Nguvu kubwa inatumika dhidi ya Hayati Magufuli au inatumika kumtetea Hayati Magufuli?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,914
Ni kama vile Katikati ya jamii ya Watanzani kuna kitendawili ambacho bado hakijapatiwa majibu. Kuna swali linalosumbua watanzania wengi kuhusu nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli katika historia yetu kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kimahusiano ya kimataifa.

Kumeibuka makundi mawili yanayopingana. Lipo kundi linaloamini Hayati Magufuli alifanya mambo mengi sana mema kwa ajili ya Tanzania. Na lipo kundi linaloamini kuwa Hayati Magufuli aliivunja msingi iliyolijenga taifa letu kuwa watu waliothamini utu wa mtu.

Makundi hayo mawili, kila moja linalishutumu jingine kwamba linatumia nguvu kubwa sana ama kumshutumu Hayati Magufuli ama kumsifia. Lakini haieleweki inaposemwa "nguvu kubwa" huwa inamaanishwa hiyo nguvu kubwa ni nini!!?

Jee nguvu kubwa inatumika kumsifia ama kumshutumu Hayati Magufuli kwa aina ya utawala wake alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania?
 
Hamna mtu mwenye shida na huyo mfu maana mfu hawezi kufanya chochote

Lakini hao yatima wake wakianza kuleta uwongo kuwa kipindi chake kulikuwa vizuri, sisi lazima tuwajibu na kuwatajia mabaya yake wanaanza kusema tunatumia nguvu kubwa dhidi yake.

Nguvu kubwa dhidi ya nini sasa? Ana pose hatari gani kwani? anakuja kugombea? Au ana mgombea wake 2025? Au ana chama chake? Nguvu kubwa dhidi ya nini sasa
 
Hamna mtu mwenye shida na huyo mfu maana mfu hawezi kufanya chochote
Uko sahihi mkuu !
IMG-20230315-WA0002.jpg

Ila kufa hawafi CCM tu!
Leo na nyinyi mpo hapo na bado zamu yako inakuja maana Mungu sio Athumani !View attachment 2552344
 
Hamna mtu mwenye shida na huyo mfu maana mfu hawezi kufanya chochote

Lakini hao yatima wake wakianza kuleta uwongo kuwa kipindi chake kulikuwa vizuri, sisi lazima tuwajibu na kuwatajia....
Inatumika nguvu kuonyesha kuwa Magufuli hakuwa kiongozi mzuri kwamba alikuwa kiongozi mbaya, na nguvu ni hata hii mitandao jinsi inavyo tumika kumuelezea huyo Magufuli kuwa alikuwa kiongozi mbaya utaona ni nguvu kubwa inatumika kila pale anapotajwa Magufuli tu basi lazima aelezwe yale mabaya yake na kila siku haipiti bila kuanzishwa mada kadhaa za kuelezea mabaya ya Magufuli.

Kwahiyo utaona kusudi ni kuenea kote Magufuli afahamike na kuzungumziwa kwa yale mabaya yake tu na si tofauti na hivyo.

Kwahiyo ni suala lenye kuhitaji nguvu.
 
Ni kama vile Katikati ya jamii ya Watanzani kuna kitendawili ambacho bado hakijapatiwa majibu. Kuna swali linalosumbua watanzania wengi kuhusu nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli katika historia yetu kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kimahusiano ya kimataifa...
Binafsi sionag mantiki ya criticism juu yake wala kutaka kumpaisha! Kikubwa ilikua kama Taifa yaendelezwe aliyofanya mazur, mabaya yaachwe maan hayakua na afya kwa Taifa!!
 
Ni kama vile Katikati ya jamii ya Watanzani kuna kitendawili ambacho bado hakijapatiwa majibu. Kuna swali linalosumbua watanzania wengi kuhusu nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli katika historia yetu kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kimahusiano ya kimataifa.

Kumeibuka makundi mawili yanayopingana. Lipo kundi linaloamini Hayati Magufuli alifanya mambo mengi sana mema kwa ajili ya Tanzania. Na lipo kundi linaloamini kuwa Hayati Magufuli aliivunja msingi iliyolijenga taifa letu kuwa watu waliothamini utu wa mtu.

