NGUVU YA KUMKAMATA MCHUNGAJI WA DECI...itumike na kwa mawaziri na viongozi wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NGUVU YA KUMKAMATA MCHUNGAJI WA DECI...itumike na kwa mawaziri na viongozi wengine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana wa Mungu, Apr 22, 2009.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nguvu iliyotumika kumkamata mchungaji wa DECI majuzi, iliniumiza sana, mtumishi wa Mungu, mtu anayesimamia makanisa vile, halafu akafungwa pingu wakati hajaleta upinzani wowote, wala hajatoa dalili ya kupingwa kukamatwa, ilikuwa ni ya kupindukia.

  Mimi sio polisi, ninaweza nikasema kuwa, kama polisi waliona ni bora kufanya vile, basi sawa, lakini basi nguvu ileile iliyotumika pale, itumike hivyohivyo na kwa mafisadi wengine kama kina mramba na mawaziri wengine wakubwa. hao mawaaziri wengine walikamatwa kwa kusindikizwa, lakini yule mchungaji alikamatwa kwa kupigwa pingu hadharani kama jambazi.

  Mchungaji yule alikuwa pale akiwapa watu mbegu zao, akawa anawatangazia matangazo. polisi wanasema alikuwa anahamasisha fujo, hivi ni fujo gani wana deci wanaweza kuileta? mimi kama mkristo, na wakristo wengine wengi tu mtaani huku, tumechukizwa sana na kitendo kile cha kumdharirisha mchungaji wetu, hata kama mimi sisali kwake, lakini kuna waumini wake wengi wameumizwa na kitendo kile. kama hakukataa kupelekwa polisi, kwanini nguvu ya ziada kama ile itumike? lini tulishasikia hata Shehe mmoja tu amepigwa pingu? mbona kuna fujo nyingi tu zinafanyika misikitini, tena kali, nyingine ni hiyo ya arusha juzi kumzuia mtu wa bakwata. na nyingine nyingi. hivi kulikuwa na umuhimu wa kumfunga pingu mchungaji wa kikristo vile? ni mioyo mingapi ya wakristo imeumia? hatutaki jambo hili lijirudie, mapolisi wawe makini, wasilete hasira zzo binafsi kumaliza machungu yao. kama walikuwa na hasira na wale wachungaji au walikuwa na hasira na wakristo, ni maadui wa wakristo nina maana, wangejiweka wazi ili tujue. ile kitendo kile, hata kama watu hawatasema hadharani kwasababu wakristo ni waoga kuandamana, selikali ijue kuwa, liko linafukuta mioyoni mwa watu. na kuna siku watawajibika, either kwa kupitia kura au kitu kingine chochote ambacho sio violent. asante.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pole sana Mwana wa Mungu kwa maswahibu yanayowakuta viongozi wako. lakini baada ya kusoma maneno yako nimebaki najiuliza, polisi walitumia nguvu kivipi dhidi ya mtu anmbaye hakuleta ubishi? Inawezekanaje kutumia nguvu kumkamata mtu ambaye ametii amri?
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ndo hicho cha ajabu, nafikiri polisi wetu wanatakiwa kwenda shule ya sheria kabla. mtu unasalenda kabisa unakubali kukamatwa, hauna bunduki wana hujui kupigana ile kuhubiri tu, wenyewe wanakutia pingu, ni udhalilishaji sana. lakini hiyo haina shida kwa mchungaji mwenyewe, tatizo liko kwa waumini wa kikristo, wa kanisa lake na hata wale ambao si wa kanisa lake, alimradi tuwawe wakristo. wanahisi kudhalilishwa kwa mchungaji au dini yao. kuna upinzani gani yule jamaa alileta? aliaka kukimbia? kulikuwa na tatizo gani hata nguvu ya aina ile itumike?
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ah kumbe DECI tena?
  haya twende kazi
  ila kama mpaka sasa wapo watu wanasimama vifua mbele na wanatumia jukwaa la IMANI kuhuisha uhalali wa DECI. basi naamini hata wafuasi watakaofuata hiyo njia ni vilaza wa kutupwa. Ninawahurumia watanzania wenzangu wanaoingizwa mkenge na hii style ya utapeli ya kizamani.
  Mwana wa Mungu Zinduka ndugu yangu, mwabudu Mungu wako ktk kweli na amini. Fahamu kuna maono mengine hayatoki juu kama mnavyoaminishwa kuwa DECI ni maono.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa unanichanganya Mwana wa Mungu... unacholalamika ni matumizi ya nguvu (kwa kumfunga pingu?) au kudhalilishwa? Maana, kutokana na post yako nilidhani polisi walimpiga mieleka mchungaji wa watu wakati hakuleta upinzani, kumbe walimfunga pingu tu! Sidhani kama hayo ni matumizi ya nguvu. Lakini, kwamba huo ni udhalilishaji, inategemea vilevile kwani naamini kuwa ni standard operation procedures za polisi kuwatia pingu watuhumiwa wanapowakamata. Otherwise, kama kweli walimpiga mchungaji wakati hakubisha kukamatwa, polisi wetu watakuwa an vituko
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  anachoongelea mwana wa mungu ni sahihi. anacholalamika ni nguvu iliyotumika, ndio maana anasema, yeye hana shinda na kumkamata yule mchungaji, shida yake ni kwamba, nguvu ile itumike vilevile na kwa wengine. kwasababu hapo wameonyesha kama upeleleo fulani. kwa mchungaji yule walipiga pingu, kwa mafisadi wote hakuna hata pingu. hivyo inaonekana kama walikuwa na visa na dini hiyo,dhehebu hilo au wachungaji binafsi.

  hakukuna na umuhimu kumfunga pingu yule mchungaji. ijulikane kuwa, hata kama watu watamwita ni tapeli, bado anao washirika wengi sana katika makanisa yao, na tatizo lao sio kukamatwa, tatizo ni kupigwa pingu. kwani alileta upinzani?kwanini pingu zitumike kwa mchungaji tu,kwanini imeanzia kwake? mimi mwenyewe sikuielewa kabisa ile ishu. mapolisi wangetumia hekima fulani kwasababu yule jamaa hakuwa na upinzani wowote. well, mimi pia nasapoti. kukamatwa kwake mimi sipingi, ninachopinga ni nguvu iliyotumika. haileti picha nzuri kwa wakristo waliowengi kwasababu ilikuwa excessive. ikumbukwe kuwa, suala la dini ni gumu na sensitive sana, vile unavyoelewa wewe sio lazima kila mtu aelewe au aamini hivyo. hata kama anaamini, hadi aje akubaliane na wewe ni muda. hivyo, msiwatukane watu wa deci kuwa hawaelewi,solve prob iliyo mezani, kwanini walitumia nguvu ile kumkamata? alileta upinzani gani?waliweka picha gani pale? mimi pia iliniuma sana. kama hamuelewe jamaa anachoongea, jaribuni kusikiliza radio za dini za kilokole msikie namna watu wanavyopinga hili jambo. poa mwana wa mungu.
   
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tunataka na kina mramba wapigwe pingu.
   
 8. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Tuache kulalamika bila msingi jamani, yaani pingu tu mnalalamika hivyo je angetiwa makofi si mngefikia hata kuandamana? Suala la kuwa yeye ni mchungaji au sheikh si la msingi kwanza nani kakwambia sheria inachagua dini, mi nilidhani unazungumzia jitihada zilizotumika kulishughulikia suala la DECI zingetumika kwa mafisadi kumbe mnazungumzia kula gud time chini ya polisi!!!

  hii post imekaa kidini kabisa yaani kama si uchochezi basi ni kutaka kututenganisha watanzania...tuache tabia hiyo kabisa. Anyway, hii haina maana kuwa post hii haifai bali ni marekebisho machache tu kwa mtazamo wangu, pia imenipa upeo mpya wa kuamini kuwa serikali ikiamua kuwashughulikia mafisadi inaweza "uNLESS NA WAHUSIKA WANA MKONO WAO"
   
 9. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  fiksiman, hujaelewa nini hapo? mbona Ubungoubungo amefafanua vizuri sana. polisi wanatakiwa wawe fair. Kama kanuni au sheria inasema watiwe pingu basi isichague. mafisadi wa EPA wanatayarishiwa executive rooms kule Keko /Segerea mchungaji anatiwa pingu!! polisi wako kwa ajili ya mafisadi au kwa ajili ya usalama wa raia wote?
   
 10. 911

  911 Platinum Member

  #10
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  An open PARADOX in here!
  Inawezekanaje polisi wakatumia nguvu kwa mtu ambaye hakuonyesha kubisha wala vurugu yeyote?Kwa mujibu wa habari za magazetini ni kuwa palikuwa na kupigana mitama katika eneo hilo,au ilikuwa ni chumvi kunogesha habari??
  Hata hivyo si wanasema kuwa uongozi wa DECI umekataza maeneo yao kuwa sehemu za mikutano kwa sasa,that being the case Huyo mtumishi na Mtikila si ni walikaidi agizo hilo.
   
 11. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  .KULETA/kuchochea vurugu si lazima uwe na silaha bali unahamasisha uvunjivu wa amani.KAMA MCHUNGAJI ANAJUA KUWA MAMLAKA ZA DUNIA ZINA WEKWA NA MUNGU NA HIVYO ALITAKIWA KUZITII MAMLAKA HIZO.
  Waziri mkuu alishatangaza kuwa DECI ipo kinyume cha SHERIA ZA NCHI AMBAZO HATA MCHUNGAJI ANATAKIWA KUZITII,PIA MKUU WA POLISI KANDA MAALUM YA DSM ALITANGAZA KUSIWE NA MKUSANYIKO WOWOTE KTK OFISI ZA DECI AU MKUSANYIKO WOWOTE WA WANANCHI KATIKA KUONGELEA DECI KWA SABABU MAMBO YAO YANASHUGHULIKIWA NA SERIKALI.
  Sasa huyu mchungani aliendaje kukusanya watu?Kama wananchi ndio walimlazimisha awaambie hatma ya mbegu zao,kwanini asitoe taarifa polisi?
  Acheni kutumia dini kama kinga ya maovu.
  ....HUENDA POLISI ALIYEMKAMATA ALIKUWA MUISLAM(joke)
   
 12. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huyo Fiksiman anasema eti anataka kugombea urais 2010 !!! Bora niende kituoni kupiga kura ya wabunge tu !!!
   
 13. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi wanaokimbilia maneno kama 'uchochezi' ndio haohao wachochezi wenyewe. Issue ni nyingine kabisa halafu wewe unaleta neno uchochezi, umelitoa wapi kama siyo wewe mchochezi?
   
 14. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima mbele jamani, naomba niwekwe sawa hapa issue ni uzalilishaji kwa mchungaji wa Mungu ama DECI na yaliyomo?
   
 15. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2009
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wabongo bwana....eti DECI...lol!!! forever loving shortcuts to wealth. Anything but hardwork... Let this be a lesson to many more!!!
   
 16. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kama unayosema ni kweli basi tumepotea. Hizo mamlaka unazosema ndizo zinazotuibia na kutuua. Mungu ameweka 'legitimate authorities' na hizi 'legitimate authorities' utendaji wake ni tofauti na hizo mamlaka unazosema wewe.

  Maana hizo mamlaka zako zina'sign dubious contracts' na kutuibia madini yetu, zinapiga raia wasio na hatia na hata wakati mwingine kuwaua kwa kisingizio kuwa hawakutii amri halali. Hivi kwa sheria za Tanzania usipotii amri halali adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa?

  Ni kweli huyo mchungaji hakutendewa haki hata kidogo na hizo mamlaka unazosema. Katika hali ilipofikia ya DECI na kwa vile yeye ni mhusika analazimika kuwaeleza wanachama wake kitu gani wategemee kwani wengi wanaamini wameibia. Kwa hiyo mwenye jibu kwa hao wanachama ni mchungaji ai kiongozi mwingine yeyote anayehusika na DECI na siyo polisi kumzuia.

  Mbona kwa vigogo mafisadi tunaona 'treatment' tofauti? Hii ndiyo issue mleta mada alitaka tuijadili.
   
