Ngúgí Wa Thiong'o awahutubia Wahispania kwa lugha ya Gíkúyú baada ya Rais wa Cataluña kumtunuku tuzo la Premi Internacional Catalunya

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
Tuzo la Premi Internacional Catalunya(kwa kicatalan) au El Premio Internacional Cataluña(kihispania) ni tuzo ambalo serikali ya Catalonia, Uhispania, imekuwa ikiwatunuku watu tofauti tangia mwaka wa 1989.

Tuzo hilo huwa linatunukiwa watu ambao wamebobea kwenye nyanja tofauti kote duniani na wakaigusa dunia kwa njia moja au nyingine. Waafrika wawili tu ndio wamepokea tuzo hilo, mmoja wao akiwa ni Desmond Tutu wa S.A.

Mwaka huu mwandishi mashuhuri kutoka Kenya, Ngúgí Wa Thiong'o, ndiye aliyetunukiwa tuzo hilo. Rais wa Catalonia kwenye hafla iliyopeperushwa live alisema kwamba Ngúgi Wa Thiong'o alitunukiwa tuzo hilo kwasababu ya juhudi zake. Kwenye kuhifadhi na kuendeleza mila, desturi, utamaduni na lugha za kiafrika.

Ngúgí alitoa hotuba ya kupokea tuzo hilo kwa lugha ya Gíkúyú, huku tafsiri ikitolewa kwa lugha ya kihispania. Ní thígio múno Ngúgi, njamba ya Kírínyaga, na Ngai arokúrathima múno.(Shukran kwake Ngúgí) *Hotuba ya Ngúgí inaanza @ 46:50.

Tribalism shall never end in Kunyaland.
Sitegemei kajamba kama wewe ambaye huwa hasomi amjue au amuelewe Ngúgí Wa Thiong'o. Muacha mila ni mtumwa. Ngúgí ametunukiwa na anafahamika kote duniani kwasababu ya kazi yake nzuri ya kuendeleza na kuhifadhi mila, utamaduni na lugha za kiafrika.

Vitabu vyake huwa anaviandika kwa lugha ya kikuyu na vimesomwa na vikashinda tuzo nyingi kote duniani. Vitabu vyake vimetafsiriwa kwa lugha zaidi ya 90! Baadhi ya vitabu vyake; Weep Not, Child, A Grain Of Wheat, Dreams in a Time of War, Petals of Blood, The Trial of Dedan Kimathi, Devil on the Cross(Shetani Msalabani), The River Between, The Black Hermit, I Will Marry When I Want, In the House of the Interpreter, Wizard of the Crow n.k, n.k.
 
Magufuli nae anafanya kampeni kwa lugha ya Kisukuma.

Ukabila kamwe hautaisha Africa. Watu badala wapaishe UTAIFA bali wanapaisha UKABILA.
 
Magufuli nae anafanya kampeni kwa lugha ya kisukuma.

Ukabila kamwe hautaisha Africa. Watu badala wapaishe UTAIFA bali wanapaisha UKABILA.
Wao huko Catalonia, Uhispania walimtunukia tuzo kwa lugha ya kicatalan, lugha ya kwao Cataluña, sio kihispania. Yeye akawahutubia kwa Kikuyu, lugha ya mama. Unataka kusema kwamba Ngúgí alikuwa anaendeleza ukabila kwa kuwahutubia wahispania kwa lugha ya kikuyu? Kumbuka Ngúgí huwa anapigania kuhifadhiwa kwa lugha za asili za kiafrika, akiwarai waandishi wenzake kutoka Afrika waandike kwa kiyoruba, kiigbo, kizulu, kitsoha, kikikuyu, kimaasai n.k, badala ya kuandika kwa kiingereza au kifaransa. Kisha baadaye vitabu vyao vitafsiriwe kwa lugha zingine.

Sasa ukabila unaingiaje hapo? Ngúgí alisema hata kwenye hotuba hiyo hapo kwamba hakuna lugha yeyote ile ambayo ni muhimu zaidi ya lugha nyingine duniani. Sio Kiingereza, Kifaransa, Kireno wala Kiyahudi.
 
