pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,344
Tuzo la Premi Internacional Catalunya(kwa kicatalan) au El Premio Internacional Cataluña(kihispania) ni tuzo ambalo serikali ya Catalonia, Uhispania, imekuwa ikiwatunuku watu tofauti tangia mwaka wa 1989.
Tuzo hilo huwa linatunukiwa watu ambao wamebobea kwenye nyanja tofauti kote duniani na wakaigusa dunia kwa njia moja au nyingine. Waafrika wawili tu ndio wamepokea tuzo hilo, mmoja wao akiwa ni Desmond Tutu wa S.A.
Mwaka huu mwandishi mashuhuri kutoka Kenya, Ngúgí Wa Thiong'o, ndiye aliyetunukiwa tuzo hilo. Rais wa Catalonia kwenye hafla iliyopeperushwa live alisema kwamba Ngúgi Wa Thiong'o alitunukiwa tuzo hilo kwasababu ya juhudi zake. Kwenye kuhifadhi na kuendeleza mila, desturi, utamaduni na lugha za kiafrika.
Ngúgí alitoa hotuba ya kupokea tuzo hilo kwa lugha ya Gíkúyú, huku tafsiri ikitolewa kwa lugha ya kihispania. Ní thígio múno Ngúgi, njamba ya Kírínyaga, na Ngai arokúrathima múno.(Shukran kwake Ngúgí) *Hotuba ya Ngúgí inaanza @ 46:50.