Nguvu umma yamtesa Pinda Mwanza, azomewa, awa mbogo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu umma yamtesa Pinda Mwanza, azomewa, awa mbogo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WOWOWO, Sep 18, 2012.

 1. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza kwa muda kutokana na wananchi wengi kumzomea.

  Kiongozi huyo alikumbana na kisanga hicho cha aina yake akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Welle Ndikilo.

  Pinda na viongozi hao, walikumbana na zomeazomea hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sahara jijini hapa, ikiwa ni hitimisho la ziara ya Waziri Mkuu huyo ya siku saba mkoani Mwanza.

  Chanzo cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kupatiwa ufumbuzi na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.

  Kitendo hicho cha wananchi kilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku akionekana kujawa jazba.

  Sababu nyingine ya wananchi kuzomea, ni hatua ya Pinda kuwaambia wananchi hao watoke mjini waende vijijini wakalime waachane na mambo ya upinzani wa kisiasa.

  Pinda alitoa kauli hiyo baada ya kundi la vijana mkutanoni hapo kuonesha alama ya V, bendera ya CHADEMA na nyimbo za Peoples, Power.

  Kwa mazingira hayo, askari wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), waliokuwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG, mabomu na marungu waliokuwepo mkutanoni hapo, walianza kuwatishia kuwapiga wananchi hao kwa lengo la kumlinda kiongozi huyo.

  Baada ya kuzidi zomeazomea hiyo, Waziri Mkuu, Pinda alilazimika kumuita mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, kisha kusema: "Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo. Kwa namna hii naona hamuwezi, maana itakuwa ni vurugu asubuhi hadi jioni". Akazomewa kisha wakaimba hatutaki CCM, hatutaki CCM. .

  Baada ya kuona hivyo, Pinda akacheka na kusema: "Hahahaaaaa, hata mkiimba peoples power, CCM ndiyo inayowaongoza". Akazomewa tena kisha Pinda akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani.

  Akahutubia mkutanoni hapo, Pinda aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa, na kwamba halmashauri ya jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA, ndiyo itapaswa kulaumiwa kama itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.

  "Hapa jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," alisema kisha akazomewa kwa mara nyingine.

  Baada ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu huyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Ndikilo alilazimika kuingilia kati kwa kusema: "Wanaozomea tunawafahamu, na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini". Akazomewa.

  Hata hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda aliendelea kuhutubia huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza waondoke mjini waende vijijini wakalime, jambo lililoonekana pia kuwakasirisha wananchi wengi kisha kumzomea tena.

  Ingawa Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza washirikiane kuleta
  maendeleo yao, na kwamba iwapo tatizo ni Mkurugenzi wa jiji suala hilo litaangaliwa.

  Aliwaomba wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.

  "Jambo jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya Ziwa Victoria wameisha...na hii ni kwa sababu ya uvuvi usiozingatia sheria. Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi", alisema Pinda kisha akazomewa tena.

  Source: Pinda azomewa
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Aiseeee sasahivi wameamua kubeba kabisa silaha za kivita ili watumalize wapenzi wa cdm!

  Hivi kuwa cdm ni kosa la jinai?

  "LIWALO NA LIWE- PINDA"
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kweli vijana wameichoka Mabwepande kabisa huyo rais ajaye atapata kazi sana sana kwenye kampeni maana sijui watawadanganyajee vijana na ahadi zoote bwana mkubwa...alishamaliza ahadi hewa ambazo hazitekelezeki....kabisaaa
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Hakika pinda ni mvumilivu sana angekuwa mtu kam Nchimbi ange agiza polisi wazitumie hizo silaha za kivita papo hapo.

  Kweli pinda amekutana na visiki vya mpingo!
   
 5. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Siasa inafanya watu kuwa kama sio mazezeta.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hakulia?
   
 7. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Afadhali kajionea mwenyewe ............. chezea M4C wewee!
   
 8. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wazomewe tu
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  ....akazomewa.....akazomewa......baada ya .....akazomewa!
   