Magufuli nae anafanya kampeni kwa lugha ya kisukuma.

Ukabila kamwe hautaisha Africa. Watu badala wapaishe UTAIFA bali wanapaisha UKABILA.

Rais wenu anachimba mikwara kwa Kisukuma, bila shaka huo ni ukabila, maana unapotoa vitisho kwa watu huku ukitumia lugha isiyo rasmi kitaifa utakua unawabagua wengi ambao wanahitaji kujua nini hatima yao baada ya vitisho vyako, ila kwa huyu Ngugi alichofanya ni kutumia lugha yake ya asili kuhutubia watu ambao pia walitumia lugha yao ya asili wakati wanamtunuku.

Huwa nafurahi kumskliza Magufuli wakati anatumia lugha ya asili mara moja moja, ni ishara tosha anauenzi uafrika wake, ila pale anahutubia tena anachimba mikwara kwa kilugha inakua hatari.
 
Huyu jamaa nimeota usiku kuwa nimekutana nae mahali tukaelekea nyumbani kwangu nikamuandalia karamu kidogo huku tukifurahi na kucheka sana!
Sijui hii ndoto inamaanisha nini...
Nilishawahi kukutana nae tukaongea kidogo na kupiga picha za kumbukumbu!
Imebidi baada ya kushtuka niperuzi picha nilizopiga nikiwa nae niziangalie! Then naingia jf nakutana na uzi unaomhusu!
 
Sitegemei kajamba kama wewe ambaye huwa hasomi amjue au amuelewe Ngúgí Wa Thiong'o. Muacha mila ni mtumwa. Ngúgí ametunukiwa na anafahamika kote duniani kwasababu ya kazi yake nzuri ya kuendeleza na kuhifadhi mila, utamaduni na lugha za kiafrika. Vitabu vyake huwa anaviandika kwa lugha ya kikuyu na vimesomwa na vikashinda tuzo nyingi kote duniani. Vitabu vyake vimetafsiriwa kwa lugha zaidi ya 90! Baadhi ya vitabu vyake; Weep Not, Child, A Grain Of Wheat, Dreams in a Time of War, Petals of Blood, The Trial of Dedan Kimathi, Devil on the Cross(Shetani Msalabani), The River Between, The Black Hermit, I Will Marry When I Want, In the House of the Interpreter, Wizard of the Crow n.k, n.k.
Lakini huyu huyu ndiye aliyeandika Kitabu cha "This time tomorrow " kuhusu siasa mbovu za ubepari za Kanya, mkamfukuza na kumfunga na kumuita msaliti hadi leo mnafurahia ubepari wakati yeye unaupinga kwa nguvu zote.

Kumbuka kwamba ukabila Kenya ulisababishwa na viongozi na wasomi wakubwa hapo Kenya Kama Jommo Kenyatta, Moi, Jaramogi, Tom Mboya na Ngugi wa Thiong, kwa kutukuza makabila yao politically, intellectually or otherwise.
 
Wao huko Catalonia, Uhispania walimtunukia tuzo kwa lugha ya kicatalan, lugha ya kwao Cataluña, sio kihispania. Yeye akawahutubia kwa Kikuyu, lugha ya mama. Unataka kusema kwamba Ngúgí alikuwa anaendeleza ukabila kwa kuwahutubia wahispania kwa lugha ya kikuyu? Kumbuka Ngúgí huwa anapigania kuhifadhiwa kwa lugha za asili za kiafrika, akiwarai waandishi wenzake kutoka Afrika waandike kwa kiyoruba, kiigbo, kizulu, kitsoha, kikikuyu, kimaasai n.k, badala ya kuandika kwa kiingereza au kifaransa. Kisha baadaye vitabu vyao vitafsiriwe kwa lugha zingine. Sasa ukabila unaingiaje hapo? Ngúgí alisema hata kwenye hotuba hiyo hapo kwamba hakuna lugha yeyote ile ambayo ni muhimu zaidi ya lugha nyingine duniani. Sio kiingereza, kifaransa, kireno wala kiyahudi.
Catalonia ni wabaguzi na wanaukabila kama Kenya, wanataka kujitenga kwasababu ya ukabila wao. Ngugi wa Thiongo kwasababu yeye pia anaendekeza ukabika ndio sababu alitumia nafasi hiyo kuungana nao. Ulishamsikia PLO akizungumza kijaluo?, Nyerere, Mandela, Nkurumah au Sekoture wakizungumza lugha za makabila yao?
 
