Nguvu ya mwanamke kiroho: Ndiye kiumbe pekee aliyekutana na Ibilisi na kuongea naye

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,751
Mfumo dume unamtambua kama kiumbe dhaifu, asiye na nguvu.... Huu ni upotoshaji mkubwa labda nguvu hizi za kimwili na si kiroho....

Namheshimu sana mwanamke hasa asili yake kiroho na in fact naweza kusema namuogopa kwa namna fulani.. Ni huyu pekee aliyeangusha tawala, falme na watu wenye nguvu na umaarufu mkubwa duniani.... Hakuna kiumbe mwenye ushawishi usiokwepeka kama mwanamke... Tumeyaona kwa yule generali mwenye cheo kikubwa hivi karibuni

Adamu pamoja na kuwa kiumbe no moja kuumbwa... Huku ikisemekana pia kuwa aliumbwa sawa na Lilith... Mwanamke jeuri aliyemsumbua sana hata kufikia kumtaliki (talaka ya kwanza OG)

Ni baada ya hapo pengine Mungu akaona pengine si vema kuumba kiumbe kingine bali kitokane na Adam mwenyewe lakini inaelekea kuna mchezo ulifanyika na Lilith kurudi kwa mlango wa nyuma na kuwa Eva/hawa rejea mada hii Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? - JamiiForums
Hawa aliyetokana na mifupa ya Adam hakuwa jeuri na kiburi kama Lilith bali akajaaliwa ushawishi... Lakini pia akakubali kushawishiwa na Ibilisi... Hapa kuna mtanziko kidogo... Lilith kiburi lakini Hawa mshawishi

Hesabu za Ibilisi zilienda vema hata kumdanganya Hawa ale tunda la kati la mti wa ujuzi wa mema na mabaya Kwanini Hawa na si Adam?

Kulikuwa na kizalia kinachofanana kati ya Lilith na Adam hivyo Lilith mtalikiwa asingeweza kumrudia Adam na kumshawishi... Ni kupitia Hawa (anayesemekana pia ni Lilith) Lilith huyo huyo kwa umbo la pili la Ibilisi anapanda mbegu yake kwa Hawa na inakuwa implant ed kwa Adam

Ibilisi akitajwa kama malaika mkuu baada ya Mungu kwa hakika alizifahamu siri nyingi za mbinguni... Kwahiyo alipoasi na kuondoka huko aliondoka na mengi... Sasa kama aliweza kumface Hawa wakapiga story na kufanya naye patano... Huyu si mtu wa mchezo hata kidogo....

Tunisha msuli, tanua mbavu, vimbisha kifua lakini kiboko yako ni mwanamke... Muite majina yote lakini mwisho wa siku kwake huna say
Mwacheni mwanamke aitwe mwanamke... Mwanaume atabaki kuwa mtumwa wake mpaka mwisho.... Kataa kubali

Jr
 

Asipokupata usiku atakupata asubuhi
Akikukosa kwenye chakula atakupata kwenye kilaji
Ukimkimbia kwenye mahusiano mtakutana kwenye dili

Jr
.Hao viumbe wewe acha tu.Tunawaita dhaifu,ila msiki wao tunaucheza haswaa.Ukifikiria tuu pale kati, kwisha habari yako.Undava pembeni,unyonge tatu mzuka.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
.Hao viumbe wewe acha tu.Tunawaita dhaifu,ila msiki wao tunaucheza haswaa.Ukifikiria tuu pale kati, kwisha habari yako.Undava pembeni,unyonge tatu mzuka.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
tapatalk_1553266495242.jpeg


Jr
 
Mshana Jr, Heshima kwako Mkuu
Kwa upande wetu sisi Waislam,Adam aliumbiwa Hawa,na hakuna mwanamke mwengine kama Vitabu vyenu vinavyodai,

Kadhalika
Mama yetu Hawa,hakuwa wa kwanza kula Tunda lililokatazwa kama mtihani kwao,Na wala hakutoa ushawishi huo kama wasemavyo baadhi ya watu(wakiwemo Waislam).
Ila Adam ndio aliemshawishi mke wake Hawa kula Tunda na si vinginevyo

Allah anajua zaidi

Shukran Chief

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom