Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,627
- 154,986
Ngumi yamuua dereva wa daladala
http://majira.co.tz/index.php?view=...adala&format=pdf&option=com_content&Itemid=57http://majira.co.tz/index.php?view=...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57 http://majira.co.tz/index.php?optio...kYWxhJm9wdGlvbj1jb21fY29udGVudCZJdGVtaWQ9NTc=
DEREVA daladala Bw. Geofrey Sendwa (32) mkazi wa Kitunda Kivule amefariki dunia baada ya kupigwa ngumi na dereva mwenzake wa daladala katika kituo cha Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.
Kondakta wa basi alilokuwa akiendesha marehemu, Bw. Vedasto Sinde aliambia majira kuwa dereva wake alipoteza maisha katika Hospitali ya Magomeni alipofikishwa baada ya kuangukia kisogo na kupoteza fahamu.
Alisema katika tukio hilo daladala lao likitokea Kariakoo kwenda Mbezi lilipofika eneo la Jangwani katika barabara ya Morogoro, dereva wake alikwepa baiskeli ya miguu mitatu (Guta) jambo lilimfanya aingia kulia.
Nyuma yao kulikuwa na daladala jingine lililokuwa likiendeshwa na Godliving Severini ambaye alihisi anachomekewa kuwahi abiria mbele, hivyo walipofika kituo cha Mapipa alizuia basi lao kwa mbele na kushuka.
"Marehemu aliniambia huyu dereva namfahamu kamsikilize anasemaje, ghalfa alishuka na kwenda kumshusha dereva wangu, alimpiga ngumi iliyomdondosha chini na kuzirai," alisema Kondakta huyo.
Alisema baada ya kutenda kosa hilo dereva huyo alitaka kukimbia lakini walimzuia na kumpeleka hospitali kupitia Polisi Magomeni, ambako alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na wao kumpeleka mgonjwa hospitali ambako alifariki dunia muda mfupi baadaye.
Shemeji wa marehemu, Bw. Edfass Bayella alisema ni kweli familia imepokea taarifa hizo na kuthibitishiwa na askari waliompokea ambao wamethibitisha amefariki.
"Walipomkamata dereva huyo walimfungulia shtaka la shambulio kwa faili namba MAG/RB/2390 la shabulio na lakini baada ya kifo nimeona limeandikwa mauaji, ni kweli shemeji yangu ameuawa," alisema Bw. Bayella
Alisema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Kitunda Kivule ambako ndugu wanapanga kuzika au kumsafirisha marehemu kwenda kwao Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga alikiri kutokea tukio hilo na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.