Wao huko Catalonia, Uhispania walimtunukia tuzo kwa lugha ya kicatalan, lugha ya kwao Cataluña, sio kihispania. Yeye akawahutubia kwa Kikuyu, lugha ya mama. Unataka kusema kwamba Ngúgí alikuwa anaendeleza ukabila kwa kuwahutubia wahispania kwa lugha ya kikuyu? Kumbuka Ngúgí huwa anapigania kuhifadhiwa kwa lugha za asili za kiafrika, akiwarai waandishi wenzake kutoka Afrika waandike kwa kiyoruba, kiigbo, kizulu, kitsoha, kikikuyu, kimaasai n.k, badala ya kuandika kwa kiingereza au kifaransa. Kisha baadaye vitabu vyao vitafsiriwe kwa lugha zingine. Sasa ukabila unaingiaje hapo? Ngúgí alisema hata kwenye hotuba hiyo hapo kwamba hakuna lugha yeyote ile ambayo ni muhimu zaidi ya lugha nyingine duniani. Sio kiingereza, kifaransa, kireno wala kiyahudi.
Waziri awasilisha ripoti ya nafasi za ajira serikalini kulingana na kabila
Endeleeni kucheza na ukabila muone kama hamtochinjana tena. Lugha ndio kitu cha kwanza na muhimu sana katika kuleta ukabila.

Kwa nchi za Kiafrica ni Tanzania pekee ndiyo iliyofanikiwa kumaliza ukabila, kitu cha kwanza ni kuzivunja nguvu lugha za makabila na kutukuza lugha moja tu ya Kiswahili, sasa ninyi endeleeni kushabikia wasomi wenu wenye kutukuza lugha za makabila yao.
 
Sio Mkenya kweli huyo Ngugi? upuuzi wa kubaguana na kuchinjana kwao wanahamishia kwa wengine hovyo sana Kenya
 
Ukiskiza reasoning ya Watanzania hapa JF unashindwa kuamini. What about those in the villages without education?
 
Kama inatamkwa "ngo" kwa nini inaandikwa "ngu"?
Ú, huwa haitamki sawa na U, na I pia huwa haitamki sawa na Í. Ngú/gí ni tofauti sana na Ngu/gi ila zinakaribiana sana na go/ge. Wanaolewa kikikuyu nipeni support jamani. Najua labda hujanielewa ila itakuwa ni kibarua kigumu sana kukueleza bila audio.
 
Ukiskiza reasoning ya watanzania hapa JF unashindwa kuamini.
what about those in the villages without education?
Watanzania hao hao wameweza kushinda ukabila, rushwa, nepotism, hunger, crime and crime.
 
Rais wenu anachimba mikwara kwa Kisukuma, bila shaka huo ni ukabila, maana unapotoa vitisho kwa watu huku ukitumia lugha isiyo rasmi kitaifa utakua unawabagua wengi ambao wanahitaji kujua nini hatima yao baada ya vitisho vyako, ila kwa huyu Ngugi alichofanya ni kutumia lugha yake ya asili kuhutubia watu ambao pia walitumia lugha yao ya asili wakati wanamtunuku.

Huwa nafurahi kumskliza Magufuli wakati anatumia lugha ya asili mara moja moja, ni ishara tosha anauenzi uafrika wake, ila pale anahutubia tena anachimba mikwara kwa kilugha inakua hatari.
Miafrika bana.

Pambaneni na umasikini. Kuzungumza mijilugha yenu hautawboreshea maisha wala kufuta colonial legacy.

Focus kwenye mambo ya msingi
 
Back
Top Bottom