Nguvu kutoka juu inawasambaratisha wenyeviti wa kamati za bunge. Bunge sasa ni joka la kibisa

Siyo siri tena kwamba bunge sasa limekandamizwa na nguvu toka juu.

Ukiniuliza sababu za kujiuzulu kwa mwenyekiti (Hawa Ghasia) na makamu wake ktk kamati ya bajeti jawabu litakuwa ni rahisi tu...
"Sakata la Korosho".

Kama mtakumbuka sakata hili lilipelekea nguvu toka juu kutishia kuwatwanga mashangazi wa kusini.

Sasa nguvu kutoka juu imeamua kumsukuma nje kinara wa sakata hili Hawa Ghasia. Na bado haitaishia hapo. Nimetonywa kwamba kila aliye lishadadia sakata hili nguvu kutoka juu itamshughulikia 2020.

Siyo mara ya kwanza kwa nguvu toka juu kuwafyeka wenyeviti wa kamati za bunge. Bado tunawakumbuka Dr Kafumu (mwenyekiti) na makamu wake Vicky Kamata amabao wallikwaza nguvu toka juu kwa kupanga mpango wa kumtembelea mbunge mwenzao G. Lema akiwa gerezani Kisongo.

Nguvu kutoka juu imelikamata bunge kweli kweli .

Hivi Nape Moses hana kamati yoyote huko?
 
Mkuu mbona hiyo hoja ya korosho ilipanguliwa kwa ustadi mkubwa wa vielelezo na mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa bajeti?
Tulidhani kelele za wabunge zilikuwa sahihi kumbe sio.Wakati mwingine ni bora kuheshimu sheria hadi hapo sheria husika itakapotenguliwa au kuboreshwa.
 
Hawa Ghasia ni mwanamke mwenye ujasiri mno,toleo jipya la akina Bibi Titi Mohamed katika CCM ya leo.
 
Kwa tunaomfahamu Hawa Abdulrahman Ghasia hatushangai!

Hawa hajawahi kupelekeshwa

Kwenye anachoamini iwe sahihi au laa ana ujasiri wa kussimamia!

Namfananisha Sana Na Hayati Bibi Titi Mohamed

Kuna Timbwili Moja liliibuka Mzumbe University Miaka ya Nyuma wengi wetu tulishangaa ujasiri wa Binti Yule wa Kimakonde
Mzumbe kulitokea nini Mkuu/Alifanyaga nini?
 
Sasa hapo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kajiuzulu ina uhusiano gani Na Serikal?

Bibi Titi Mohamed ndio Mwanamke pekee wa enzi hizo alikuwa Na uwezo wa kumwambia Mwl Nyerere hapo umekosea Mwalimu!

Kuna Siku aliwahi kusema kwenye Kikao Kuwa Yeye anamuogopa Mungu Pekee akalazimishwa kuomba Radhi Kwa Kauli hiyo akakataa akasema yupo tayari Kwa lolote

Hawa anafanana Sana Na Bibi Titi japo wana utofauti kidogo
 
Back
Top Bottom