NGO's vs Serikali vs Biashara: Nani anaweza kutatua changamoto za kijamii?

Izzi

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
553
1,107
Coronavirus limekuwa ni janga kubwa la kijamii. Lakini, kwa bahati mbaya, sio janga pekee la kijamii ambalo dunia inalikabili kwa mwaka huu 2020.
  • Mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Kuongezeka kwa 'gap' la walionacho na wasionacho.
  • Ongezeko kubwa la watu.
  • Mgawanyo usio sawa wa matumizi ya rasilimali.
  • Ukosefu wa ajira.
  • Wafanyakazi kufutwa kazi kwasababu ya kuingia kwa teknolojia (automation).
  • Rushwa.
  • Ukosefu wa elimu bora.
  • Ongezeko la 'Obesity'.
  • Magonjwa sugu.
  • Njaa.
  • Vita.
  • Na kadhalika. (Listi ni ndefu)
NI NANI WA KUTATUA CHANGAMOTO HIZI ZA KIJAMII?
By default na kwa miaka mingi jibu lilikuwa rahisi tu; ni serikali. Huwa tunaifikiria serikali - au labda NGOs na mashirika yaliyoanzishwa na matajiri wakubwa duniani. Ni kweli, wote wanafanya kazi kubwa sana. Lakini pengine kazi kubwa zaidi inaweza kufanywa na yule ambae wengi hawamfikirii - Makampuni ya kibiashara.

Utauliza, makampuni ya kibiashara yanawezaje kutatua changamoto za kijamii? Wao si wanachoangalia ni faida tu au? Naomba nikujuze - ukweli ni kwamba 'Purpose' na 'Profit' huwa havitengani kuliko wengi wanavyofikiri.

KWANINI NGOs NA SERIKALI PEKE YAKE HAZIWEZI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIJAMII?
Nimesoma mara kadhaa kuwa, Rais Obama, kila akiwa anakabiliwa na changamoto ambayo anahitaji ufumbuzi - alikuwa anawaita wajasiriamali waende ikulu ili wampe mawazo. Na ofcourse alikuwa anafanikiwa. Nimesikia pia marais wa nchi nyingine kadhaa wanatumia huo mfumo. Marais hawa wanaamini kitu kimoja - Business can solve any problem. Swali ni kwanini serikali peke yake haiwezi? Kwanini NGOs pia haziwezi?

Kwanza; miradi mingi ya kiserikali huwa na malengo ya kisiasa. Kwa hiyo, uendeshaji wake unakuwa wa kisiasa-siasa; wasimamizi wanapatikana kisiasa, wanufaika wanahudumiwa kisiasa, n.k. Siasa na utaalamu havikai zizi moja.

Pili; kampuni za kibiashara zina kitu ambacho kwenye Serikali na NGO’s / mashirika kinakosekana: scale. Kampuni za kibiashara zina rasilimali nyingi zaidi, na hivyo zina uwezo mkubwa zaidi wa ku-promote mabadiliko ya kijamii kwa kasi na kwa ufanisi zaidi. Badala ya kuunganisha rasilimali tofauti tofauti, mahitaji na matakwa ya NGOs 1,000 - tunaweza kuwa na kampuni ya kibiashara moja tu inayoweza kutatua changamoto kwa kiwango sawa na NGOs 1,000.

Tatu, kampuni za kibiashara zimeanza kuona kuwa kutatua changamoto za kijamii kunaleta faida kubwa. Mfano kuna kampuni inazalisha viatu vinaitwa TOMS shoes, ambayo ina mfumo unaitwa “One for One”. Ukinunua pea moja ya viatu vya TOMS, unakuwa umemuwezesha mtu mmoja mwenye uhitaji kupata pea moja ya viatu. Ukinunua pea mbili, unakuwa umewasaidia watu wawili, pea tatu watu watatu, pea milioni moja watu milioni moja n.k

KAMPUNI IKIWAFAIDISHA WATEJA (JAMII) WAWEKEZAJI WANAFAIDIKA VIPI?
Well, utafiti unaonesha kuwa kampuni zinazo-'deliver value' kwa jamii ndizo kampuni zinazofanya vizuri zaidi - na ile 'purpose' yao inapelekea wapate faida kubwa zaidi, badala ya faida kuwafanya watafute 'purpose'. Ni kweli, hili ni wazo gumu kibiashara.

Wamiliki/ viongozi wengi wa makampuni wanaendesha biashara zao kwa mtazamo wa "Mgao wa keki". Wanaiona value ambayo wanaitengeneza kwa jamii kama keki isiyoongezeka ukubwa. Kipande chochote cha keki hiyo kikikatwa na kupelekwa kwa jamii kinapunguza kiasi cha keki watakachokula wawekezaji. Kwahiyo wanachofanya ni ku- maximise profits kwa kuinyonya jamii - kupunguza mishahara, kupandisha bei za bidhaa, au kupuuza madhara ya biashara yao kwa mazingira. Lakini ushahidi una-support mtazamo mpya - "Keki inayoongezeka ukubwa". Kampuni ikiweka kipaumbele cha ku-create social value, haiwapunguzii mgao wa keki wawekezaji wake bali inaongeza ukubwa wa keki yenyewe; na matokeo yake wawekezaji wanapata mgao mkubwa zaidi. Faida inabaki kuwa jambo muhimu, lakini inapatikana kama by-product ya kuihudumia jamii tofauti na kampuni nyingi zinavyofanya.

OK, KWAHIYO KAMPUNI INAONGEZAJE UKUBWA WA KEKI?
Kwanza ni ku-define purpose ya kampuni – Kwanini ilianzishwa, kwanini ipo, na ina mchango gani kwa jamii. Purpose ya kampuni ni jibu la swali hili; “how is the world a better place by your company being here?” Muhimu zaidi, purpose inatakiwa kuwa focused. Kampuni nyingi zina purpose ambazo ni mtambuka (broad purpose statements), mfano “to serve customers, colleagues, suppliers, the environment, and communities while generating returns to investors,” na wanafanya hivyo kwasababu zinavutia kuzisoma.

Lakini purpose ambayo inalenga kufanya kila kitu kwa kila mtu huwa inaleta matokeo hafifu sana. Viongozi wa makampuni wanahitaji kufanya maamuzi magumu ambayo pengine yanafaidisha kundi moja na kuliumiza kundi jingine. Ukifunga kiwanda kinachofanya uchafuzi wa mazingira unasaidia kutunza mazingira kwa faida ya wengi lakini unawaumiza wafanyakazi ambao watakosa kazi.

Of course, purpose statement peke yake haitoshi - inahitaji kufanyiwa kazi. Kuna kampuni nchini marekani inaitwa CVS - ilitengeza faida kubwa kupitia biashara ya kuuza sigara. Ikafika mahali wakaamua kubadili purpose yao. Hivyo wakabadilisha mpaka jina la kampuni, kutoka CVS na kuwa “CVS Health”. Lakini hawakuishia kubadili jina tu - wakaacha kuuza sigara pia ili kuendana na puspose yao mpya ambayo ni “helping people on their path to better health”. Hapo ndipo umuhimu wa kuwa na focused purpose statement unapokuja kwasababu inaisaidia kampuni kujua nini wafanye na nini wasifanye.

Viongozi wa leo wa makampuni wana fursa nzuri zaidi, teknolojia inawawezesha kuifikia dunia nzima na hivyo wana nguvu zaidi ya ku-create social value kuliko ilivyowahi kuwa. Na kuna ushahidi ulio wazi ambao wanaweza kuusimamia: To reach the land of profit, follow the road of purpose.

NINI JUKUMU LA SERIKALI?
Serikali haiwezi kufanya biashara - angalia makampuni mengi yanayomilikiwa na serikali utaelewa ninachomaanisha. Badala ya serikali kuwa mtatuzi pekee wa matatizo, inatakiwa itengeze mazingira ambayo problem solvers wanashamiri na kufanikiwa. Naomba niandike kwa Kiinglishi kwa msisitizo - Instead of sole problem solver, government’s role is to create an environment where problem solvers can flourish.

Serikali za nchi mbalimbali duniani zinatengeneza "accelerators" kwaajili ya "social entrepreneurs na startups" ambazo zinatatua changamoto za kijamii wakati huo serikali inaweza sera, sheria na kanuni rafiki kwa bidhaa zinazotengenezwa. Accelerators kazi yake ni kuhakikisha startups zina- scale up bidhaa na huduma zake zinaleta matokeo yanayokusudiwa. Katika maeneo mengine - kampuni, serikali na NGOs zinashirikiana kutatua changamoto za kijamii.

BOTTOM LINE
Watumishi wa serikali waache mentality ya 'mabeki' - waache kukaba kila saa - wawe 'viungo wachezeshaji' wasaidie magoli yafungwe magoli mengi. It's a win win situation.
 
Umesema vyema. Hasa hapo kwenye " Serikali haiwezi kufanya biashara". Lakini unatakiwa kujua mfumo wa kiitikadi wa uzalishaji na utawala wa nchi yetu Ni UJAMAA. Na katika kipindi cha awamu mbili ya 3 na 4 tumejitahidi kuukimbia ujamaa na kuforce kuingia UBEPARI lakini tumeshindwa.


Haya uliyoyaeleza na kuyashauri hayawezi kufanya kazi kama hatutabadili mifumo yetu uzalishaji na utawala. Makubaliano yetu ya 1977 ya namna ya kuendesha nchi ni UJAMAA(COMMUNISIM). Ili haya uliyoyasema yatumike lazima tuwe na mfumo mzuri wa uzalishaji unaoakisi uhalisia wa watu kujengewa uwezo wa kuzalisha na si kuitegemea serikali kuzalisha kwa ajili yao. Nazungumzia UBEPARI(CAPITALISM). Kwamba watu wapewe na wawezeshwe katika kurelease potential waliokuwa nayo au waliyoipata shuleni na vyuoni.

Ahsante.
 
Umesema vyema. Hasa hapo kwenye " Serikali haiwezi kufanya biashara". Lakini unatakiwa kujua mfumo wa kiitikadi wa uzalishaji na utawala wa nchi yetu Ni UJAMAA. Na katika kipindi cha awamu mbili ya 3 na 4 tumejitahidi kuukimbia ujamaa na kuforce kuingia UBEPARI lakini tumeshindwa.

Biashara
Haya uliyoyaeleza na kuyashauri hayawezi kufanya kazi kama hatutabadili mifumo yetu uzalishaji na utawala. Makubaliano yetu ya 1977 ya namna ya kuendesha nchi ni UJAMAA(COMMUNISIM). Ili haya uliyoyasema yatumike lazima tuwe na mfumo mzuri wa uzalishaji unaoakisi uhalisia wa watu kujengewa uwezo wa kuzalisha na si kuitegemea serikali kuzalisha kwa ajili yao. Nazungumzia UBEPARI(CAPITALISM). Kwamba watu wapewe na wawezeshwe katika kurelease potential waliokuwa nayo au waliyoipata shuleni na vyuoni.

Ahsante.
Biashara
 
Back
Top Bottom