Nguvu ya mafisadi na majangili yadhihiri

Mwanamume

Senior Member
Jan 3, 2013
185
225
Ndg zangu wanaJF kujiuzuru kwa mawaziri 4 ni njama na mbinu chafu ya mafisadi ambayo yanatekeleza ujangili. Mbinu hii imeandaliwa kwa ufundi mkubwa sana na lengo lake ilikuwa kumuondoa Kagasheki peke yake lkn ni bahati mbaya tu kwamba imewagusa na hao mawaziri wengine 3. Kagasheki alionekana mwiba kwa majangili haya yenye mtandao na ushawishi mkubwa mpk kwa rais.
Kilichofanyika ni kumuingiza rais ktk mtego huu kwa kumpa ushauri wa kuendesha operesheni tokomeza ujangili huku wakijipanga kuitekeleza kinyume na haki za binadamu. Wakafanya mateso dhidi ya raia wasio na hatia mbele ya kadamnasi na kwa makusudi wakarekodi video, wakapiga picha na kukusanya kila aina yavielelezo vya wanayoyafanya kwa kuwatumia watendaji ktk ngazi mbalimbali. Walijua muda ukifika watatumia vielelezo hivyo kumrudi Kagasheki kwa mgongo wa ukiukwaji wa haki za binadamu. Sote tu mashahidi, Kagasheki kalalamika sana kuwa mtandao unatisha na dhahiri hakupata hata chembe ya ushirikiano.

Basi wakati umefika mafisadi hao wamewanunua/kuwaghiribu wabunge kwa kuwapa picha na ushahidi uaoonyesha mateso ya raia ambazo wamezipiga ama kuzirekodi wenyewe toka kwa raia waliowatesa wenyewe ili kumsurubu Kagasheki. Hatimaye wamefanikiwa. Hebu tujiulize kati ya operesheni tokomeza na operesheni kimbunga ni ipi imetesa raia sana. Bila shaka ni kimbunga lkn kwann tokomeza ndiyo iwe na ushahidi mwingi sana na kupigiwa kelele sana? Mafisadi yana maslahi huko. Nchimbi alipaswa kujiuzuru tangu vifo vya mapadri wa Zanzibar, milipuko ya mabomu Arusha na vurugu za Mtwara ama kifo cha Mwangosi.
Huyu wa ulinzi alipaswa kujiuzuru tangu mabomu ya Mbagala na baadaye yale ya Gongolamboto. Kwann leo? Hili limegusa maslahi ya mafisadi majangili. Naomba kuwasilisha.
 

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
1,846
2,000
Mbona hukusema kabla au tukio limekupa stori

Mch.Msingwa,"Hatuwezi tumia fikra zilezile zilizoshindwa kutatua tatizo tunahitaji fikra mpya zaidi ya zile

Ssm bana wakishindwa stori
 

Mwanamume

Senior Member
Jan 3, 2013
185
225
Siyo stori na hoja siyo mm kusema kabla nataka wanaJF tufikirie nje ya kinachoonekana kutendeka sasa. Karibuni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom