Nguvu inayotumika kusimika mgombea Urais CCM ndiyo hii? Je, CCM itakufa kishujaa?

Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,011
2,000
Hakuna anayebisha kuwa, Mwaka 2015, CCM iliponea chupuchupu kwenye kuwa Chama cha Upinzani.

Ilikuwa haiuziki, ilitukanwa kila pahala, ilichukiwa na kila raia nchi hii, na wao Kwa kuusoma upepo, walibadili namna yao ya kawaida katka kuendesha kampeni zao kupitia mgombea wao ambaye Leo ni Hayati Doct JPM.

Ilifika mahali wakagundua kuwa, Jina CCM ni Sawa na sumu ya nzige linapotajwa masikioni mwa watu, walikubaliana kutumia zaidi Jina la mgombea wao ili tu uwepo uangalau.

Kulitawala Neno Chagua Magufuli na sio chagua CCM, wakaiba na slogan ya Chadema iliyokuwa ikitambulika kama M4C na kuitumia kama _Magufuli For Change Kwa wastani CCM iliwasaidia Sana kueleweka Kwa wapiga Kura na ndiyo ikawa sababu ya kupata ushindi kiduchu Mbele ya mpinzani wao mkubwa Chadema kupitia Kwa mgombea wake aliyekuwa ni Waziri mkuu wa zamani bwana EL.

Nirudi kwenye hoja,

Yanayoendelea sasa ndani ya CCM ni uleule utaratibu wao wa jopo ambalo huwa linahakikisha Nani asimame kuwa mgombea wa Uraisi katika kipindi cha uchaguzi, jopo hili lina watu wazito sana ndani ya Chama, ambalo ninauhakika huwa lipo Kwa manufaa makubwa ya matumbo Yao na mambo Yao, na hili jopo ni tishio zaidi na linanguvu Sana ndani ya Chama, hasa pengine mtu anapoonekana anataka kugusa maslahi Yao, lipo tayari kufanya chochote ili tu kuhakikisha mtu wao anaingia kwenye nafasi watakalo wao

Ndani ya CCM, kuna wengi ambao wanaipenda Sana hii nchi, miongoni mwao ndio hao sasa wanatibuliwa kunyang'anywa kila sifa nzuri za ujenzi wa Taifa walizozisimamia Kwa jasho na damu Chini ya Raisi Hayati JPM.

Na Kinafanyika hicho, ili tu kazi zoote walizozisimamia Kwa kujitoa usiku na mchana ionekane Kwa wananchi kuwa walikuwa wanapiga pesa tu!!

Ieleweke kuwa, Sipingi ripoti ya CAG, Ila nachotaka kuonesha ni jinsi gani CCM ilivyo na watu wanaopanga Nani awe Nani na Nani awe hivi ama vile.

Jopo hili baada ya kugundua kuwa, aliyekuwa Raisi wetu JPM amekuwa na kundi kubwa zaidi ndani ya Chama kiasi cha kufikia Robo tatu ya watu mhimu ndani ya Chama na pengine huwenda naye kama kiongozi, pengine alikuwa tayari naye ameshaanza kumwandaa mtu wa kumrithi mikoba

Sasa, ili kuondoa nguvu hiyo iliyotaka kumea Kwa nguvu na Kwa Kasi kubwa na kundi kubwa kuwa nyuma ya JPM, ndipo tunashuhudia nguvu ya kuchafua Miradi yoote iliyoanzishwa na kujengwa na Hayati JPM Chini ya wasaidizi wake waliokuwa na Nia ya kuiona nchi inakwenda kuwa na Miradi mikubwa na yenye faida kwa nchi.

Yanafanyika haya pengine bila ya wao wasaidizi wake kujua ni nini hiki kinafanyika, ama tena ndani Yao kunakitu kimetembea ili nao wawe nyuma ya jopo Hilo lenye maslahi ndani ya chama, na ndiyo maana unaona kila anayesimama anaponda Miradi ya mwenda zake

Sasa, unajiuliza, Miradi hiyo inamatatizo gani, Eti Hadi standi ya Mbezi Nayo haifai, Stiglasgoji nao haufai, SGR pia, bomba la mafuta halifai, ndege pia, Wakati kipindi cha kabla ndege hazijanunuliwa, yalikuwa masimango kutoka kwa wapinzani.

Je, sasa, Waliosimamia hii Miradi Kwa jasho na damu, watakubali Miradi Yao hiyo kugezwa na Kisha waonekane walikuwa wanapoteza pesa zetu kwenye Miradi ambayo sasa Mbele ya Chama Chao inaonekana ni ya hovyohovyo na isiyo na faida, au sasa ni wakati wa wao kufa kiume ndio sasa?

Na kama hawatakubali kudharilishwa huko, ndio wakati wa CCM kuchanika vipandevipande? Ni heri sasa waliokuwa wasimamizi wa Miradi hii inayoshambuliwa kuwa si kitu, wasimame kidete kutetea uzuri wa Miradi hiyo, siyo kukaa kimya Wakati tunajua hamkupata hata usingizi Wakati mwingine mkiwaza kazi zenu, kama mbwai, mbwai tu, ni Bora kufa ukiwa unasimamia unachokiamini, na huko ndiko kunaitwa kufa kishujaa

Mimi nataka CCM ifike kikomo Kwa kuchanika chanika vipandevipande, si kwa kutudharau huko, hamuwezi kuanzisha Miradi nyinyi wenyewe halafu badaye mseme Miradi hiyo si kitu tena!

Mungu saidia hili dude CCM life

Amina
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,797
2,000
Nataka CCM ife, tumechoka na michezo Yao ovu
Kila Mtanzania atapumua na tutakuwa tumepata Uhuru mara ya pili

Ila ni CCM hii hii ambayo imekifanya hiki kizazi kijione kuwa bila ya kuiibia Serikali na Jamii yako basi wewe ni mjinga
 
Daftari la Watoro

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
373
1,000
Niliwaambia wenzangu kabla ya uchaguzi 2015 ccm inamiaka tena km 20 huko mbele, wakaona sijui kusoma nyakati. Ukweli mchungu kutokana na system ya nchi yetu na mizizi mikubwa iliyopandikizwa na ccm kwenye nyanja zote za serikali hiki chama tunacho tena 15yrsmore. Mimi sio mkereketwa wa hiki chama ila huu ndo mtazamo usio na bias.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,035
2,000
Hakuna anayebisha kuwa, Mwaka 2015, CCM iliponea chupuchupu kwenye kuwa Chama cha Upinzani.

Ilikuwa haiuziki, ilitukanwa kila pahala, ilichukiwa na kila raia nchi hii, na wao Kwa kuusoma upepo, walibadili namna yao ya kawaida katka kuendesha kampeni zao kupitia mgombea wao ambaye Leo ni Hayati Doct JPM.

Ilifika mahali wakagundua kuwa, Jina CCM ni Sawa na sumu ya nzige linapotajwa masikioni mwa watu, walikubaliana kutumia zaidi Jina la mgombea wao ili tu uwepo uangalau.

Kulitawala Neno Chagua Magufuli na sio chagua CCM, wakaiba na slogan ya Chadema iliyokuwa ikitambulika kama M4C na kuitumia kama _Magufuli For Change Kwa wastani CCM iliwasaidia Sana kueleweka Kwa wapiga Kura na ndiyo ikawa sababu ya kupata ushindi kiduchu Mbele ya mpinzani wao mkubwa Chadema kupitia Kwa mgombea wake aliyekuwa ni Waziri mkuu wa zamani bwana EL.

