Nguo ya ndani inabidi ivaliwe kwa miezi mitatu tu na itupwe. Kina dada acheni kununua sidiria za mitumba

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
3,030
3,324
Wakuu,

Kuna watu huwa wanatumia nguo za ndani kwa muda mrefu bila kununua mpya.

Kiafya, nguo ya ndani inabidi ivaliwe kwa miezi mitatu tu baada ya kuinunua, kisha itupwe au ichomwe moto.

Unapoitumia nguo ya ndani mwaka mzima kwanza ni aibu.

Vile vile nguo za ndani za mitumba siyo njema kuvaliwa. Hasa kina dada mnapenda sana kuvaa brazia za mitumba. Siyo nzuri kiafya na huweza kukuletea magonjwa ya ngozi.

Mjina Mrefu (M. M)
 
Back
Top Bottom