Ngurdoto: EAC Ilimshinda Nyerere. Hawa Wachakachuaji Wataiweza?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,831
2,000
Jana, kupitia taarifa ya habari kwenye kituo kimoja cha TV, walioneshwa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wakizungumzia ishu ya kutunza misosi, sijui mabadiliko ya tabia nchi. Ilifanyika Ngurdoto. Hivi ngurdoto inamilikiwa na nani?

Ajabu:
Hakukuwa na Kagame wala Museven. Walikuja wawakilishi wao.

Kibaya zaidi:
Wakuu wa nchi waliokuwepo ni wale wachakachuaji:

Kibaki: Mwizi wa kura aliyeingia madarakani kwa 'zulia la damu' ya Wakenya zaidi ya 1000.

Kikwete: Msanii aliyetumia ubovu wa Katiba na umbumbumbu wa Watanzania hasa wa vijijini, kurejea Ikulu ya Magogoni licha ya kuzidiwa kila kitu na Dr. Wilbroad Peter Slaa wa Chadema

Nkurunzinza: Dikteta aliyechini ya muavuli wa demokrasia lakini nchi yake inaongoza kwa 'kupotelewa' na wapinzani katika mazingira tatanishi. Itakumbukwa kuwa aliingia madarakani licha ya kususiwa na vyama vya upinzani kikiwemo cha Aghaton Gwasaa ambaye anaongoza chama cha upinzani chenye nguvu. Burundi ni nchi masikini lakini iko chati katika swala zima la ufisadi wa viongozi kama Tanzania tu.

Kumbukumbu:
Wakati wa kuapishwa kwa Mkwere katika viwanja vya Uhuru, Paul Kagame na Yoweri Mseveni hawakuhudhiria. Hiki si kitu kidogo. Kuna siri wanayo hawa mabwana wawili.

Samuel 6 inabidi afanye utafiti. Atuambie ni kitu gani hasa bila 'unafiki' kama alivyojitapa yeye 'unafiki' kwake 'mwiko'.

Vinginenvyo,

Mfupa uliomshinda Nyerere hawa wachakachuaji utawashinda hata kabla ya kuuona.

Naomba kutoa hoja.
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,532
2,000
hiyo Ngurdoto huwa nashindwa kuelewa ni ya nani wengine wanasema ni ya mkwere na wengine wanasema ni ya Sumaye na mkapa so tufanye utafiti.

Kuhusu hao jamaa wanaojiita marais wote walewale tu walokuja na wasokuja ila ukiamua kuchukua lesser evil bora hata huyo nyang'au manake anajitahidi sana kurekebisha kwa kufanya maendeleo kwake hawa wengin bure tu.

Suala la Africa ya Mashariki ni majukwaani zaidi wala si katika utendaji!
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,515

Mmiliki anayetambulika officially anaitwa Awio Meleu Mrema (ambaye pia ni mmiliki wa Impala Hotel ya Arusha).

Inawezekana pia kuna watu wengine nyuma ya pazia.....lakini hawatajwi (wako ki-incognito zaidi).
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,669
0
Mmiliki anayetambulika officially anaitwa Awio Meleu Mrema (ambaye pia ni mmiliki wa Impala Hotel ya Arusha).

Inawezekana pia kuna watu wengine nyuma ya pazia.....lakini hawatajwi (wako ki-incognito zaidi).

Hili ni pambo na geresha mkuu. Unakumbuka waasisi wa kutaja mali unapoingia na unapotoka madarakani?? Unakumbuka ilijengwa kipindi/mwaka gani???

Hawawezi miliki wao, maana ingewatesa kwenye kutaja mali.

Pia ilijengwa strategic kwa ajili ya ku-host vitu kama hivi, je huoni ingewaletea utata kupeleka ulaji waziwazi kwao???

Kuna mtu nyuma ya pazia mzee na wadaku wanataja wazito wa awamu ya 3.
 
mchakachuaji1

Senior Member
Nov 4, 2010
104
195
Hii EAC mpaka sasa mimi sioni kama ina umuhimu wowote kwa nchi yetu zaidi ya kujibebesha zigo lisilo na umuhimu wowote kuendesha taasisi hii isiyo na faida. Inawezekana umbumbumbu wabgu ndio unanifanya nisione umuhimu, mtanzania mwingine anayeona umuhimu wa EAC atanabahishe hapa jamvini.
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,531
2,000
hivi JK anaelewaga kweli mambo yanayoongelewaga kwenye hizi meetings jamani
 
WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,463
0
hiyo ngurdoto huwa nashindwa kuelewa ni ya nani wengine wanasema ni ya mkwere na wengine wanasema ni ya sumaye na mkapa so tufanye utafiti.

!
uzushi mtupu!...unajua impalahotels, naura springs hotels?? Basi mmiliki ni mwenye ngurdoto
 
NgomaNgumu

Senior Member
Nov 20, 2010
194
0
Kichwa cha habari cha hii topic kinasema kua EAC ilimshinda Mwl Nyerere je itawezekana sasa.Jawabu inaweza ikawezekana au isiwezekane kwani hata tatizo la Zanzibar halikumalizwa wakati wa mwalimu. La kuangalia zaidi nafikiri ni kua je watanzania wako tayari kwa huo umoja au badi in terms of Education and others factors.

Wasiwasi mkubwa uliopo ni kua bado watanzania wengi hawajawa ktk position ya kucompete ukilinganisha na nchi jirani. Kwahiyo uwezekano wa ajira nyingi kwenda nchi jirani ni mkubwa zaidi, ingawa hilo linafanyika hata bila ya muungano lakin kwa sababu ya muungano wanaweza kupata access zaidi. Upande mwengine ni ule wa kumilki ardhi, huu nao unapaswa kuangaliwa kwa makini. In any case ni swala ambalo haliko very clear na linahitaji more research ili kudetermine wether it is worth doing it at this moment of time.
 
Bull

JF-Expert Member
Nov 4, 2008
985
0
Nyerere hakushindwa na East africa pekee bali pia alishindwa kuongoza na kutuletea maendeleo watanzania, Hivi Nyerere aliweza nini ??
 
kansiana

Member
Nov 8, 2010
33
0
Nyerere hakushindwa na East africa pekee bali pia alishindwa kuongoza na kutuletea maendeleo watanzania, Hivi Nyerere aliweza nini ??

Bull, His personality and image seserve him to be a charismatic leader, alijua mengi ambayo watanzania wengeelewa katika miongo miwili ijayo, "If you want to menage you future, you have to manage information, therefore information is power" ni vile tu ni mvivu wa kufikiri otherwise Nyerere ni kila kitu kwa Tanzania. Alikuachia madini ambayo kwa umri wako ungesikia kama historia angalia unavyofanya? Be quite and think again!!!!
 
Kudadeki

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
859
0
Ukiuliza USHAHIDI wa hizo ngonjera za uchakachuaji? Unaambiwa WANANGOJEA MUDA MUAFAKA!

Ama kweli nchi hii wamejaa WENDAWAZIMU!
 
Kudadeki

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
859
0
Bull, His personality and image seserve him to be a charismatic leader, alijua mengi ambayo watanzania wengeelewa katika miongo miwili ijayo, "If you want to menage you future, you have to manage information, therefore information is power" ni vile tu ni mvivu wa kufikiri otherwise Nyerere ni kila kitu kwa Tanzania. Alikuachia madini ambayo kwa umri wako ungesikia kama historia angalia unavyofanya? Be quite and think again!!!!

Hayo madini aliyatengeneza yeye huko chini ya ardhi ama vipi hata unaweza ukadai kuwa ALITUACHIA? Je umasikini wa kutupwa, foleni kwa ajili ya unga na sabuni? Viatu vya matairi? Utamaduni wa kupiga mayowe ya zidumu fikra za Mwenyekiti wa chama? Na viongozi wabovu tuliokuwa nao?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom