Ngume kumeza:Hii ndio changamoto kubwa kwa TUCTA hivi sasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limesema changamoto kubwa iliyopo sasa kwa chama hicho ni uwepo wa idadi ndogo ya wafanyakazi waliojiunga katika vyama vya wafanyakazi hatua inayochangia kushindwa kufikia maelengo.

Katibu Mkuu wa Tucta, Dk Yahya Msigwa,aliyasema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya sherehe ya wafanyakazi ambayo hufanyika Mei Mosi ya kila mwaka ambazo mwaka huu zinafanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro

Kwa mujibu wa Tucta hadi sasa ni wafanyakazi 650,000 kati ya wafanyakazi 3.7 milioni waliopo nchini pekee ndio waliojiunga na vyama hivyo katika sekta rasmi hali inayochangia baadhi yao kutojua haki zao za msingi.

Chanzo:Mwananchi

My take:
You choose to be silent,we choose not to join you.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Watu wameacha kujiunga maana wameona hawawasaidi wafanyakazi bali wapo wapo tu, wanafanyakaz wana kero nyingi sana huko maofisini lakini hivyo vyama vimeshindwa wasaidia
 
Utaratibu wa kuanzisha vyama vya wafanyakazi upoje?
IPO haja ya kuwa na chama cha waliojiriwa 2005 na kuendelea. Maana Tunatofautiana malengo na mitazamo. Wa nyuma ya hapo washaanza kuwaza pensheni. Wengi waoga. Why viongozi wa vyama vya wafanyakazi wengi umri umewapiga mkono. Ni lazima kuwa na wakongwe?
 
Wakati wanaongea juzi na jpm walienda kuzungumza nae nn??, kwani sikuona wala kupata mrejesho wowote kwamba wafanyakazi watasaidiwaje kupata stahiki zao.. Zaidi nilisikia wakisifia tu
 
Wakati wanaongea juzi na jpm walienda kuzungumza nae nn??, kwani sikuona wala kupata mrejesho wowote kwamba wafanyakazi watasaidiwaje kupata stahiki zao.. Zaidi nilisikia wakisifia tu
Hii kazi inahitaji ujasiri hivyo kama huna huo ujasiri ni bora kutoiomba.
 
Utaratibu wa kuanzisha vyama vya wafanyakazi upoje?
IPO haja ya kuwa na chama cha waliojiriwa 2005 na kuendelea. Maana Tunatofautiana malengo na mitazamo. Wa nyuma ya hapo washaanza kuwaza pensheni. Wengi waoga. Why viongozi wa vyama vya wafanyakazi wengi umri umewapiga mkono. Ni lazima kuwa na wakongwe?
Mkuu umenena vyema..Hata ktk Fao la kijitoa hawajakaza maana umri wao wengi 56+ kwa hiyo ngumu kumfikiria kijana mwenye miaka 27,ambaye malengo yake kufanya kazi miaka 10 akajiajiri .Wanataka wote wastafu kama wao....
 
Mungu wangu! Dr. Yahya Msigwa ni katibu wa TUCTA! Mbona huyu daktari wa binadamu ni katibu mwenezi wa CCM Iringa mjini? Hadi hapa juzi tu nilimwona akieneza chama chake? Halafu anaendelea kueneza chama chake wakati huo ni daktari wa kuajiriwa na serikali, yaani ni mtumishi wa umma. Huyu ni daktari wa hospitali ya rufaa ya Iringa na wakati huo huo ni katibu mwenezi wa CCM Iringa Mjini. Hii hospitali ya rufaa ya Iringa ipo Iringa mjini na mbunge wa jimbo hili ni Mch. Peter Msigwa. Kama kweli huyu ni katibu wa TUCTA basi TUCTA haina tofauti na UVCCM. Jamani, huu sasa ni utani uliopitiliza.
 
Wakuwashangaa zaidi ni wafanyakazi wanaochagua watu wa aina hii.
 
Back
Top Bottom