Ngurumo ya maalim Seif yafadhaisha wengi London | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngurumo ya maalim Seif yafadhaisha wengi London

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by alibaba, Feb 16, 2010.

 1. a

  alibaba Senior Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Takriba watu miatatu walihudhuria mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF uliofanyika juzi jmosi 13/2/2010.
  Baada ya maelezo marefu na ya ufasaha kuhusu mwangalio mpya uliofikiwa kati yake na mh. Karume hapo tarehe 5/11/2009 na ambao unatoa na kuleta matumaini mapya visiwani, wengi wa wasikilizaji wake yaelekea kuwa hicho sicho walichokuwa wamefuata.
  na mara nafasi ya kuuliza maswali ilipotolewa nao walijaribu kuchomekea hoja yao abayo ni kuwepo kwa Muungano!
  Maalim Seif aliipapatua hoja ya kwanza kuhusu Muungano kwa kusema kuwa "Hatupo kwa kuvunja Muungano" Kauli hiyo yaonekana kuwa haikupendeza kwani ukumbi ulionekana kupigwa na butwaa kidogo.
  Swali la pili kuhusu Muungano liliitaka CUF ivunje Muungano mara moja ikiwa mambo kadhaa yasingefanyika, Kauli hii ilipata umaarufu kwa kushangiliwa na zaidi ya 3/4 ya wasikilizaji.
  Maalim Seif akimtaja jina mtoa hoja alisema nafikiri Fulani hakunisikia nimesema: "hatuko kwa kuvunja Muunganio", kwa mara nyingine ukumbi ilipigwa na butwaa, ndipo nilipoamini kuwa wengi wataondoka wakiwa wamefadhaika.
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Pengine watamsikiliza mwenzao, naona aliunguruma vizuri. Nilishangaa kuona mabango yanayosema mkutano wa wazanzibari. Jamani hivi kweli sisi watanganyika mmetuchukia kiasi hicho? Bora hii ndoa ife kifo cha mende.
   
 3. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana wamekimbilia huko majuu. Sisi tuko hapa na mambo yote tutayatatua tukiwa hapa kwa sanduku la kura. Maalim Seif ameonyesha ukomavu wa kisiasa. Wao wanataka watuletee matatizo ya uvunjifu wa amani hata hii ndogo tuliyonayo!! Wakafie mbali. S**..,,<<;;//@@33#34%%6....nzi zao.
   
 4. B

  BUBBA Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahenga walisema "Ficha upumbavu wako, onyesha hekima yako", ndugu zetu walionnje ya nchi wamekua watu wa kwanza kuchochea kuvunjika kwa muungano wetu hasa wakati huu viongozi wetu wanaangalia njia nzuri ya kuendea umoja wa Africa. Pale wanapowachochea jamaa zetu wa Mchamba wima,kisiwandui wavuje mkataba wa muungano pengine kwa njia ya fujo wakati wao wako uk na familia zao na wengine wameshakana uraia wa Tanzania. Ndugu zangu inatupasa kuwa makini na hawa watu wanaojaribu kuwa washauri kwenye maisha yetu ambayo wao hawayaishi. Kwanini MAALIM SEIF kila akifanya jambo Tanzania(Zanzibar) anakimbilia nje kuwaona hao wanaojiita Wanzanzibari? Ni wakati wa kuonyesha HEKIMA zetu na kuficha UPUMBAVU wetu.
   
 5. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,397
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tuachane na Wakimbizi wa kujitakia ambao wanadhani uzuzu wao na ubinafsi wao unaweza kutuhadaa sisi tuliobaki nyumbani tukipigania mustakabali wetu. Kama wangekuwa na uchungu wa wapemba ama wa-zenj wangebaki nchini na si kukimbilia ughaibuni huku wakiukana uraia wao, lakini wanajiweka kimbelembele kushadidia mambo ya huku....Watu hao ni wa kuogopwa kama Ukoma.
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Watu 300 anafanya mkutano wa hadhara this is rediculous..angefanya nao tu kikao cha ndani akazungumza nao kwa mapana na marefu..
   
 7. bona

  bona JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,794
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  inabidi tuanzishe vita baridi na hawa watanzania walio majuu, kwanza kilichowafanya kukimbia tz ni kuepuka challenge za umasikini hapa nyumbani, badala ya kubaki kushirikiana kuyatatua wao wakakimbia, leo wanachochea muungano uvunjike, wengine ndio walioukana utanzania leo hii wamekumbuka kua "asiye na kwao ni mtuma" wamekuja na dual citizenship(uraia wa nchi mbili), hatuwaitaji kaeni ukouko kwani mmesahau nini uku? kama cuf wamevunja uhasama na wako tayari kuboresha nchi yao well and good na kama kuvunja muungano kutaleta amani ya kudumu zenji basi rukhsa na muungano uvunjike!
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukiachilia ubinafsi wa kisiasa wa hapa na pale kati ya Watanzania Bara na Visiwani Maalim Seif kama ana akili za kuangalia mbali hawezi kutaka kuvunja Muungano. Wanaotaka Muungano uvunjike cannot see beyond their noses! Zanzibar ni visiwa kama vilivyo visiwa vingine, hatuombi lakini inaweza ikatokea kwamba baada ya miaka 50 ijayo baadhi ya maeneo yanaweza kumezwa na bahari.

  Zaidi ya hayo, Wazanzibari wataendelea kuzaliana na kuijaza Zanzibar. Wakijitoa kwenye Muungano watashindwa kupata mahali pa kwenda hapo ongezeko la watu litakapozidi eneo la Zanzibar litakalokuwepo. Hata kama watajenga magorofa ku-accomodate hiyo population bado watahitaji 'outlet' - Tanzania Bara! Hao 'wakimbizi' walio huko nje hawayafikirii hayo yote wanadhani kila kitu ni siasa tu.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,614
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hayo masuala aliyoulizwa kuhusiana na muungano yameulizwa na amshushu ,nae ameyasitukia .
  Afu mbona akuna tena muungano ,just ni nchi mbili zilizokuwa na mipaka iliyowaazi na watu wake wanaruhusika kwenda huku na kule.
   
 10. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,087
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Huu Muungano umeisha lini? Halafu inaelekea utafurahi kweli siku kitamkwa rasmi kuwa umeisha Muungano!..Agrrr!!
   
 11. Kamamaa

  Kamamaa Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Watu kama hawa ndio wasioitakia nchi mema, lolote litakalo tokea wataumia waliopo na si wao...nafikiri waliache hili suala na wao waendelee kutafuta maisha huko mbele ya safari
   
 12. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 3,060
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Huu ni ujinga na upumbavu wa watu wasio ona. Mim kila mara nasema wale wanataka kuv├╣nja Muungano nakuleta uraia wanchi mbili nivipofu wasiofaa kutuongoza. Napinga sana kusikia uvunjwaji wa huu muungano nakama zipo silaha tutapigana mpaka risasi ya mwisho. Nalipenda taifa hili naupenda utanganyika wangu naupenda uzanzibar naupenda utanzania wangu. God is great
   
 13. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Binafsi ningependelea kuwe na shirikisho tu kama zilivyo nchi za Scandinavia au east Africa ilivyokuwa na kila upande uwe na uongozi wake na serekali yake Tatizo mlilonalo wezetu ni hili neno Tanganyika na laiti kama mgekuwa na Proper Name of that Country instead of Tanganyika nahakika zamani mgelikubali hili lakuwa kila upande aongoze watu wake na tuwe na shirikisho la mambo fulani na siuo kuingiliana kama ilivyo hivi sasa .
   
 14. a

  alibaba Senior Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Babylon,
  Tatizo la neno Tanganyika ni nini?
  Mwengine anaweza kudai kuwa tatizo ni neno Zanzibar au Wazanzibair..........!
   
 15. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hawa ndo watu wanaoishi kama asylum seekers yaani serikali inawapa posho y kila kitu na wanachofanya wenyewe ni kuzaliana watoto wengi ili upate posho nyingi tu. Shule kwenda ni tatizo sana. Yaani ukiona makazi yao ni duni sana bora warudi home sweet home. Huko ndo kwenye shootings za kila siku. Hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kutumia tu je unategemea wataitakia mema nchi walioiacha na watu wake? Hawana maslahi nayo
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  hao jamaa watakuwa si Watanzania, labda ni Wacomores ndiyo maana mtizamo wao siyo wa kuangalia mbele na kuitakia mema fyucha yao na kizazi chao, na kama ni Wazanzibar, nitakuwa na mashaka na uwezo wao wa akili,
   
 17. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Ray B,you are right ,hawa Wazenj,ni lazy people.Wengi walijilipua ,wanapata mafao toka serikalini,hakuna kwenda shule,ni kuzaa watoto tu.Hawana mpango wowote.

  Miaka ya 1989/90 kuliuwa na Mzenj mmoja anaomba omba pale station ya West Ham,sio mbali sana na Maalim Seif alipofanya mkutano.Ilikuwa embarrasment kwa sababu kwa Mtanzania kuombaomba Ulaya ni aibu sana hasa station ya rail.Hii ni fact kama Mtanzania ulishuhudia huyu bwana miaka ile,hebu waambie wana JF
   
 18. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni muda gani sasa kutokea kuijuwa kwako zanzibar? umeshawahi kusikia Raia wake kukataa kuitwa miongoni mwa majina ya visiwa vyao?wezetu hamataki kuitwa watanganyika imekuwa kama vile Taboo au fedheha , hamtaki kusia au au kuitwa watanganyika na isitoshe hamko tayari kusikia kuisimamisha serekali itwayo ya Tanganyika
   
 19. C

  CHAMPUNGA Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu sikukatishi tamaa katika kutetea aina hii ya muungano, ambao hakuna hata sehemu moja ya binadamu wenye akili duniani wanaweza kuuafiki. Lakini pia nakutahadharisha kuwa ipo haja hata sisi wa Newala kuanza kuhoji sababu za kuendelea kuitwa Watanzania au Watanganyika kama kila kitu kwetu ni shida, maji, umeme afya, barabara tena hata hiyo elimu ni kwa vile takwimu zinazowekwa wazi ni za taifa lakini kiukweli illiteracy level katika eneo hili imepanda tangu tulipoanza kuitwa Watanzania, kaka hawa wataendelea kutuimbisha nyimbo tusizojua lafudhi zake richmond, epa, kiwira, ufisadi shiit. Tujipange kaka hili dubwana kubwa litaendelea kutumaliza tu hakuna kitu hapa. Watu wakae dodoma wajadili maji ya mkupete ambako hawakujui ni usanii. mimi nilifanya tathmini nikiwa chuooni miaka ya karibuni asilimia zaidi ya tisini ya Watanzania ambao walikuwepo chuoni kwa wakati huo wametembea maeneo mengi ya nchi lakini hawajafika Mtwara na Lindi. Na huku Ulaya ndo kabisaaa ukijitambulisha kuwa unatoka kusini mwa Tanzania watu wanaanza kuangaliana usoni.
  Kaka maisha huru ya kutembea au kuishi popote pale hayawezi kuzuiliwa na limuungano feki kama hili kwa dunia ya sasa hata likivunjika watu wataenda kuishi Zenji na wazenji wataishi huku "Ufisadini" msiwatishe watu. Tutaendelea kuhitajiana kiuchumi nk. Ni mtazamo
   
 20. a

  alibaba Senior Member

  #20
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CHAMPUNGA,
  Ikiwa Maalim Seif Kasema yeye na CUF hawapo kwa kuvunja Mungano! Unadhani Mh. Karume atasemaje? Hii ina maana Wazanzibari na Wapemba hawawezi kupewa nafasi ya kuamua juu ya Swali hili.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...