Ngumu lakini hakuna namna: Rais Magufuli mteue Mwigulu wizara ya fedha

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,652
2,628
Amani iwe kwenu..
Hata kama nitakuwa upande wa pili wa shilingi ila huyu bwana wa Iramba ana mazuri yake pia. Kwa tulipofika naomba Rais John Pombe Magufuli amteue Mwigulu awe waziri wa fedha.

Sababu;
1. Akiwa naibu serikali iliyopita alimfunika kabisa Saada Mkuya na kuleta matokeo chanya.

2. Ni mchumi anayejua hali halisi ya watanzania.

Mpeni Rais ujumbe huu, hali ni tete huku,japo wengine tunaolalamika hatukuwa mafisadi. CCM msiposhauri.. Tuacheni sisi mawe tushauri,hili taifa letu sote
 
Shida ni kwamba Mkulu hapendi kuonekana amekosea..

Akimteua hivi sasa Mwigulu itatoa picha kwamba uteuzi wake kwa Dr Mpango ulikuwa bomu.

Na kumbuka Mpango alimteua kwa mbwembwe.

Alimpa kwanza U Commissioner General wa TRA.. then akampa U Waziri baada ya kukusanya mapato vizuri pale TRA.

Lakini nakubaliana na wewe.. Mwigulu anapaweza Finance.

Mpango ameharibu Uchumi.
 
Mwigulu yuko poa na hata aliyepo yuko poa tatizo ni remote control iliyo ikulu... Yule jamaa ndo wakushauri aache watendaji alio wachagua wafanye kazi sawa sawa na Elimu na weledi wao...
Nadhubutu kusema watendaji wote walio chini ya raisi wanayo nidhamu ya uoga, wote wanaogopa na sijui uoga wao unajengwa na nn?
 
Mwafwaaaa! Akimtoa Mwigulu tena alipo italeta picha mbaya na huyu waziri wa fedha arudishwe nyumba TRA
 
Amani iwe kwenu..

Hata kama ntakuwa upande wa pili wa shilingi ila huyu bwana wa Iramba ana mazuri yake pia.

Kwa tulipofika naomba Rais John Pombe Magufuli amteue Mwigulu awe waziri wa fedha.
Sababu;
1.Akiwa naibu serikali iliyopita alimfunika kabisa Saada Mkuya na kuleta matokeo chanya.
2.Ni mchumi anayejua hali halisi ya watanzania.

Mpeni Mh..Ujumbe huu,hali ni tete huku,japo wengine tunaolalamika hatukuwa mafisadi.

CCM msiposhauri.. Tuacheni sisi mawe tushauri,hili taifa letu sote
WASHAURI wa RAIS at large/ Wasiojulikana toka JF?
Watanzania bhaana!!
 
Namimi naunga mkono hoja, namkubali sana Mwigulu kwenye uchumi, Yeye na Saada Mkuya walipiga kazi nzuri sana, Nadhani Wizara ya fedha ndo inayomfaa, Siyo wizara hii ya kutumia polisi kukandamiza demokrasia, kwanza wizara hii inamuharibia political future yake maana mbeleni miaka ijayo watu Watamuogopa kumpa dhamana kubwa kwa kuhofia kuwa ni dikteta anayeweza kutumia vyombo vya dola kukandamiza uhuru wa watu.
 
Amekutuma?
Achilia mbali kutumwa lakini mwigulu aliiweza sana wizara ya fedha chini ya JK sasa sijui chini ya huyu bosi mpya maana uongozi wowote bora ni ule wa kuvuta kwa pamoja na sio kuvutana. Ila kwa huyu tuliye naye sasa hapana mwigulu atapakazwa tope bure abaki hukohuko kijana wa watu ili awe salama maana kufanya kazi karibu na huyu boss mpya yataka moyo kwelikweli na uvumilivu wa hali ya juu sana.
 
Katika kuajiriwa, kama bosi wako hashauriki, hata mzuri namna gani haisaidii kitu!!!
 
Amani iwe kwenu..

Hata kama ntakuwa upande wa pili wa shilingi ila huyu bwana wa Iramba ana mazuri yake pia.

Kwa tulipofika naomba Rais John Pombe Magufuli amteue Mwigulu awe waziri wa fedha.
Sababu;
1.Akiwa naibu serikali iliyopita alimfunika kabisa Saada Mkuya na kuleta matokeo chanya.
2.Ni mchumi anayejua hali halisi ya watanzania.

Mpeni Mh..Ujumbe huu,hali ni tete huku,japo wengine tunaolalamika hatukuwa mafisadi.

CCM msiposhauri.. Tuacheni sisi mawe tushauri,hili taifa letu sote
Mkuu kwani Dr. Mpango siyo mchumi? Kwani Dr. Mpango hajui hali halisi ya Watanzania? Siamini kama Dr. Mpango hafanyi vizuri, naamini anafanya vizuri. Tatizo lililopo kwa kwamba kwa sasa wanaziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha za umma baada ya hapo wataweka misingi mizuri ya government spending ili ku stimulate uchumi kupitia private sector. Wanasema matumizi ya serikali kupitia private sector hayakuwa halisi na halali. Naamini baada ya muda watakuwa wamemaliza kuangalia na kuziba mianya na mambo yatakuwa murua. Tumpe Dr. Mpango nafasi apambane.
 
Mwigulu yuko poa na hata aliyepo yuko poa tatizo ni remote control iliyo ikulu... Yule jamaa ndo wakushauri aache watendaji alio wachagua wafanye kazi sawa sawa na Elimu na weledi wao...
Nadhubutu kusema watendaji wote walio chini ya raisi wanayo nidhamu ya uoga, wote wanaogopa na sijui uoga wao unajengwa na nn?
yupo poa japo hajui hata tafsiri ya VAT????
 
Hata Alfayo kidata pale tra hapamfai.mtaalamu wa masuala ya ardhi mambo ya fedha atayawezea wapi?toa wote.
 
Back
Top Bottom