Nguvu ya mkaa katika kutakasa mwili

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Mkaa (charcoal) ni moja ya tiba isiyotiliwa maanani lakini inathamani katika kuleta uzima na kuuboresha.

kazi ya mwili sio kupokea sumu bali chakula. Lakini kwa bahati mbaya kwa dunia ya sasa vyakula vingi na vinywaji lukuki vinaambatana na sumu hata kama ni viwango vya chini lkn madhara ya muda mrefu ni hakika.

Mkaa unasifa ya pekee. haufyonzi(absorb) sumu au kemikali hatarishi bali unazikamata(adsorb) na kutoka nazo nje kwa njia ya haja kubwa.

jinsi ya kufanya:
saga mkaa weka kwenye glass kiasi cha robo changanya na maji kujaza sehemu iliyobaki kisha kunywa hata mara mbili kwa siku. sio lazima kila siku ila kwa kipindi kifupi tu.

kama ambavyo mkaa hutumika kunyonya dhahabu migodini, utanyonya na kuondoa kemikali hasa heavy metals na kuziondoa. Hapo utakuwa umejiepusha na safari za matibabu india miaka yako ijayo bila gharama.

nimejifunza mahala...
 
Ile Carbon inayotumika Migodini inakua ni Changarawe ndogo ndogo. Sasa kwa idea yako tukisaga si itakua unga! Je unga unga unaweza kukamata chochote?

Otherwise kuna maelekezo hujayaweka!
 
Kipindi fulani nilikuwa natumia kusafishia meno na yalikuwa meupe kweli.
sana tu.
kusafisha meno badala ya kutumia mkaa au dawa ya meno tumia strawberry yale matunda.
kuna chemistry hapo kati ya hilo tunda na ule uchafu mambo ya acid na base. ukifanikiwa unaweza kuendelea na ustaarabu wa kawaida.

God created nature as a healing agent if we disregard some basic natural laws.
 
Ile Carbon inayotumika Migodini inakua ni Changarawe ndogo ndogo.
Sasa kwa idea yako tukisaga si itakua unga! Je unga unga unaweza kukamata chochote?

Otherwise kuna maelekezo hujayaweka!
ni kweli mkuu zile carbon ni kubwa kipenyo ni mm kadhaa nadhani. lkn zile nadhani zimekuwa customized kwa kukamata dhahabu kwa msaada wa kemikali nyingine na kwa kiwango flani (mfani NaCN) na LIME kwa ajili ya kumaintain PH inayitakiwa.

na dhani kusagwa kumeangalia mazingira ya tumbo la mwanadamu na chemistry yake mkuu.
ila hiyo form ya carbon hasa natural mkaa uliosagwa ndio ilikuwa recommendation ya hiyo rejea.
 
anhaa..vipi hamna madhara
Mkaa wa mti gani? Au wowote tu?? Vp kuhusu madhara yoyote
mkaa umekuwa ukitumika kwa maelfu ya miaka kama tiba asilia bila kuwa na record ya kuleta madhara. unaweza kukumbuka hata tukiwa watoto tulikula mikaa bila madhara yoyote.

Mkaa umekuwa rated category 1 na Food and Drug Administration FDA ya US kuwa ni salama na unafaa. kwa tfda au taasisi za tiba asilia bongo sifahamu.

mkaa unakuwa recommended na vyanzo ya uhakika vya kuondoa sumu mwilini kama Poison Control Centers,Padiatric and Toxicologist associations...

mwenyewe nimetumia sioni madhara yoyote.
 
una kunywa na mkaa wote?
ndio huo ndio unaotakiwa...
kuondoa wasiwasi kuna makampuni duniani wanatengeneza mikaa maalumu "activated charcoal" na kuusaga kuongezq adsobility yake hadi mara 100 ya mkaa wa kawaida kwa kuufanya kuwa ungaunga na kuuza kwa maelfu ya shilingi.

kitu hicho unaweza kukifanya mwenyewe nyumbani. hapa nimetoa simple home remedy. hata kama mtu kanywa sumu baada ya kutapishwa saga mkaa nusu kikombe jaza maji mnyweshe wote, utakomba sumusumu zote zikizobakia.
 
ni kweli mkuu zile carbon ni kubwa kipenyo ni mm kadhaa nadhani.
lkn zile nadhani zimekuwa customized kwa kukamata dhahabu kwa msaada wa kemikali nyingine na kwa kiwango flani (mfani NaCN) na LIME kwa ajili ya kumaintain PH inayitakiwa...
OK, na inatakiwa Powder kabisa au Chengachenga?
 
Kila mtu ni mtaalamu siku hizi atii...
Kuna somo naliandaa, ntawafunza jinsi mavi ya mbuni na mkojo wa mbuzi ilivyo na nguvu...
unaandaa kwa sababu kila mtu siku hizi anajifanya mtaalam au kwa sababu unakitu unataka kushare na jamii ndugu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom