Ngo's Zimekuwa Deal Tanzania

Nshomile

Member
Nov 21, 2007
48
0
Antiqua"]Ndugu zangu, tumejadili sana habari za madini. Ni sawa, lakini Je vipi hawa watu wanaoanzisha NGO'S kusingizia watoto yatima? Hatuoni kwamba haya mashirika yametajirisha watu binafsi kuliko malengo yenyewe? Hawa yatima wanapata misaada mingi kupitia haya mashirika lakini matokeo yake wachache wanajinufaisha. Je hii inatofauti na hawa mafisadi. Mimi nawaweka kwenye page moja yenye malengo sawa mabaya ya kuharibu maendeleo yetu. Ukizingatia hizi NGO'S hazilipi kodi. Ebu tulichangie mawazo kidogo kwa wenye utafiti na hili.
 

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,021
2,000
Ukienda wilayani utadhani NGO ndo zimereplace role ya serikali! Ngos zinakuwa nginyi hasa Tz kwa kuwa serikali saa ingine inashindwa kutimiza wajibu wake!
 

Nshomile

Member
Nov 21, 2007
48
0
Mimi niko huku california na nimekuwa nikiona masponsor kibao ambao wanajihusisha na makampuni hewa huku Tz, na wakienda kukagua shughuli zinazofanyika kule kwa watoto yatima, yanayoonekana ni madogo kuliko $$$ wanazotuma kusaidia. Idadi ya watoto wa namna hii ni nyingi mno, na ukiangalia hali zao inasikitisha. Sasa tunapopata watu wa kusaidia kwenye kupitia haya makampuni inabidi serikali iwke mkono wake kwenye hayo makampuni binafsi kuhakikisha pesa hii inawasaidia watoto hawa. Watanzania hatuna huruma jamani, yaani pesa ya kusaidia kitu kama hiki unajengea ghorofa yako?
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
109,447
2,000
Mama Mkapa alipewa pesa chungu nzima na Bill Gates ili kusaidia wagonjwa wa ukimwi Tanzania kupitia NGO ya Anna Mkapa. Hadi hii leo haijulikani kiasi halisi alichopewa na wala alichotumia. Inawezekana kabisa ametumia kiasi kidogo sana na zilizobaki zimemnufaisha yeye na familia yake.

Mama Kikwete naye alitembelea Oman kama sikosei mwaka jana au huu na kupewa $200,000ili kusaidia watoto yatima. Haijulikani kiasi gani kimetumika hadi sasa, inawezekana kilichotumika ni kidogo sana.

Kwa maoni yangu wake au waume wa viongozi wa juu wasiruhusiwe kuwa na NGO au kuwe na udhibiti wa hali ya juu na kuwataka waweke records za mapato na matumizi ambayo ni lazima yakaguliwe na wakaguzi kila mwaka kuhakikisha NGO hazitumiki na vingunge kama mradi wa kujitajirisha.
 

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
195
Kwanza kwa Tanzania kupata kazi kwenye NGO nyingi ni big deal, maana ndio unakaa mkao wa kula, mradi uweze kuandaa(au sijui niseme kufyatua) ripoti za kuwapelekea wadhamini. Hata hivyo natambua kwamba ziko NGO nyingine ambaza kweli zinatimiza majukumu au niseme malengo yake ipasavyo.

Ndio maana utakuta wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanapigana vikumbo kutuma maombi kwenye asasi zisizo za kiserikali badala ya kufuatilia fani zao wanazosomea. Ninafahamu wahandisi majengo ambao sasa wanatoa ushauri nasaha kuhusu ukimwi katika asasi moja maarufu nchini.

Kwa mtaji huu sekta zingine hazina budi kupwaya siku za usoni.
 

Kasana

JF-Expert Member
Apr 3, 2007
418
225
Sasa tunapopata watu wa kusaidia kwenye kupitia haya makampuni inabidi serikali iwke mkono wake kwenye hayo makampuni binafsi kuhakikisha pesa hii inawasaidia watoto hawa.

kaka unaongelea serikali ipi ya Tanzania? ambayo inatafuna pesa kama hizo NGO.
Public -Private Mix/Partneship ni nzuri kuinua hali ya wananchi kama zote zitatimiza malengo.
 

MiratKad

JF-Expert Member
May 2, 2008
294
170
Hivi wakuu kuna mtu anaweza kutupatia taarifa za NGO mbalimbali kama zinatimiza wajibu wake? Tuelekeze kwenye website zao kama mnazifahamu...
 

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,740
1,225
Let's be specific please, lest we conundrum the proverbial "mtego wa panya uwanasao watakiwao na wasiotakiwa"
 

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
`Ni kweli matokeo ya kuwa ngo utitiri hayaonekani.
Lakini siyo sababu wana JF kuanza kulipiza hasira kwa individuals, kabla ya kutaja jina, fanya utafiti, unashushia hadhi forum yetu.
kama kuna mtu anafahamu ngo ambayo mahesabu yake hayaridhishi, ndiyo anahaki ya kusema.
HADHI YA FORUM INASHUKA KWA AJILI YA KUENDEKEZA MAJUNGU, NA MAAMUZI YA HASIRA DHIDI YA MTU AU KIKUNDI.
FACTS ZENYE TIJA KWA TAIFA NDIO ZINATUTOFAUTISHA NA MAGAZETI YA UDAKU.
 

BadoNipo

Senior Member
Jul 4, 2008
175
0
ni ukweli usiopingika kuwa kuna ngo's kibao ambazo hazina faida kabisa kwa walengwa. wanajinufaisha wao wenyewe tu kwa kujenga majumba ya kifahari na kuendesha magari ya kifahari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom