Ngumi yamuua dereva wa daladala

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,270


Ngumi yamuua dereva wa daladala
http://majira.co.tz/index.php?view=...adala&format=pdf&option=com_content&Itemid=57http://majira.co.tz/index.php?view=...nt&print=1&page=&option=com_content&Itemid=57 http://majira.co.tz/index.php?optio...kYWxhJm9wdGlvbj1jb21fY29udGVudCZJdGVtaWQ9NTc=

DEREVA daladala Bw. Geofrey Sendwa (32) mkazi wa Kitunda Kivule amefariki dunia baada ya kupigwa ngumi na dereva mwenzake wa daladala katika kituo cha Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.

Kondakta wa basi alilokuwa akiendesha marehemu, Bw. Vedasto Sinde aliambia majira kuwa dereva wake alipoteza maisha katika Hospitali ya Magomeni alipofikishwa baada ya kuangukia kisogo na kupoteza fahamu.

Alisema katika tukio hilo daladala lao likitokea Kariakoo kwenda Mbezi lilipofika eneo la Jangwani katika barabara ya Morogoro, dereva wake alikwepa baiskeli ya miguu mitatu (Guta) jambo lilimfanya aingia kulia.

Nyuma yao kulikuwa na daladala jingine lililokuwa likiendeshwa na Godliving Severini ambaye alihisi anachomekewa kuwahi abiria mbele, hivyo walipofika kituo cha Mapipa alizuia basi lao kwa mbele na kushuka.

"Marehemu aliniambia huyu dereva namfahamu kamsikilize anasemaje, ghalfa alishuka na kwenda kumshusha dereva wangu, alimpiga ngumi iliyomdondosha chini na kuzirai," alisema Kondakta huyo.

Alisema baada ya kutenda kosa hilo dereva huyo alitaka kukimbia lakini walimzuia na kumpeleka hospitali kupitia Polisi Magomeni, ambako alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na wao kumpeleka mgonjwa hospitali ambako alifariki dunia muda mfupi baadaye.

Shemeji wa marehemu, Bw. Edfass Bayella alisema ni kweli familia imepokea taarifa hizo na kuthibitishiwa na askari waliompokea ambao wamethibitisha amefariki.

"Walipomkamata dereva huyo walimfungulia shtaka la shambulio kwa faili namba MAG/RB/2390 la shabulio na lakini baada ya kifo nimeona limeandikwa mauaji, ni kweli shemeji yangu ameuawa," alisema Bw. Bayella

Alisema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Kitunda Kivule ambako ndugu wanapanga kuzika au kumsafirisha marehemu kwenda kwao Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga alikiri kutokea tukio hilo na maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.
 
R.I.P
DEREVA daladala Bw. Geofrey Sendwa (32) mkazi wa Kitunda Kivule amefariki dunia baada ya kupigwa ngumi na dereva mwenzake wa daladala katika kituo cha Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.

huyo atakuwa alipigwa ngumi ya chembe!
 
Mh! kweli tunatembea na kifo, yaani ngumi moja tu?
we dereva unaejifanya bondia utajuuuta!
 
Wacha afe manaake wao wakiwa wanaendesha daladala huwa wanatutesa sana madereva wa magari mengine madogo, wacha rife
ndugu usitukane mamba kabla hujavuka mto! kifo ni kifo tu, kiwe cha moto, ajali, au kuumwa! unadhani alipenda hivyo? au dereva aliyeua alikusudia kuua au alitaka kumpa maumivu tu? Nakuomba uombe radhi kwa kauli yako hiyo ambayo siyo ya kiungwana ukiwa kama mwana jamii
 
Bujibuji habari nilizozipata ni kwamba yule dereva amechukuliwa msukule na hao ndugu zetu wa kanda ya ziwa, nawe pia inaelekea ni wa kuko au sio?
 
Dunia tambara bovu, sasa mpiga ngumi kageuka asusa ya washkaji huko segerea kiulainiii kwa kujifanya mbabe wa barabarani! Atajuta kulenga ngumi nzito za mauaji! Wenzie wanapiga za kuvimbisha nundu tu yeye anapiga za kuua!
 
poleni wafiwa,thx buji kwa taarifa,smtime uncle nahisi kama ww ni ......................!
 
RIP. Inasikitisha. Hili pia ni fundisho kwetu sisi tusiwe wepesi wa kunyanyua mikono yetu kupigana na wenzetu. Ni mbaya kweli. It is really bad, hata huyo aliyepiga alikuwa hajakusudia kuua na ndiyo hajamfuatilia kumpiga wakati alipoanguka. Lakini inawezekana amezimia sasa kama ameshawekwa kwenye friji basi tena!
Moyo unaweza ukawa umesimama kusukuma damu lakini ubongo ukawa bado uko hai. Inatokea sana huku kwetu mtu kuwa pronounced amekufa haraka sana!
 
crocuta crocuta
user_offline.gif

crocuta crocuta has no status.
Junior Member
red_left.png
red.png
red_right.png
green_left.png

green.png

green_right.png
Join Date: Tue Feb 2010
Posts: 5
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
HAWA watoto sijui leo wamekula nini?
uhuru wa kutoa maoni sio uhuru wa KUBWABWAJA. yasiyo stahili....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom