Takriba watu miatatu walihudhuria mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF uliofanyika juzi jmosi 13/2/2010.
Baada ya maelezo marefu na ya ufasaha kuhusu mwangalio mpya uliofikiwa kati yake na mh. Karume hapo tarehe 5/11/2009 na ambao unatoa na kuleta matumaini mapya visiwani, wengi wa wasikilizaji wake yaelekea kuwa hicho sicho walichokuwa wamefuata.
na mara nafasi ya kuuliza maswali ilipotolewa nao walijaribu kuchomekea hoja yao abayo ni kuwepo kwa Muungano!
Maalim Seif aliipapatua hoja ya kwanza kuhusu Muungano kwa kusema kuwa "Hatupo kwa kuvunja Muungano" Kauli hiyo yaonekana kuwa haikupendeza kwani ukumbi ulionekana kupigwa na butwaa kidogo.
Swali la pili kuhusu Muungano liliitaka CUF ivunje Muungano mara moja ikiwa mambo kadhaa yasingefanyika, Kauli hii ilipata umaarufu kwa kushangiliwa na zaidi ya 3/4 ya wasikilizaji.
Maalim Seif akimtaja jina mtoa hoja alisema nafikiri Fulani hakunisikia nimesema: "hatuko kwa kuvunja Muunganio", kwa mara nyingine ukumbi ilipigwa na butwaa, ndipo nilipoamini kuwa wengi wataondoka wakiwa wamefadhaika.