Nguo na Mitindo ya Zamani ambayo kwa sasa ukivaa ni kituko

suruali za "don't touch my shoe" kwa akina kaka

ila fashion nyingi zinarudi, leo hii jaribu kuvaa suruali ya bugaloo mtaani uone kesho yake tu watu kibao watakuwa wameiga. hata raizon na viatu vya wanchoma kumoyo vyote sasa hivi ni fashion
 
Chupi za VIP zimekumbusha mbali sana!! mafuta ya shanti, yolanda unajipaka siku maalum ukiwa na kidate, we acha tu, maisha haya, Mungu anajua!
 
Hizi ulikuwa ukifua zinapaa(kuwa ndogo) bana, yangu nikaongezea na kitambaa cha rangi tofauti kwa chini.. hahahaaaa bonge la mtoko na viatu vya TAFU (e.g Benqi).

Unazungumzia NDOPA enzi tunavaa suruali za TOKYO, BIG SAM; Usipokuwanayo sikukuu hata pilau halipandi.
 
79693402_191286652031264_3111588314281410560_n.jpg
 
Anzia mika y sabini mwishoni mimi nilikuta Crimplin hiyo wanavaa wenye hela,Jeans hazikuwepo kb zilizokuwepo japo zilifanana ziliitwa Lee na hizi lazima uwe umeletewa toka ulaya
ila common ilikuwa suruali bwanga halaf haina selebration na shati tait lazima liwe na mistari ndio kaka modo za siku hizi halaf chini unapiga Santana au Platform hiyo ilikuwa kwa rika zote , kichwa no bonge la Afro halafu unapiga way kama Waasia, Miaka ya 80 mwanzoni hali ilikuwa mbaya sana tukwa tunapiga Khaki iliyoitwa MaRIKANI, halafu ikafuatiwa na Kaniki hiyo ndio economic crisis ya dunia ;. Kuanzia 1985 zikaingia Bag wash,Big Sam, na Mashatiya Ujiuji ukilikosa hilo uadui na dingi, zikafuata viatu Mokasi ukiwa nacho mamanzi unachukua si mchezo, gogo za shule, na DH ndio yaani da. Reebok zilikuja lakini watu hawakuziweza kbu ya bei ispokuwa kwetu Arusha wa mererani walitamba nazo. Chupi za VIP siku umenunua unapandisha shati ili watu waone au kuchomekea shati kwa ndani ya chupi ili ibali nje japo si kata k kama siku hizi,hapo tukaacha afro tukawa tunanyoa Kibwenzi na Panki, miziki siku hizo ilikuwa Chiko Tchikaya, Chicco Chimora ,Pat Shange, Tchachaka, Alpha Blondy, Bob Marley na Michel Jackson nyingne za Kizungu

Miaka ya mwishononi 88,89,kukaja suruali za TOKYO, Sheriff,na Ujiuji na hapo miziki ikawa ya Kongo zaidi ila chini mokasi ukabadilika kidogo kb wapare walianza kutengeneza
Ilikuwa tamu sana si sasa hivi.
Mimi nilikuwa nadhani kuwa humu jukwaani naongoza kwa utu uzima, kumbe hapana, kumbe nami pia nina kaka zangu humu. Viatu vile vya Raise On, miaka ya mwanzoni mwa themanini pamoja na saa zile za disco. Baadaye sasa ndiyo zikaja suruali Michael Jackson, zikafuatiwa na zile zenye celebration unavalia tumboni. Jeans aina ya Lee nimeivaa mwaka 1983 pamoja na viatu vyaraba mtoni, soli ikiwa ina meno kama ya mamba, halafu ni ya kandambili hizi za kawaida.
 
Shati la ndege, moro shoes, tinabuu, dontach (don't touch), asante mchaga kiatu, safari boot na viatu vya mataili ya gari
Mkuu Zatara dontach saizi imerudi kwa kasi sana vijana wajanja wa town wanatupia hizo ni 🔥🔥
 
Anzia mika y sabini mwishoni mimi nilikuta Crimplin hiyo wanavaa wenye hela,Jeans hazikuwepo kb zilizokuwepo japo zilifanana ziliitwa Lee na hizi lazima uwe umeletewa toka ulaya
ila common ilikuwa suruali bwanga halaf haina selebration na shati tait lazima liwe na mistari ndio kaka modo za siku hizi halaf chini unapiga Santana au Platform hiyo ilikuwa kwa rika zote , kichwa no bonge la Afro halafu unapiga way kama Waasia, Miaka ya 80 mwanzoni hali ilikuwa mbaya sana tukwa tunapiga Khaki iliyoitwa MaRIKANI, halafu ikafuatiwa na Kaniki hiyo ndio economic crisis ya dunia ;. Kuanzia 1985 zikaingia Bag wash,Big Sam, na Mashatiya Ujiuji ukilikosa hilo uadui na dingi, zikafuata viatu Mokasi ukiwa nacho mamanzi unachukua si mchezo, gogo za shule, na DH ndio yaani da. Reebok zilikuja lakini watu hawakuziweza kbu ya bei ispokuwa kwetu Arusha wa mererani walitamba nazo. Chupi za VIP siku umenunua unapandisha shati ili watu waone au kuchomekea shati kwa ndani ya chupi ili ibali nje japo si kata k kama siku hizi,hapo tukaacha afro tukawa tunanyoa Kibwenzi na Panki, miziki siku hizo ilikuwa Chiko Tchikaya, Chicco Chimora ,Pat Shange, Tchachaka, Alpha Blondy, Bob Marley na Michel Jackson nyingne za Kizungu

Miaka ya mwishononi 88,89,kukaja suruali za TOKYO, Sheriff,na Ujiuji na hapo miziki ikawa ya Kongo zaidi ila chini mokasi ukabadilika kidogo kb wapare walianza kutengeneza
Ilikuwa tamu sana si sasa hivi.
hyo crimplin alikua anaisema mama yangu sijui ata ni vazi gani
 
Back
Top Bottom