Nguo na Mitindo ya Zamani ambayo kwa sasa ukivaa ni kituko

Sketi za charanga.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

charanga mbona za juzi kati tu. Mitindo ya kizamani ya kinadada ni pa1 na Mbilia bell, maksi sketi zenye mpasuo wenyewe walikuwa wanaziita Sina habari Nywele walikuwa wanachomo ama kwa pasi au kopo lenye mkaa wa moto.
 
Raba za aina ya DH,chachacha,LOSO....na maviatu flan ya plastic asubuhi yanachubua miguu sabab ya barid yanakua magumu sna..mchana yanachoma sabab yameshagain joto....
 
Suruali za uji uji! lo!!! long time.....

Dah kuna mchele mchele baba hiyo ilikuwa 1986 mpaka early 90s km huna baba wewe ----- tu. Nakumbuka form one hapo mkono wa mala sec kilosa kuna jamaa alikuwa frm4 akiitwa Manengo alikuwa anawatafuna mademu kinoma eti kisa suruali zake zote mchele mchele na mashati yake yote ni ya bahama hahahaha tehe jamani
 
Raba za aina ya DH,chachacha,LOSO....na maviatu flan ya plastic asubuhi yanachubua miguu sabab ya barid yanakua magumu sna..mchana yanachoma sabab yameshagain joto....

Unazungumzia NDOPA enzi tunavaa suruali za TOKYO, BIG SAM; Usipokuwanayo sikukuu hata pilau halipandi.
 
Anzia mika y sabini mwishoni mimi nilikuta Crimplin hiyo wanavaa wenye hela,Jeans hazikuwepo kb zilizokuwepo japo zilifanana ziliitwa Lee na hizi lazima uwe umeletewa toka ulaya
ila common ilikuwa suruali bwanga halaf haina selebration na shati tait lazima liwe na mistari ndio kaka modo za siku hizi halaf chini unapiga Santana au Platform hiyo ilikuwa kwa rika zote , kichwa no bonge la Afro halafu unapiga way kama Waasia, Miaka ya 80 mwanzoni hali ilikuwa mbaya sana tukwa tunapiga Khaki iliyoitwa MaRIKANI, halafu ikafuatiwa na Kaniki hiyo ndio economic crisis ya dunia ;. Kuanzia 1985 zikaingia Bag wash,Big Sam, na Mashatiya Ujiuji ukilikosa hilo uadui na dingi, zikafuata viatu Mokasi ukiwa nacho mamanzi unachukua si mchezo, gogo za shule, na DH ndio yaani da. Reebok zilikuja lakini watu hawakuziweza kbu ya bei ispokuwa kwetu Arusha wa mererani walitamba nazo.

Chupi za VIP siku umenunua unapandisha shati ili watu waone au kuchomekea shati kwa ndani ya chupi ili ibali nje japo si kata k kama siku hizi,hapo tukaacha afro tukawa tunanyoa Kibwenzi na Panki, miziki siku hizo ilikuwa Chiko Tchikaya, Chicco Chimora ,Pat Shange, Tchachaka, Alpha Blondy, Bob Marley na Michel Jackson nyingne za Kizungu

Miaka ya mwishononi 88,89,kukaja suruali za TOKYO, Sheriff,na Ujiuji na hapo miziki ikawa ya Kongo zaidi ila chini mokasi ukabadilika kidogo kb wapare walianza kutengeneza
Ilikuwa tamu sana si sasa hivi.
 
Back
Top Bottom