Nguruwe pori asababisha ajali na kuua watu watatu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Wengine sita wajeruhiwa vibaya, walazwa hospitalini

Watu watatu wamekufa papo hapo na wengine watano kujeruhiwa vibaya baada gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kata ya Kitunda kwenda Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora kuacha njia na kugonga kingo za barabara kisha kupinduka.
Diwani wa kata hiyo, Julius Simwela, aliliambia gazeti hili kuwa gari lililohusika katika ajali hiyo ni lenye namba za usajili DFP 6698, mali ya shirika la mradi wa EGPAF.
Simwela alisema ajali hiyo ilisababishwa na ngiri ambaye aliingia ghafla barabarani na dereva alipojaribu kumkwepa, gari lake liligonga kingo za barabara na kupinduka.
Alifafanua kwamba dereva wa gari hilo, Jeremia Nyunja, alifanya jitihada kubwa za kumkwepa ngiri huyo lakini zilishindikana ambapo mnyama huyo alitokomea porini akiwa salama.
Simwela aliwataja watu waliokufa papo hapo kuwa ni Chacha Mugesi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kitengo cha ugani, Mwajuma Masegese na Ramadhani Chapa, wote wakazi wa Wilaya ya Sikonge.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Dk. Enock Magana, majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo na wanaendelea na matibabu ambapo walipelekwa hapo na basi la kampuni ya Sabena lilikokuwa likitokea mkoani Mbeya.
Dk. Magana aliwataja majeruhi hao kuwa ni Hezron Mbewa, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Frederick Mtao, ambaye ni mtumishi wa hospitali teule ya wilaya ya Sikonge, Frederick Kayungilo, mtumishi wa Temesa mkoani Tabora na Simon Sungura.
Alisema hali za majeruhi hao kwa sasa zinaendelea vizuri isipokuwa dereva Nyunja ambaye alihamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kupatiwa matibabu zaidi.
Watumishi hao wa Halmashauri ya Wilaya Sikonge, walipata ajali hiyo wakati wakitoka katika shughuli za kikazi kata ya Kipili, Kitunda na Kiroli, Tarafa ya Kiwele.



CHANZO: NIPASHE

Dereva kakubali amkwepe Ngiri kunusurisha maisha yake huyo mnyama na na Gari lake likapinduka na kuuwa watu ama kweli kazi ipo hapa
 
Let them rest in peace!!!
Ni vizuri dereva wa gari akaisaidia polisi kupata ukweli wa jambo hili...
 
Back
Top Bottom