Nguvu ya CHADEMA yamwondoa DC Fatuma Kimario wa Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya CHADEMA yamwondoa DC Fatuma Kimario wa Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jun 29, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete, amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Kimario kimya kimya.
  Habari za kuaminika zilizopatikana jana kutoka Igunga mkoani Tabora na Kisarawe mkoani Pwani, zinasema Kimario amehamishwa wiki mbili zilizopita.

  Itakumbukwa siku moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutangaza majina ya wakuu wa wilaya wapya, Kimario aliiambia MTANZANIA kuwa yuko tayari kuacha kazi, baada ya Rais Kikwete kushindwa kumhamisha kituo cha kazi pamoja na kukumbwa na matatizo lukuki wilayani humo.

  Alisema angeweza kukataa uteuzi huo, kutokana na kupata vitisho vingi, vikiwemo vya kuandikiwa barua za vitisho, kutumiwa ujumbe mfupi wa simu za mkononi (Sms) na kutukanwa kila anapokwenda kushiriki kazi za ujenzi wa taifa, hasa anapoitisha mikutano ya kujadili kero zinazokabili wananchi.

  Alisema kuteuliwa kwake, kulionyesha wazi namna Rais anavyomwamini katika utendaji kazi, lakini si kuendelea kufanya kazi katika Wilaya ya Igunga.

  Chanzo hicho, kilisema Kimario amehamishiwa katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, kuchukua nafasi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu, ambaye amehamishiwa Igunga.

  "Ni kweli ndugu yangu, Rais amemhamisha kimya kimya Mkuu wa Wilaya yetu, Fatuma Kimario kwenda Kisarawe, hii inatokana na DC huyu kutokuwa na uhusiano mzuri na wananchi.

  "Amehamishiwa Kisarawe, hapa tumeletewa DC anaitwa Elibariki Kingu kama wiki mbili zilizopita, tunaona ameanza kazi ya kutembelea maeneo mbalimbali kama sehemu ya kujifunza na kutambua mazingira ya Igunga.

  "Unajua kuhamishwa kwa Kimario kumetokana na mambo mengi mno, siku zote ambazo amekaa hapa, amekuwa na uhusiano mbaya na wananchi, alishindwa kujitokeza hadharani kutatua kero zao, utakumbuka baada ya tukio lililowahi kutokea katika kijiji cha Isakamaliwa wakati wa uchaguzi mdogo, alipigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alipoteza kabisa mvuto kwa wananchi.

  "Kama unakumbuka vizuri lile tukio la Isakamaliwa, lilikuwa ni doa kubwa mno kwake, alipoteza mvuto baada ya kukutwa akiendesha kikao cha siri na watendaji wa vijiji, kata, tarafa na wazee maarufu kwa lengo la kuchafua mkutano wa Chadema." alisema.

  Itakumbukwa katika tukio hilo, alibebwa mzobemzobe na wafuasi wa Chadema, huku watendaji wakiambulia kipigo.

  Kimario, alikutwa na gari lenye namba STK 38O6 ambako alitiwa misukosuko mingi hadi kufikia hatua ya kuomba maji ya kunywa.

  Itakumbukwa katika tukio hilo, wabunge wawili wa Chadema, Slyvester Kasulumbai (Maswa Mashariki) na Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga, walikamatwa na kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, kwa madai ya kumdhalilisha kwa kumvua hijabu kinyume na misingi ya dini ya Kiislamu.


  Source: Mtanzania Ijumaa
   
 2. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RAIS amebadili Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wengi sio wa Igunga Peke yake. Na huko Pia NGUVU YA PEOPLES POWER?

  BIASED ARTICLE
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Nani wengine wameamishwa kwenye batch moja na kimario?
   
 4. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KAMA INGEKUWA NGUVU YA CHADEMA; uhamisho ungefanyika siku nyingi. Ni uhamisho wa KAWAIDA. Watu wanapenda ku conclude wanavyotaka. Ndio maana kichapo cha Dkt Olimboka wanasema ni Serikali

   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Wewe tuongelee hili la Kimario hilo la ulimboka hata watoto wa chekechea wanajua serikali imehusika.
   
 6. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wee mwendawazimu, jibu swali la Sangarara. Hivi Magamba hata shule mlienda kweli? Na wewe ukafaulu vizuri kama Mchumi wenu mwenye daraja la Kwanza huku Tanzania ina inflation ya karibia 20%? Ama kweli heri shetani kuliko anayetetea serikali ya Magamba!
   
 7. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUJUA ni Tofauti na KUDHANI

  Sasa kama wewe unaendeleza DHANA poa.

   
 8. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Teteeni mpendavyo, lakini kweli alikuwa na mahusiano mabaya na wale anaowaongoza, hana mvuto asingeweza kuendelea kuwa mkuu wa wilaya ile maana tayari alijipakaza kinyesi mwili mzima na kilinuka kila anapotembea hata watu wake hawakutaka kumwona wala kumsikia. Mnamtetea nini, iwe kwa ajili ya CHADEMA au kwa ajili ya kuwa mboga za watu anajua mwenyewe, lakini cha moto amekiona Igunga. Walinyang'anya uhuru wa watu kuchagua wabunge wao wakatumia hila, ngojea 2015. Mimi sishabikii chama chochote na wala sina haja ya kujiunga na chama chochote sababu naangalia mtu anayefaa kama mtu kuwa kiongozi bila kujali chama.
   
 9. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Infaltion ni UJINGA WA WADAU KUKAA KIMYA Walipopandisha bei ya Umeme kwa takriban 50%; na EWURA CCC walibariki; mimi kwa hilo siwaelewi. Na hivi jana Mkurugenzi wa BoT anasema eti wame revise tarehe ya kuwa na single digit rate kuwa June 2013. Huu ni UTUMBO. Economic Management haifanyiki hivo. Na mimi nishasema sana kuhusu hilo humu.

  Turudi IGUNGA.

  Uhamisho ulikuwa wa KAWAIDA na sio nguvu ya CHADEMA; kwanini tusikae kimya kuliko kusema jambo kwa dhana tu; tena dhana binafsi?

   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Sikujua kama najihusisha nawasira. kwaheri
   
 11. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haumwezi kuwa uhamisho wa kawaida huo, uhamisho gani ndani ya miezi miwili (2) tangu walipoteuliwa? Maana katika kipindi hicho ni vigumu hata kupima utendaji wa mtu, lazima kuna external force katika hilo.
   
 12. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe wacha fixi

  Huyu DC alikuwa Igunga kabla ya kujiuzulu Rostam

  Usikurupuke kama uliebanwa na haja ya kwenda choo

   
 13. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,097
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hapa ntapata BAN, Wacha niwe mtazamaji!
   
 14. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sikiliza Makame, najua alikuwepo tokea kipindi kile cha uchaguzi lakini kama ni kumuhamisha wangefanya hivyo miez miwili ilopita wakat wamewatangaza wapya. kufanya sasa hivi, tena ndani ya kipindi kifupi sio maamuz yao ya kawaida, lazma kuna pressure flani!!
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Naona Pro-Chadema JF wameamua kujifariji na kujiliwaza...Rais kafanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya karibia mikoa yote sasa cha kuchekesha Chadema wamechukuwa jina la Mkuu wa Wilaya moja na kutanganza eti ni nguvu ya umma.
   
 16. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  President's Jurisdiction;
  Pressure kwa Waziri sawa; sio DC. DC ni mtu mdogo sana kwa Rais.

  Besides; Kikwete would not give a damn, yeye hagombei tena; 2015 anaishia zake!
   
 17. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama isingukuwa nguvu ya CDM angebadili baraza la mawaziri?!??!?
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Why fighting CDM inaleta sad ending?
  -Mudhihiri na Zitto.
  - CUF
  -NCCR
  -CCM.
  -MKAPA
  -Wassira
  -Jaji wa Lema.
  -Mama Kimario.
  -Now upepo haumwendei PM-ingawa bado hajabadili tabia ya kuwafunda wabunge kabla ya vikao ili wakapambane na CDM.
  -Mukama kuumbuka ktk msiba wa Bob na uzushi wa ukanda na udini.(CDM INA NGUVU MBEYA NA MWANZA KULIKO ARUSHA NA MOSHI)

  -etc
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Hajaanza hata day care, sasa masomo magumu ya chekechea atayajulia wapi?
   
 20. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145

  You are fighting with WEAK

  Lets play a game!!!!
  CDM ni chama cha Wachaga na Wakristu
  LEMA ni kilaza
  ZITO ananyanyaswa kwa sababu si wa aina yenu

  Tuanze hapo!!!!!
   
Loading...