Ngozi kufubaa na kuwa kavu. Ni mafuta gani mazuri ya kupaka sehemu za baridi?

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
1,457
2,435
Salutations kwenu!

Nipo Iringa wakuu baridi ni kali sana. Tangu nifike nimeona ngozi yangu ikiharibika sana sana.

Hapo kabla ya kuja Iringa, nilikuwa naishi Pwani. Nilikuwa sipaki mafuta na ngozi ilikuwa nzuri tu. Sasa baada ya kuja Iringa na kutokana na baridi nimekuwa napaka mafuta ya mgando ili kufanya ngozi isiwe kavu lakini bado haisaidii.

Naweza kupaka mafuta lakini baada ya nusu saa yale mafuta yanakauka na ngozi kuwa kavu kama mwanzo.

Je, ni mafuta au kitu gani kizuri cha kupaka au kutumia ili kuifanya ngozi iwe nzuri?

Rangi;- Maji ya kunde.
Jinsia;- ME
 
Nilienda Mbeya Jumatatu nikakaa siku nne tu ila uso wangu umeanza kubanduka maganda..
Baridi ya huko siyo poa aiseeh
Huu ukanda kwa barid ni noma mkuu yaan hata kunywa maji ni shughuli.

Sometimes hadi nasahau mara ya mwisho kunywa maji ni lini.

Vipi umetumia mafuta gani?
 
Si kwamba naogopa au sitaki kunywa maji kwa sababu ya baridi ila nakosa kiu kutokana na ubaridi.

Yaani hadi ukumbuke kunywa either kwa kuyachemsha n.k.
Kuna zile app za kukumbusha wakati wa kunywa maji, itakuwa ya muhimu kwako. Kweli wakati wa baridi, kiu hukatika ila maji hatufai kuacha kunywa, maximun of 8 glasses a day to avoid dehydration.
 
Ni mafuta gani ya mgando unayotumia?
Kama Ni baby care , rays na yanayofanana na hayo hayatakusaidia,
Ukiwa sehemu au kwenye nyakati za baridi na hewa kavu kama nyanda za huko ni vizuri kutumia vipako vizito ambavyo vitakuletea joto pamoja na kutunza unyevu nyevu wa ngozi yako usipotee na kusababisha kukakamaa na kubabuka kwa ngozi.


Tumia vaseline na glycerin tena upake ukishatoka kuoga/kunawa kabla mwili haujakauka ili yashikane vizuri na ngozi, vitakusaidia kukinga kwa kiasi kikubwa dhidi ya uharibifu wa ngozi yako.
 
Back
Top Bottom