 17. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwana wa Mungu!
  Huna sababu ya kuwatetea hao matapeli ambao wanajiita Wachungaji labda wewe ni mmoja wao. Ni chui waliovalia ngozi ya kondoo period!

  Wala huna mandate ya kusema mna machungu yapi?
  Kwa hili la DECI nashawishika niungane na yule jamaa anayejiita Mchungaji Chris Mtikila hajasomea popote he is simply a self proclaimed Priest na ni matunda ya ile sera mbovu ya Uhuria aliyoruhusu Mzee Ruksa ya kusajili taasisi za dini kama viosk vya Voda Fasta

  Kwa ujinga wa wadanganyika as usual waliingia mkenge na kuanza kupanda pesa (this is crazy) Yoyote aliyejiunga na DECI kwangu mimi namwaona kama **** wa kutupa and the blame should go to the CCM!

  Hivi hizo pesa za ruzuku MNAZOGAWANA si zingetosha kuchapisha zile Hekaya za Abunuwazi hawa wajinga wakjisomea!

  Angalau wakasoma ile Hekaya ya Sufuria iliyozaa na baadae ikafa! Wangengamua kwamba kila kinachozaa sharti kife then wasingeingia huo mkenge wa maono ya kupanda pesa na zikazaa!
  Polisi na Usalama wa taifa siku hizi wanafanya kazi gani wasilione hilo! Do we really need them ?

  Tunataka maelezo kutoka kwa Kikwete in person kwenye hotuba yake ya kumalizia April japo hazina mvuto as ni copy and paste!

  Mwana wa Mungu don't make any mistake about what I am saying! Hakuna udini the guy you saw is a criminal per se! Usijaribu kuvaa kakofia cha askofu au shehe as a cover alafu ukuleta za kuleta the cops won't take up that nonsence!!

  The bottom line is haya ni madhara ya muda mfupi na mrefu ya upuuzi wa yule Mwinyi aliyelambwa kelbu na Mjukuu wake! Yea I said it laikini hapa jamii mtabisha mpaka majogoo yawike!!!!

  Hao mnataka staha kwa mashehe na wachungaji etc... yatakiwa wote wawe registered minimum qualifications na hiyo yahitaji kuundwa kwa Regulator like SUMATRA!!! CCM mpo au mwangojea watu wafe ndio kuunda tumee??? You like human blood!!

  For all kabla ya kuanzisha mchezo you need a plane field and a set of rule ehee!! You can't change the rules when the game is on!! Kwaherini!!!

   
 18. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Walitakiwa wamtie pingu Chenge aliyekuwa akiendesha gari akiwa amelewa, Kwa Kasi , na pia bima iliyokwisha muda wake aaaam! na kusababisha vifo vya wanawake wawili. Walitakiwa wamtie pingu Rostam kwa kuhusika na ufisadi wa EPA na Richmond, Walitakiwa wamtie pingu Liyumba kwa kuisababishia nchi hasara ya mabilioni kwa ujenzi wa majengo pacha ya Benki kuu, Walitakiwa wamtie pingu Mkapa kwa kuihalalisha nchi kwa mafisadi huku yeye akibariki kazi yao akiwa ikulu, walitakiwa wamtie pingu Yona kwa kuuza madini yetu kwa wawekezaji huku yeye akipata asilimia kumi Khatibu Senkoro ni shahidi na ndiye anayelinda maslahi yake . Walitakiwa watie pingu waliosababisha ajali ya MV Bukoba, Treni. Walitakiwa wamtie pingu Kavishe aliyekuwa PSRC (sijui bado yupo?) aliyehalalisha uuzwaji wa mashirika ya umma kwa shinikizo bila ya tathmini huyu namwambatanisha na Dk Abdallah Kigoda fisadi na mshirikina aliyesahaulika...........List ni ndefu mno.
   
 19. S

  Semjato JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mwana wa Mungu..
  hivi ulijaaliwa kuvuna mbegu zako kweli ndugu yangu?nakumbuka kama uliitetea sana DECI hapa awali,kabla mamlaka hazijaichinjia baharini...anyway,kama huandiki tu kwa maumivu ya kutovuna hicho kitendo cha polisi sio cha kiungwana kabisa..
   
Loading...