Nguvu ya mafisadi na majangili yadhihiri

Mwanamume

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
262
190
Ndg zangu wanaJF kujiuzuru kwa mawaziri 4 ni njama na mbinu chafu ya mafisadi ambayo yanatekeleza ujangili. Mbinu hii imeandaliwa kwa ufundi mkubwa sana na lengo lake ilikuwa kumuondoa Kagasheki peke yake lkn ni bahati mbaya tu kwamba imewagusa na hao mawaziri wengine 3. Kagasheki alionekana mwiba kwa majangili haya yenye mtandao na ushawishi mkubwa mpk kwa rais.
Kilichofanyika ni kumuingiza rais ktk mtego huu kwa kumpa ushauri wa kuendesha operesheni tokomeza ujangili huku wakijipanga kuitekeleza kinyume na haki za binadamu. Wakafanya mateso dhidi ya raia wasio na hatia mbele ya kadamnasi na kwa makusudi wakarekodi video, wakapiga picha na kukusanya kila aina yavielelezo vya wanayoyafanya kwa kuwatumia watendaji ktk ngazi mbalimbali. Walijua muda ukifika watatumia vielelezo hivyo kumrudi Kagasheki kwa mgongo wa ukiukwaji wa haki za binadamu. Sote tu mashahidi, Kagasheki kalalamika sana kuwa mtandao unatisha na dhahiri hakupata hata chembe ya ushirikiano.

Basi wakati umefika mafisadi hao wamewanunua/kuwaghiribu wabunge kwa kuwapa picha na ushahidi uaoonyesha mateso ya raia ambazo wamezipiga ama kuzirekodi wenyewe toka kwa raia waliowatesa wenyewe ili kumsurubu Kagasheki. Hatimaye wamefanikiwa. Hebu tujiulize kati ya operesheni tokomeza na operesheni kimbunga ni ipi imetesa raia sana. Bila shaka ni kimbunga lkn kwann tokomeza ndiyo iwe na ushahidi mwingi sana na kupigiwa kelele sana? Mafisadi yana maslahi huko. Nchimbi alipaswa kujiuzuru tangu vifo vya mapadri wa Zanzibar, milipuko ya mabomu Arusha na vurugu za Mtwara ama kifo cha Mwangosi.
Huyu wa ulinzi alipaswa kujiuzuru tangu mabomu ya Mbagala na baadaye yale ya Gongolamboto. Kwann leo? Hili limegusa maslahi ya mafisadi majangili. Naomba kuwasilisha.
 
Uadilifu wa wabunge wetu unatia shaka hata taarifa zao si ajabu zikatolewa ili kuwafurahisha watu maalum na wanufaika wakawa ni hawa wabunge. Wiki hii tumeambiwa wabunge wamepewa posho ya safari wawakazila bila kusafiri.
 
Lini hii MIzigo aka CCM aka magamba watakubali kuwa wamechoka, wananuka uovu kwa kiasi hata wao hawajui tofauti zao.Nani muovu nani ni mwema.Hii ndio shida ,ndio maana wote huona wamonea,hata el.alisema shid ani uwaziri mkuu na tuu..
 
Kwa siasa yetu hii, siamini ka tutakuja pata waziri makini.
kama leo Kagasheki ameonekana hafai...!!
Tumezoea unafiki leo Kagasheki akifa ndo utasikia sifa kem kem jinsi alivyokuwa mtendaji mzuri.
 
I thought Nchimbi is among them? Kilichofanyika hapa; kwa sehemu ni ushindi wa mafisadi na mwendelezo wa wizi meno ya tembo. Tunabili kitakochofuata tuwe na maelezo sahihi.
 
Kagasheki ni Jembe nitamheshim daima milele,nakuunga mkono kaka Majangili wana nguvu sana.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
...wakiunganisha na mizigo ya kinana iliyosalia si atabaki waziri mmoja tu..?!!
 
Kagasheki kachinjiwa baharini tu.Hii nchi kuna watu wanataka watumikiwe wao tu.
 
Mafisadi wapo njamani..kagasheki amejitahidi sana katika kukamata majangili na hisi ilikuwa mbinu ya kumtoa tu.
 
Maporini hali si shwari. Na alichokuwa akifanya Balozi Kagasheki ni kuokoa kilichosalia akiangalia tulikotoka na tunakoenda. Sasa majangiri nyangumi wamemzidi kete ,watanzania tutegemee meno ya tembo kuuzwa mtaani kama karanga halafu tutaandika historia nzuri ya hawa wanyama wakubwa wa nchi kavu kwamba waliwahi kukanyaga Tanzania na kutoweka. Saivi mapori ya wanyamapori yamegeuka ranch za ng'ombe.
 
Pesa mwanaharamu, acheni tu.

Umenena kweli. Pesa ni Mwanaharamu. Kwa kutumia pesa huyu huyu Hamis Kagasheki amefanikiwa kusambaratisha mipango ya kuendeleza manispaa ya Bukoba kwa kuwahonga madiwani shilingi laki moja kila kinapopangwa kikao cha baraza la madiwani kiasi ambacho ni mara mbili ya kiasi wanachopaswa kulipwa iwapo watahudhuria kikao. Ndipo hapo watu wazima kama mzee Ngalinda naibu mayor wanapanga foreni kwa Kagasheki kulamba laki moja huku Mipango ya kuendeleza manispaa ikikwama. Kagasheki ni Mnafiki hacha akumbwe na yaliyomkumba. Inaweza kuonekana kaonewa sawa lakini pale mtu unapofanya uovu hujui huo uovu utazaa matunda kupitia kona hipi. Nadhani huo ni mwanzo wa mwisho wake.
 
Back
Top Bottom