Makundi hayo mawili, kila moja linalishutumu jingine kwamba linatumia nguvu kubwa sana ama kumshutumu Hayati Magufuli ama kumsifia. Lakini haieleweki inaposemwa "nguvu kubwa" huwa inamaanishwa hiyo nguvu kubwa ni nini!!?

Jee nguvu kubwa inatumika kumsifia ama kumshutumu Hayati Magufuli kwa aina ya utawala wake alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania!!??
Genge S wanafanya lolote lile kumtetea Magufuli kwani walifaidika na staili mbovu ya uongozi wake.
 
Huyu mwamba kawa N/waziri wa ujenzi na baadae Waziri 1995-2005
akawa waziri wa nyumba na makazi 2006-2007
akawa waziri wa mifugo & uvuvi 2007-2010
akawa tena waziri wa ujenzi 2010-2025
Rais wa JMT 2015-March 2021
kama kiongozi kuna mengi mema kafanya (hii inamfanya akumbukwe kwa wema)
kama kiongozi kuna watu waliumia kwenye kutendaji wake wa kazi (hii itafanya watu wamkumbuke pia, kwa namna walivyoumia)

Wengi wote tumesoma shule na baadae vyuoni, it was not smooth all the way through ila ndio shule ilivyo.

Wakazi kama wa Magomeni kota, unadhani wana kumbukumbu gani kwa mtu aliewarejeshea hadhi yao ya ukaazi kwa kuwajengea nyumba bora zaidi?
Wazee wa tembo (kipindi kabla Urais wake tembo walipungua sana) bila shaka watakuwa na ill feeling.

Kuna watu kawatoa kwenye professional zao na huenda hawakuwahi kuwaza kuwa wanasiasa kwenye level ya uwaziri Dr. Mpango, Prof. Mkumbo, Prof. Kabudi, Prof. Mkenda; hawa wote walikuwa wananzuoni, at some point kupitia mikononi mwake, leo hii wengine bado ni mawaziri, mwingine VP na wengine wanakumbukwa kukalia cabinet post.

SUMA JKT, Watumishi Housing na TBA watamkumbuka kwa kuwa-empower kwa local content kwenye ujenzi wa Idodomya, jambo ambalo zamani construction of many public buildings walikuwa wachina na kuna waliokuwa wanavuta 10%.

Amecha gold purification plant ya kwanza EA na serikali (STAMICO) akiwa mbia

Amenzisha SGR project ambayo itakuwa ndefu kuliko zote africa siku ikikamilika

Ameanzisha JNHPP ambayo ikikamilika itakuwa na umeme nafuu na wa kutosha kuliko uwezo wa mitambo ya sasa.
Amecha kumbukumbu ya kujenga ukuta Mirerani ili kudhibiti utoroshwaji wa gemstone (Tanzanite)
Fika Mafinga, aliwafanya wauza nguzo kupata biashara, wakati zama zile nguzo zilikuwa zinatoka bondeni.
Aliasisi mikoa ya ofisi za madini iwe na masoko ya madini na biashara ya madini iwe na uhalali na serikali ipate kodi na watu kudhulumiana kukome.
Alisimimia maslahi ya taifa ya kuifanya serikali kuwa na ubia kwenye Twiga Corporation (Barrick akiwa mbia) na Tembe Corporation (Kabanga Nikel)
Nidhamu ya kazi iliongezeka na wananchi walihudumiwa bila kuwa "unajua mimi ni nani"
Aliweza kudhibiti/kuondoa wapiga deals za mishahara hewa.
Alimpa Bakheresa shamba na kumsisitiza azalishe sukari badala ya kuendelea ku-import sukari huku, akijua sukari ni raw material ya viwanda vyake,
Wakulima wa korosho kupata mpaka elfu 4 kwa kilo moja ikapelekea mpaka mbuzi, kunyweshwa soda.
Amekuwa sehemu ya ujenzi wa madaraja makubwa akiwa waziri na Rais (Mkapa bridge, Kigamboni bridge, Tanzanite Bridge, Mfugale Flying over na Kijazi) unganisha vile kaviacha vinajengwa.
Amekuta nchi haina ndege hata moja, na sasa wana ndege za abiria na ya mizigo iko njani kukamilika.
Ameikuwa Channel 10 na Magic FM zikimilikiwa na mtu aliezinunua kwa hela ya CCM na sasa wana-CCM imekuwa mali yao.
Alihakiki mali za chama chake na kuwaondoa wana-CCM wenzake kwenye ulaji ambao waliozoea.
Namna alivyo-handle covid 19 na kutokuweka lockdown na kusisitiza watu wafanye kazi, wachukue tahadhari, wavae barakao za vitenge, vitambaa kujikinga then akafungua shule na vyuo watoto/vijana wakarejea shule/vyuo; uamuzi ule haukuwa mwepesi, ila alisimama na Watanzania.

Kiubinadamu, atakuwa celebrated kwa mema. Ila kuna ambao waliumia au kuumizwa nao, watakuwa na yao ya kusema.

Kiufupi, jina lake liko vijiweni, whatsapp group chats, mainstream media, social media. Vyovyote vile, itachukua muda JPM kusahaulika.

Ameacha historia ya kuwa na VP wa kwanza mwanamke ambae amegombea nae vipindi viwili (2015, 2020) ambae kwa sasa pia ndio CinC.
Ameacha watoto ambao hawajulikani kama wana "ma-deal" kama walivyo watoto wa.....

116292-Do-You-See-3-Or-4.jpg
 
Ni kama vile Katikati ya jamii ya Watanzani kuna kitendawili ambacho bado hakijapatiwa majibu. Kuna swali linalosumbua watanzania wengi kuhusu nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli katika historia yetu kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kimahusiano ya kimataifa.

Kumeibuka makundi mawili yanayopingana. Lipo kundi linaloamini Hayati Magufuli alifanya mambo mengi sana mema kwa ajili ya Tanzania. Na lipo kundi linaloamini kuwa Hayati Magufuli aliivunja msingi iliyolijenga taifa letu kuwa watu waliothamini utu wa mtu.

Makundi hayo mawili, kila moja linalishutumu jingine kwamba linatumia nguvu kubwa sana ama kumshutumu Hayati Magufuli ama kumsifia. Lakini haieleweki inaposemwa "nguvu kubwa" huwa inamaanishwa hiyo nguvu kubwa ni nini!!?

Jee nguvu kubwa inatumika kumsifia ama kumshutumu Hayati Magufuli kwa aina ya utawala wake alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania!!??
Nguvu kubwa inatumika kuua falsafa ya magufulication Ii ndio inawasimbua ,si magu kama magu mwenyewe
 
Ni kama vile Katikati ya jamii ya Watanzani kuna kitendawili ambacho bado hakijapatiwa majibu. Kuna swali linalosumbua watanzania wengi kuhusu nafasi ya Hayati John Pombe Magufuli katika historia yetu kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kimahusiano ya kimataifa.

Kumeibuka makundi mawili yanayopingana. Lipo kundi linaloamini Hayati Magufuli alifanya mambo mengi sana mema kwa ajili ya Tanzania. Na lipo kundi linaloamini kuwa Hayati Magufuli aliivunja msingi iliyolijenga taifa letu kuwa watu waliothamini utu wa mtu.

Makundi hayo mawili, kila moja linalishutumu jingine kwamba linatumia nguvu kubwa sana ama kumshutumu Hayati Magufuli ama kumsifia. Lakini haieleweki inaposemwa "nguvu kubwa" huwa inamaanishwa hiyo nguvu kubwa ni nini!!?

Jee nguvu kubwa inatumika kumsifia ama kumshutumu Hayati Magufuli kwa aina ya utawala wake alipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania!!??
Nguvu kubwa inayotumika ni ya kumsifia sifia.
 
Back
Top Bottom