 10. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  huu uzi upo humu tokea asubuhi mods fanya kazi yenu
   
 11. z

  zee la weza Senior Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  liwalo na liwe
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  kwa maelezo ya pinda kwa wenje seems wanajua kuwa nchi muda mchache ujao nchi inaondoka mikononi mwao...........
   
 13. m

  mmwaisoba JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 434
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ziara za mh pinda zimeoneshwa sana kwenye tv aliyeandika haya majungu anajidanganya. Mbona aelezi kilichomkuta lema kule tabata kimanga. Mdanganye wajinga wenzenu hakuna kitu hapa.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]• VIJANA MWANZA WAIMBA ‘PEOPLE'S POWER, HATUITAKI CCM'

  na Sitta Tumma, Mwanza

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]​[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza kwa muda kutokana na wananchi wengi kumzomea.

  Kiongozi huyo alikumbana na kisanga hicho cha aina yake akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Welle Ndikilo.

  Pinda na viongozi hao, walikumbana na zomeazomea hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sahara jijini hapa, ikiwa ni hitimisho la ziara ya Waziri Mkuu huyo ya siku saba mkoani Mwanza.

  Chanzo cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kupatiwa ufumbuzi na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.

  Kitendo hicho cha wananchi kilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku akionekana kujawa jazba.

  Sababu nyingine ya wananchi kuzomea, ni hatua ya Pinda kuwaambia wananchi hao watoke mjini waende vijijini wakalime waachane na mambo ya upinzani wa kisiasa.

  Pinda alitoa kauli hiyo baada ya kundi la vijana mkutanoni hapo kuonesha alama ya V, bendera ya CHADEMA na nyimbo za Peoples, Power.

  Kwa mazingira hayo, askari wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), waliokuwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG, mabomu na marungu waliokuwepo mkutanoni hapo, walianza kuwatishia kuwapiga wananchi hao kwa lengo la kumlinda kiongozi huyo.

  Baada ya kuzidi zomeazomea hiyo, Waziri Mkuu, Pinda alilazimika kumuita mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, kisha kusema: "Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo. Kwa namna hii naona hamuwezi, maana itakuwa ni vurugu asubuhi hadi jioni". Akazomewa kisha wakaimba hatutaki CCM, hatutaki CCM. .

  Baada ya kuona hivyo, Pinda akacheka na kusema: "Hahahaaaaa, hata mkiimba peoples power, CCM ndiyo inayowaongoza". Akazomewa tena kisha Pinda akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani.

  Akahutubia mkutanoni hapo, Pinda aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa, na kwamba halmashauri ya jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA, ndiyo itapaswa kulaumiwa kama itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.

  "Hapa jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," alisema kisha akazomewa kwa mara nyingine.

  Baada ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu huyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Ndikilo alilazimika kuingilia kati kwa kusema: "Wanaozomea tunawafahamu, na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini". Akazomewa.

  Hata hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda aliendelea kuhutubia huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza waondoke mjini waende vijijini wakalime, jambo lililoonekana pia kuwakasirisha wananchi wengi kisha kumzomea tena.

  Ingawa Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza washirikiane kuleta maendeleo yao, na kwamba iwapo tatizo ni Mkurugenzi wa jiji suala hilo litaangaliwa.

  Aliwaomba wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.

  "Jambo jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya Ziwa Victoria wameisha...na hii ni kwa sababu ya uvuvi usiozingatia sheria. Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi", alisema Pinda kisha akazomewa tepa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ndio, Kaka LAU MASHA anasema atarudi kuugombea UBUNGE wa NYAMAGANA ? Kwanza ndani ya CCM sidhani watampitisha

  na MAPESA YOTE!!!
   
 16. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Na ile sura sipati picha!
   
 17. O

  Original JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wangemrushia kandambili kabisa.
   
 18. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,769
  Trophy Points: 280
  Mtoto wa mkulima anayelima kwenye lami.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. L

  Liky Senior Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mi mwenyewe nlikuwepo.hakika amezomewa na ni aibu sana
   
 20. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Bado zamu ya Mr. Dhaifu...
   
Loading...