Ngosha kalishwa limbwata

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
FB_IMG_1490292035452.jpg


Ngosha kapawa limbwata, hajiwezi mtimani,
Alivyo kama zezeta, kapoteza umakini,
Mwepesi kukunja ndita, kumlinda mwafulani.

Uchao azua vita, athama Bwana fulani,
Sasa kuna vutavuta, ndani hawaelewani,
Watu apeleka puta, kama mbuzi hitimani.

Hasikii wanoita, kiumbe hawezekani,
Pia hataki kuwata, watu wanayolaani,
Hebu fanyeni kumwita, wazee mwaogopani?

Haya hatukuyaota, wala hatukuyadhani,
Kama atawakung'uta, hata wake wa ubani,
Malaika tulopata, amegeuka shetani.

Hivi leo ameshuta, kachafuwa hewa ndani,
Tena ule wa tatata, kama honda la zamani,
Sasa yanalia mbwata, kisa kapata jamani.

Zinatosha beti sita, kalamu naweka tini,
Nachelea kunikuta, kama ya kamanda Beni,
Mkaanza nitafuta, kama vile marijani.

23 Machi 2017 Alhamis 21:08

JiniKinyonga
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatsp 0622845394 Morogoro.
 
Aisee limbwata alilolishwa Ngosha sio la nchi hii kabisa
 
Jifunze uchawi, limbwata haifanyi kazi kwa watu wa jinsia moja. lol
in case likitokea kufanya kazi basi huwa ni la kipekee.
 
Naona umeweka na mawasiliano kabisa, ili mbowe akupe kile cheo cha ben saa tisa, maana zitto kashakutumia vya kutosha
 
Back
Top Bottom