Nguvu ya Dola Haishindi Nguvu ya Umma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
NGUVU YA DOLA HAISHINDI NGUVU YA UMMA ISIPOKUWA TU PALE WANANCHI HAWAJAELIMISHWA JUU YA UENDESHWAJI WA SERIKALI.

Naomba kuutumia ukurasa wangu kushiriki pamoja katika kusoma andiko hili(article) na kutafakari kwa pamoja na figisufigisu za uchaguzi wa mameya na wenyeviti katika manispaa zetu na Halmashauri za wilaya.

Ukifuatilia matukio yote ya chaguzi hizi za mameya na wenyeviti, ni ukweli usiopingika na usio na kificho kwamba serikali ya CCM inavunja katiba kwa makusudi pale ambapo Serikali hii inaelekeza matumizi makubwa ya nguvu za dola ikiwemo polisi na usalama wa taifa ili tu kukibeba chama tawala cha CCM.

Leo hii hapa Tanzania, polisi wanapokea order kutoka kwa viongozi wa ccm kwa ajili ya kufanya ufanya udhalilishaji, usumbufu, kupiga viongozi wa vyama vya upinzani na wanachama wao, leo hii polisi wamedhihirika ni sehemu ya CCM kwa matendo yao, ikiwemo kutokutenda haki, kuingilia vikao vya wana siasa kwa kivuli cha kutuliza ghasia, kusema kwa niaba ya ccm, na vitendo vya kutowakamata wahalifu wote wanaotokana na CCM, mfano RAS alivyosoma zuio la kughushi kwenye uchaguzi ulioahirishwa wa Meya jijini Dar, na hata kusababisha vurugu., mauaji ya Mawazo Alphonce ,Mauaji ya Mbwambo nk.
Yote hayo na mengine yamelifanya jeshi la polisi litizamike kichama zaidi na sasa linaitwa Policcm.

Aidha haya yote yanawezekana tu kwa kuwa CCM na vyombo vya dola, ambapo viongozi wengi wa ngazi za juu waliingia polisi na vyombo vingine kwa kupitia ccm, miaka ile ilipokuwa moja ya kigezo cha kupata ajira, wameendelea kujidanganya kwamba nguvu ya dola inashinda nguvu ya Umma.

Ninavyoamini mimi na kwa kuangalia mifano ya nchi nyingi duniani, sijawahi kuona wala kusikia nguvu ya dola imeshinda nguvu ya Umma, hapa kwetu Tanzania ni suala la Muda tu. ....haya yanamwisho. ...lazima yatapungua kama sio kuisha kabisa.

Ukiisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, sura ya nane (8) kuhusu madaraka ya Umma, ibara ya 145 (1) na ibara 146 (1) na kifungu cha 2(c) utaona jinsi serikali ya CCM inavyovunja katiba ya nchi. .

Maana serikali za mitaa zipo kwa utashi wa katiba na si utashi wa UKAWA, na suala la kuimarisha demokrasia hapo ccm wamefeli vibaya. ..

Mwisho wa matumizi ya dola kwa kudhani ina nguvu kuliko umma utashi tu pale ;

1:Wananchi wataelimishwa vya kutosha juu ya Madhumuni ya kuwepo kwa serikali ya Mitaa, kwamba ni KUPELEKA MADARAKA KWA WANANCHI AMBAO NDIO CHIMBUKO LA MAMLAKA YOTE KATIKA NCHI YETU.

2:Wananchi wataelimishwa vya kutosha juu ya Uendeshaji wa serikali za mitaa katika ngazi za Kitongoji, Kijiji, na Mitaa

3:Dhana ya ugatuzi wa madaraka kisiasa (Political devolution) ambayo maamuzi ya wananchi kupitia uchaguzi huru na wa haki yanaamua na kuweka viongozi wao wa kisiasa watakaowaongoza katika ngazi mbali mbali ikiwemo mitaa/Kijiji, Kata na majimbo.

4:Wananchi wataelimishwa vya kutosha juu ya Matumizi ya fedha za Umma (Ambapo kimsingi ni Fedha zao zinazotokana na kodi mbali mbali, michango na mapato kutokana na rasilimali za nchi, ikiwemo gas, dhahabu, Almasi, Tanzanite nk, mbuga za wanyama, bahari, mito maziwa, milima nk)

5:Wananchi wataelimishwa vya kutosha juu ya Haki na Wajibu muhimu, kama ilivyoanishwa na katiba ya nchi sehemu ya 3 ya sura ya kwanza (1).

VYAMA VYA UPINZANI HASA UKAWA (CHADEMA NA WASHIRIKA WAKE)

NASHAURI:
Vyama vya Upinzani hususan ni UKAWA wajielekeze kwenye kutoa elimu ya mambo niliyoyabaini mimi kwamba yatasaidia sana katika kupata uungwaji mkono katika mapambano ya nguvu ya dola inayotumika kukandamiza katiba, kuwakandamiza wapinzani hasa ukawa, kukandamiza haki za binadamu, dhidi ya Umma, kukandamiza uhuru wao wa kuchagua viongozi wanaowataka na uonevu mwingine unaoendelea hapa nchini.

Kwa nchi zenye uelewa mkubwa wa wananchi wake juu ya niliyoyataja, hili la kamata kamata ya polisi kwa wabunge, madiwani na wanachama wa Chadema, lisingefanyika, hili la kulazimisha meya jijini Tanga ambako madiwani na viongozi wa CUF kuishia kukamatwa nalo lisingefanyika. ..kutaja kwa uchache.

Maana mchakato wa kumpata Meya au mwenyekiti wa halmashauri, unaanzia kwenye uchaguzi mkuu, ambako wananchi wanakuwa wameshafanya uamuzi, chaguzi hizi za mameya na wenyeviti kimsingi ni formalities tu katika mazingira ya siasa za Africa hasa Tanzania. ..na kura ni namba hivyo pale wananchi wanapokuwa walishachagua madiwani na wabunge wengi kupitia Ukawa, maana yake walishachagua meya au mwenyekiti. ..Lkn hili CCM hawataki, na polisi hawataki.

KUHUSU UENDESHWAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI YA MTAA KATIKA NGAZI YA KITONGOJI, KIJIJI NA MTAA.

Tuangalie mfano mmoja wa Upitishaji wa bajeti za Manispaa na Halmashauri kwenye Full Council.

● Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani tayari Baraza la Madiwani limepitisha bajeti ya Halmashauri zaidi ya shilingi billion 4 kwa mwaka 2016/17(Gazeti la Guardian Feb 27,2016)

●Halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma , Baraza la Madiwani wamepitisha bilioni 27.32 kwa mwaka 2016/17 (Gazeti la Mtanzania, March 1,2016)

●Manispaa ya Kigoma-Ujiji nao tayari wamepitisha bajeti hii iko chini ya ACT wazalendo.

●Bariadi mkoani Simiyu nao walishaanza mchakato japo mkuu wa wilaya aliusitisha kikao hicho (Mtanzania ya 2 7 Feb, 2016) Sina updates kama uliendelea hoja hapa ni mchakato kufikia ngazi ya baraza la madiwani.

Ukienda kote huko kwenye vijiji na Mitaa ukawauliza wananchi kama walishirikishwa, sidhani kama utakuta na na kitongoji, kijiji wala mtaa ambao wananchi wake walishirikishwa kwenye mchakato wa bajeti.

Kwa utaratibu wa Mfumo Shirikishi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (Opportunities and Objections For Development) almaarufu kama O and OD planing process, mchakato wa mpango na bajeti kwa vijijini unaanzia ngazi ya Vitongoji, kisha Kijiji halafu Kata kupitia Kamati ya Maendeleo ya Kata KMK au WDC halafu Mchakato huo unaelewa kwenye ngazi ya Halmashauri. Kwa Mjini unaanzia Mtaa halafu Kata halafu Manispaa.

Na hii ni kwa sababu mchakato wa mpango na bajeti ni wa wananchi kwa fedha zao za Jasho lao na hivyo kwa kuwa ni matatizo yao, ni kwa mahitaji yao wanaohitaji kwenye maisha yao ya kila siku, ndio maana wao ni wadau wakubwa wa mipango na bajeti katika maeneo yao.

Fedha za Serikali ya Mtaa zinapaswa kusimamiwa kwa kutumia makisio na vitabu vya mahesabu...hivyo wananchi wanaposhiriki kunawapa nafasi ya kujua
1.Makisio, hii ni mapato na matumizi na yanaidhinishwa na vikao vya juu vya kijiji, kitongoji au Mtaa.

1:Mapato ya ndani haya hutokana na fedha kutoka kwa wananchi ikiwemo
-Ushuru wa mazao
-Yatokanayo na Biashara au huduma
-Ushuru na ada mbalimbali
-Michango mbalimbali iliyokubaliwa na kijiji au Mtaa
-Sehemu ya mapato ya Halmashauri yanayoachiwa kijiji, kitongoji au Mtaa

2:Mapato kutoka nje ambayo ni pamoja na;
-Ruzuku kutoka Halmashauri
-Mkopo kutoka taasisi ya Fedha
-Msaada kutoka mashirika ya hiari

Yote hayo yanahitaji ushirikishwaji wananchi kwenye kuandaa bajeti (Budget Participatory process,ikiwemo maandalizi ya bajeti, bajeti kupitishwa, bajeti kuangaliwa upya (budget Review,Wananchi kushirikishwa kwenye kusimamia matumizi ya bajeti (budget expenditure) na kwenye kutahimini thamani ya fedha katika matumizi ya bajeti hiyo.

Wananchi kwa kutambua changamoto zao wanatakiwa watambue mahitaji yao ya kijamii ikiwemo, huduma za afya, Maji, Shule, Barabara, madaraja madogo, Soko, pamoja na mambo mengine.

Sasa kwa mifano ya Halmashauri nilizozitaja na Manispaa, wananchi najua hawajajengewa uwezo wa kuhoji, kudadisi, kukosoa, kukubali au kukataa taarifa na mapendekezo ambayo hayatokani na maamuzi yao, Ni kinyume cha utaratibu na sheria kutokuwashirikisha wananchi kupanga, kusimamia, kutahimini na kuhoji matokeo ya miradi yote katika Vitongoji, Vijiji na Mitaa ambayo haitokani na wao kushiriki katika kupanga.

Andiko hili linalenga kuwajengea uwezo wananchi kuyatambua niliyoyainisha hapo juu na nimeelezea kidogo kwa mifano ya halmashauri na Manispaa kupitisha bajeti pasina ushiriki wa wananchi.

Endapo wananchi wataelimishwa yote haya itakuwa rahisi kushindana na nguvu ya dola inayotumiwa na CCM kudidimiza maendeleo, nguvu ya dola ikitumika kuwanyonya wananchi kupitia ukiukwaji wa mipango ya Uendeshaji wa serikali za mitaa, ama kwa kuwachagulia viongozi kinyume na uamuzi wao kupitia sanduku la kura.

Ukawa wajikite kuwajengea uwezo wananchi wa kusikia uchungu wa fedha zao zinazotokana na mapato niliyoyaeleza hapo juu, waelezwe wananchi namna yao ya kushiriki kupanga matumizi.

Wakielimishwa wananchi vya kutosha watakuwa tayari kushiriki ipasavyo kwenye vita ya dola dhidi ya nguvu ya Umma kwenye maamuzi ya wananchi kupitia uchaguzi, iwe wa Rais, wabunge, madiwani, mameya nk na mwisho watashiriki vema kwenye kupanga mipango na kuanisha vipaumbele vyao badala ya kupangiwa.

Nitaendelea wakati mwingine.

Kwilasa E
 
Back
Top Bottom