Kwanini Waziri mkuu anakuwa na siasa za kitoto kiasi hiki?
Kwanini aongee uongo mkubwa namna hii?
Kassim Majaliwa ni mwongo sana unakumbuka hata wakati wa kifo cha mwendazake,alisema Rais ni mzima na anaendelea na kazi zake,je huyo ni wa kumwamini??
 
Nyumbu bhana...kwani PM alitoa kauli hiyo muda gani na kifo kimetokea muda gani?, kauli ya PM ilikuwa mahsusi kwa clip ya juzi yake na si juzi wala jana.
Shida ya kauli ya PM ni kuwa Ngorongoro kuko shwari hakuna kinachoendelea..
Wakati huo ametuma mama ya Maninja wanachinjana na wamaasai... matokeo yake ndo haya. Hao polisi walikuwa kutalii?
 
MONGELLA: ASKARI AMEUAWA KWA MSHALE LOLIONDO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amethibitisha kutokea mapigano Wilayani Ngorongoro katika eneo la Loliondo ambapo askari polisi mmoja aliuawa jana Julai 11, 2022

“Alasiri ya jana (Julai 11) askari mmoja aliuawa kwa kupigwa mshale na kundi la watu lililotokea likitaka kuathiri zoezi la kuweka alama,” - Mongella

Aidha, RC Mongela amesema hakuna kituo chochote cha Afya ama hospitali yenye majeruhi na ameomba kama wapo wajitokeze.
Kassim majaliwa anapaswa kujiuzulu kwa kutoa taarifa ya uongo bungeni. Sijui jiwe aliona nini mpaka akampa cheo kikubwa mtu mwongo na asiyejua nini kama majaliwa
 
Kwanini Waziri mkuu anakuwa na siasa za kitoto kiasi hiki?
Kwanini aongee uongo mkubwa namna hii?
Hekima saa nyingine inatakiwa ili kutochochea vita
Mapigano yeyote inaweza ikamalizwa kwa propaganda hata kama ikibidi kuweka uongo
 
Hekima saa nyingine inatakiwa ili kutochochea vita
Mapigano yeyote inaweza ikamalizwa kwa propaganda hata kama ikibidi kuweka uongo
No sio ujinga huu.
Mimi nilimsifu kwa juhudi za awali sio ujinga huu.
Kwa hali ilivyo hakutakiwa kuhudhuria bungeni badala yake angeongoza timu ya maridhiano eneo la tukio.
 
MONGELLA: ASKARI AMEUAWA KWA MSHALE LOLIONDO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amethibitisha kutokea mapigano Wilayani Ngorongoro katika eneo la Loliondo ambapo askari polisi mmoja aliuawa jana Juni 10, 2022

“Alasiri ya jana (Juni 10) askari mmoja aliuawa kwa kupigwa mshale na kundi la watu lililotokea likitaka kuathiri zoezi la kuweka alama,” - Mongella

Aidha, RC Mongela amesema hakuna kituo chochote cha Afya ama hospitali yenye majeruhi na ameomba kama wapo wajitokeze.
Hao majeruhi hawana akili! Yaani wajitokeze ili wakamatwe! Mkuu wa Mkoa hayuko serious hata kidogo.

Na kama hakuna mapigano, huyo askari ilikuwaje akapigwa huo mshale? Naona nguvu kubwa inatumika kuficha huu mgogoro!
 
Hili Taifa tumerogwa. Nilisema jana huyu waziri mkuu atoke tu lakini wakaja juu Sasa ona mambo yote hadharani. Siku zote njia ya mwongo nifupi. Mkuu wa mkoa wa Arusha amesema askari wao kafa kwa mshale chanzo ni vita inayoendelea Kati ya wamasai na polisi. Jana waziri mkuu alikanusha na kusema loliondo ni shwari. View attachment 2257218
Hawa jamaa wanaleta siasa kwenye mambo yenye madhara makubwa kwa Taifa! Mara hao Wamasai wanatoka nchi jirani! Mara hakuna aliyejeruhuwa! Mara picha ni za miaka 3 iliyopita!

Yaani siasa na propaganda kila sehemu!
 
Utakuta vurumai zote hizo eti wanataka wamasai waondoke kisa kuna mwekezaji anataka aende pale.

Si ni ubwege huo?.....eeh ubwege kabisa huo!!!
 
Back
Top Bottom