Nirudi kwenye hoja,

Yanayoendelea sasa ndani ya CCM ni uleule utaratibu wao wa jopo ambalo huwa linahakikisha Nani asimame kuwa mgombea wa Uraisi katika kipindi cha uchaguzi, jopo hili lina watu wazito sana ndani ya Chama, ambalo ninauhakika huwa lipo Kwa manufaa makubwa ya matumbo Yao na mambo Yao, na hili jopo ni tishio zaidi na linanguvu Sana ndani ya Chama, hasa pengine mtu anapoonekana anataka kugusa maslahi Yao, lipo tayari kufanya chochote ili tu kuhakikisha mtu wao anaingia kwenye nafasi watakalo wao

Ndani ya CCM, kuna wengi ambao wanaipenda Sana hii nchi, miongoni mwao ndio hao sasa wanatibuliwa kunyang'anywa kila sifa nzuri za ujenzi wa Taifa walizozisimamia Kwa jasho na damu Chini ya Raisi Hayati JPM.

Na Kinafanyika hicho, ili tu kazi zoote walizozisimamia Kwa kujitoa usiku na mchana ionekane Kwa wananchi kuwa walikuwa wanapiga pesa tu!!

Ieleweke kuwa, Sipingi ripoti ya CAG, Ila nachotaka kuonesha ni jinsi gani CCM ilivyo na watu wanaopanga Nani awe Nani na Nani awe hivi ama vile.

Jopo hili baada ya kugundua kuwa, aliyekuwa Raisi wetu JPM amekuwa na kundi kubwa zaidi ndani ya Chama kiasi cha kufikia Robo tatu ya watu mhimu ndani ya Chama na pengine huwenda naye kama kiongozi, pengine alikuwa tayari naye ameshaanza kumwandaa mtu wa kumrithi mikoba

Sasa, ili kuondoa nguvu hiyo iliyotaka kumea Kwa nguvu na Kwa Kasi kubwa na kundi kubwa kuwa nyuma ya JPM, ndipo tunashuhudia nguvu ya kuchafua Miradi yoote iliyoanzishwa na kujengwa na Hayati JPM Chini ya wasaidizi wake waliokuwa na Nia ya kuiona nchi inakwenda kuwa na Miradi mikubwa na yenye faida kwa nchi.

Yanafanyika haya pengine bila ya wao wasaidizi wake kujua ni nini hiki kinafanyika, ama tena ndani Yao kunakitu kimetembea ili nao wawe nyuma ya jopo Hilo lenye maslahi ndani ya chama, na ndiyo maana unaona kila anayesimama anaponda Miradi ya mwenda zake

Sasa, unajiuliza, Miradi hiyo inamatatizo gani, Eti Hadi standi ya Mbezi Nayo haifai, Stiglasgoji nao haufai, SGR pia, bomba la mafuta halifai, ndege pia, Wakati kipindi cha kabla ndege hazijanunuliwa, yalikuwa masimango kutoka kwa wapinzani.

Je, sasa, Waliosimamia hii Miradi Kwa jasho na damu, watakubali Miradi Yao hiyo kugezwa na Kisha waonekane walikuwa wanapoteza pesa zetu kwenye Miradi ambayo sasa Mbele ya Chama Chao inaonekana ni ya hovyohovyo na isiyo na faida, au sasa ni wakati wa wao kufa kiume ndio sasa?

Na kama hawatakubali kudharilishwa huko, ndio wakati wa CCM kuchanika vipandevipande?

Mimi nataka CCM ifike kikomo Kwa kuchanika chanika vipandevipande, si kwa kutudharau huko, hamuwezi kuanzisha Miradi nyinyi wenyewe halafu badaye mseme Miradi hiyo si kitu tena!

Mungu saidia hili dude CCM life

Amina
Itakuwa heri mno kama CCM ikifa mapema, hiki chama ni cha majangili wa kiuchumi.
 
Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
4,363
2,000
Ukiachana na swala la kuitoa sisiem madarakani kubaki ndoto vichwani mwa watanzania...

Ila awamu iliyopita sio kwamba inachafuliwa ni kwamba watu wamepata pa kusemea.

Enzi za JPM uzalendo ilikuwa ni kusifia na kukosoa ilikuwa ni Uhaini,,, naona sasa waliohubiri ule uzalendo wanageuka tena
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom