Tetesi: Ngurumo; Wakala wa Mabeberu, Chadema Anayemaliza Mwaka Vibaya

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Na Mwandishi Wetu

Mamia ya Watanzania wamepinga upotoshaji wa mwandishi wa habari aliyegeuka mwanaharakati, mwanasiasa na zaidi wakala wa mabeberu, Ansbert Ngumrumo, ambaye kazi yake kubwa ni moja tu; kupotosha kila jema la nchi yake awe ndani au nje ya Tanzania na kusifia hata ujinga wa nchi za nje.

Hata hivyo leo amepata kinachomuhusu baada ya wasomaji wengi mitandaoni kumvamia na kumzodoa kwa tabia yake ya undumilakuwili.

Ngurumo ambaye kwa sasa anaishi nchini Finland baada ya jaribio lake la kujiteka ili aichafue nchi kushindikana, ametoa kali ya mwaka alipoweka mtandaoni picha ya wananchi wanaovuka kijito cha maji kijijini huko Nyeri nchini Kenya na kuandika kuwa eti ni wananchi wa Manyara, Tanzania na kudai kuwa wananchi hao hawana haja na ndege zinazonunuliwa na Serikali badala yake wanahitaji daraja.

“Kitu gani unacholipwa na mabeberu kwa kuchafua taswira ya nchi yako“; anahoji Bw. Francis Sindimwo katika ukurasa wake wa twitter na kuonesha kusikitishwa na kitendo cha mwanaharakati huyo ambaye pia ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoa habari za uongo kwa maslahi binafsi.

"Katika Taifa lolote lile uwekezaji katika miundombinu ni jambo muhimu ili kujenga uchumi jumuishi ikiwemo kuwa na usafiri wa anga ulio imara, barabara, madaraja, hospitali, reli, maji, shule na vingine vyote ambavyo kila mtanzania kwa sasa anashudia utekelezaji wake kupitia Serikali iliyopo madarakani na maendeleo ni mchakato haiwezekani kila kitu kumalizwa leo.....unataka hata kwenye korongo shambani kwa mtu Serikali iweke daraja?" aliandika mwingine.

"Hata katika nchi ulikopewa hifadhi Bw. Ngurumo wameimarisha usafiri wa anga na umechochea ukuaji wa uchumi unaowezesha mabeberu kukulipa posho ya kujikimu ukiwa unaishi maisha ya upweke kwa sababu ya ujinga wako," ameandika mmoja.

Kwa upande wake Bw. Amon Nguma katika ukurasa wake wa twitter na anamtaka Bw. Ngurumo kuacha upotoshaji kwa kudanganya wananchi kupitia picha za mitandaoni zinazoonesha taswira mbaya huku picha hiyo ikiwa kiuhalisia ni kutoka nchini Kenya.

Aidha, Bw Nguma anaendelea kusisistiza kuwa kwa sasa watanzania hawana imani tena na taarifa zinazotolewa na watu kama Bw. Ngurumo na genge lake la vibaraka wa mabeberu wanaotumiwa kwa maslahi yao binafsi yasiyo na tija kwa wananchi wa Tanznaia.

Baadhi ya wananchi wamekwenda mabali na kumuwekea Ngurumo picha za mafuriko nchini Finland, ombaomba nchini humo na ndege zilizonunuliwa na serikali hiyo.

"Haya sasa huko kwa mabwana zako nako barabara zimejaa maji na kuna ombaomba kibao, washauri wauze ndege walizonunua za Air Finland wajenge miundombinu."

Kutokana na hoja hizo, Ngurumo amekimbia mjadala huo kwa kushindwa kujibu hata hoja moja.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Beberu.
tapatalk_1577354951190.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom