Nguvu ya kitanda

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,072
18,258
NGUVU YA KITANDA

Utafiti umeonyesha baadhi ya vitu vilivyosababisha ndoa za babu zetu zidumu ilikuwa babu na bibi kulala pamoja kwenye vitanda, ngozi za wanyama au mikeka yenye ukubwa usiozidi futi 2.5. Umbali wa futi 2.5 uliwawezesha wanandoa kuwa pamoja na kugusana usiku kucha.

Hiyo iliwalazimisha waongee hata kama wamegombana mchana, maana bila kusema sogea huko huwezi kupata nafasi ya kulala. Baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimisha wasameheane hata bila ya kuombana samahani, maana kugusana kule kuliwapa joto lililokuwa linafuta lenyewe makosa yote waliyofanyiana mchana na kuanza upya.

Vitanda vyetu vya 6 x 6 vinakwenda anti-clockwise na kazi iliyokuwa inafanywa na vitanda vya akina babu. Vitanda vyetu havina ubavu wa kufuta makosa ya wanandoa waliyofanyiana mchana. Kila mtu anakuwa kwenye kona ya 6x6 na kujisikia aibu kuanza kumgusa mwenzie, nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenzie wakati kulikuwa na ugomvi? Ngoma inakuwa droo hadi asubuhi na ugomvi ukiwa palepale na kila mtu akijfanya nunda wa kukataa kujishusha kwa kusema samahani ama kumpapasa mwingine.

Rudisheni vitanda vyenu kwa fundi seremala avipunguze viwe 3 x 6 ili viweze kuwasuluhisha wanandoa mnapokoseana sio kwenda kwa mshenga, shoga, wazazi, majirani kutafuta suluhu.

Nimekopi kutoka sehemu siyo maneno yangu

NDOA MARIDHAWA
 
Tabutupu ni mazingira gani uliyoyaongelea? Maana hata miji mikubwa kama Dar na Mwanza ni wachache wenye kulala kwenye kitanda cha 6 kwa 6.

Pengine kauli hii ingekuwa na mashiko kama ingetolewa kwenye group la what'sap ambalo members wake wengi wana ahueni ya maisha.
 
Kuna wengine tunalala kama wapiga mbizi au ngozi imeanikwa. Sasa vitanda vidogo si mke atakosa pa kulala?
 
Mkuu wengi wetu hapa kwa mwendokasi/kiongozi mkuu wa mk..., vyumba vyetu ni mita tatu kwa mbili na nusu, sasa hizo futi sita ni kwa Mkoa gani !?
 
Tabutupu ni mazingira gani uliyoyaongelea? Maana hata miji mikubwa kama Dar na Mwanza ni wachache wenye kulala kwenye kitanda cha 6 kwa 6.

Pengine kauli hii ingekuwa na mashiko kama ingetolewa kwenye group la what'sap ambalo members wake wengi wana ahueni ya maisha.
Vitanda vya wanandoa in 5x6 6 x 6.

Jaribu Sikh 3x6 uone ndoa itakavyo dumu
 
wakati wa kulala ugomvi unawekwa Pause (poo) tukiamka ugomvi unarudishwa!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom