki wa mwanamke) ugomvi ulikuwa mkubwa hadi mume akaamua kuondoka nyumbani, na hakurudi mpaka kesho yake ilipofahamika kuwa mwili wake umekutwa nyumba ya wageni akiwa amejiua kwa kunywa sumu.

Jamani wanawake hii midomo yetu ina nini? Ni kwanini hatujifunzi kila siku!!!
Twapaswa kutambua kuwa tuna nguvu kubwa sana dhidi ya hawa wenzetu, mwanamke unauwezo wa kumfanya mwanaume masikini ajisikie na kujiona tajiri, lakini nguvu hiyo hiyo tukiitumia vibaya inaweza haribu kila kitu.

Tuwe basi watu wa kuwapa moyo na kuthamini wanachofanya hawa wenzetu, wanakazi kubwa sana na mzigo mkubwa sana walioubeba katika kuhakikisha tunapata mahitaji na mambo yote yanakuwa sawa. Tuwe faraja yao, tuishi katika misingi ya upendo,kujaliana na kuchukuliana kadiri ya mapungufu yetu.

Tujenge familia bora zenye misingi imara,maana watoto wetu sisi ndio role model wao wa kwanza(hii ni kwa wote wanaume na wanawake). Tusije shangaa watoto baadae wanakuwa watu wa ajabu ajabu kumbe wamerithi kutoka kwetu.

Muwe na usiku mwema.

Ujumbe Bora wa mwaka 2016......Tatizo Wanawake wengi hawalioni hili kabisa...
 
Sijutii weye kuwa shemeji yangu umeandika kwa mpangilio mzuri na hisia za juu kabisa ubarikiwe threads chanya kama hizi ndio zinatakiwa hapa penye uzi huu najiona nipo jf.
 
Back
Top Bottom