Ngoswe: Penzi Kitovu Cha Uzembe

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
Ngoswe:
Penzi Kitovu Cha Uzembe
by Edwin Semzaba

long time wenye data mtuambie kitabu hiki kilikuwa na dhima gani kwa jamii??mie nakumbuka tu kama kilikuwa kinaelezea mambo ya ufisafi hv na wahusika walikuwepo kama ngoswe mwenyewe na mzee ngengemkeni mito mingi hv bado kinatumika mashuleni kwenye fasihi ya kiswahili?
 
Moyo ulishikwa ganzi>>>mwili ukatetemeka
Nilijawa na simanzi>>>mwili jasho ukatoka
Kwa kuupenda uzinzi>>>kazi imeharibika
KweLi mapenzi na kazi>>>haviendani hakika.

Kweli mapenzi na kazi>>>haviendani hakika
Ukitaka chapa kazi>>>penzi silipe dakika
Hili nalisema wazi>>>kwakua yamenifika
Tenda kazi kwa bidii>>>mapenzi pembeni weka

Baadhi tu ya mistari ya kajitabu haka!
 
bado kinatumika ni kitabu cha kujibia swali la tamthilia.
kilikuwa kinafundisha kutokuchanganya mapenzi na kazi, kama ngoswe alivyofanya akaharibu kazi karatasi za sensa zikachomwa na mzee mitomingii,
na pia kinaelezea madhara ya imani za kishirikina kwenye jamii nyingi za kitanzania, watu walidhani wanaohesabu watu ni wachawi tu kwa ajili ya kuwala nyama.
dah1 nakumbuka mbali sana those days
 
Nakumbuka vijitabu vile vilikuwa vizuri sana .... sikuhizi hawavitumii mkuu sijui what happened!
 
tatizo serikali kila kukicha wanabadili mtaala mie naona kama enzi zile elimu ya bongo ilikuwa na thamani sana kuliko sasa!maana hata mashuleni msingi kulikuwa na vipindi kwa sanaa,muziki na michezo man ila kwa sasa hakuna kabisa!
 
Nakumbuka vijitabu vile vilikuwa vizuri sana .... sikuhizi hawavitumii mkuu sijui what happened!
Sijui kamatz inaweza rudi tena kama enzi zile maana mtu alikuwa anasoma kwa kuelewa na sio kukaririshwa kama sasa!
 
hakika kilikuwa kitabu cha kusisimua..mapenzi, ndoa za mitara, uzembe kazini vyote vilielezewaa kwa lugha tamu na yakufundishaaaa..

nilikipenda sana kitabuu hiki
 
tatizo serikali kila kukicha wanabadili mtaala mie naona kama enzi zile elimu ya bongo ilikuwa na thamani sana kuliko sasa!maana hata mashuleni msingi kulikuwa na vipindi kwa sanaa,muziki na michezo man ila kwa sasa hakuna kabisa!

siku hiz hamna halafu vitabu vimebadilishwa sana na masomo, ndo maana watoto hawafanyi vizuri, lakini nasikia serikali inataka kuanzia sasa nchi nzima itatumia kitabu kimoja, hakuna mambo ya vitabu vingi, lakini hiyo pia itawafanya watoto wakose maarifa kwa sababu kila mwandishi wakitabu ana uelewa wake
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom