Ngorongoro inaangamia, tuache Siasa kwenye ukweli

Wanabodi JF!,

Nawasalimia popote pale mlipo!
Naomba niende kwenye Mada hii kuhusu NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY.(NCAA).

Nimefuatilia mijadala mbalimbali ambayo imekuwa ikiendelea kwenye social platforms,takriban muda wa wiki moja na ushei sasa.
Parody la mshambuliaji hili. Period
 
Umeua mkuu....akirudi nitag
Mimi sihitaji kusoma tafiti ya mtu wakati binafsi nina miaka zaidi ya thelathini nikiwa katika eneo husika.

Hao watafiti huja kuandika kwa kuhoji watu kwa kipindi fulani na kuondoka lakini mimi ninielewa eneo hilo kuanzia Loduare mpaka Wasso kule Loliondo.

Ninaijua milima yote na nimeipanda kwa miguu yangu ukiwemo huo wa Le Magurut

Nimezitembelea crater zote kuanzia Ngorongoro, Olmoti na Empakai.

Nimepanda mpaka kileleni mwa mlima pekee wenye volcano hai...Oldoinyo Lengai.

Nimetembelea na kufanya kazi katika ziwa pekee lenye mazalia ya flamingo Lake Natron.

Nimewatembelea mpaka machifu maarufu wa Ngorongoro akiwemo marehemu Birkaa na Ole Mereiya.

Utafiti gani zaidi nauhitaji #Lukubuzo ramsis!

Labda watafiti ndio wanitafute ili niwatafiti.
 
Ile semina aliyoagiza waziri mkuu kwa ajili ya wabunge,inawafaa wengine pia kama hawa
Mkuu
Unahitaji kueleweshwa kidogo kuhusiana na hili.

Hapa haiongelewi Ngorongoro ya Loliondo,huko ndio kuna mwarabu.

Bali inaongelewa tarafa ya Ngorongoro ambalo ni eneo linaloihusu Crater ya Ngorongoro na vijiji kadhaa vya kuizunguka hiyo crater.
 
Hata kule selou wapo waliopongeza na wapo wengi waliopinga huo mradi.
Watanzania ni wanafiki sana au tuna undumilakuwili kwenye mambo sensitive kwenye maisha yetu.

Wakati miti karibu milion 2 inakatwa selous national park kule tunakojenga mradi wa stiegler hakuna mtu aliepiga kelele na hata kutoa hoja za kwanini tusikate hiyo miti badala yake wengi sana walipongeza mradi bila kuangalia postive na negative effect.

Kwa mtazamo wangu, nadhani suala ni kuwaelimisha jamii husika iliyopo NCAA jinsi ya kuishi na wanyama pori na serikali ku-control namba ya watu na mifugo ili isizidi kiwango ambacho kinaweza kuleta athari kwa wanyamapori.
 
Kweli Ngorongoro inaangamia kwa kuendekeza siasa za kijinga, Tanzania tuna maeneo mengi ya mapori wanaweza kupelekwa huko kuishi lakini hatuna ngorongoro nyingine.
 
Usipotoshe umma,hapa hatuongelei suala la Loliondo!

Hapa tunaiongelea tarafa ya Ngorongoro pekee.

Wewe nadhani huielewi jiografia ya eneo husika zaidi ya kuchangia bila uelewa.

Pia hakuna mmasai alietishiwa kuangamizwa,zaidi ya kutakiwa kuhamishiwa na kupewa fidia katika maeneo mbalimbali ya nchi hii.

Je huko wanakopelekwa unataka kuniambia wananchi wa huko wanaangamia?

Je unazo taarifa kwamba zoezi la kuwahamisha lilikwisha anza kutekelezwa,na hivi tunavyoongea na kuandika.
Wale waliokwishahama leo hii wanaendelea na maisha yao kwa uhuru na hawatamani tena Ngorongoro.!
Mkuu asante kwa uchambuzi mzuri.
 
Hivi ukimpa mtu offer ya kumhamishia mahali ambapo maisha yake yatakuwa qualitatively better kuliko yalivyo pale alipo sasa atakaa kweli?

Sidhani kama Serikali imenadi mpango wowote wa maana kwa hii jamii ya Wamaasai.
Huu muda ambao wamasai wanaupoteza kwa kubishana na serikali nadhani wangetumia kujadili hayo maana mwisho wa siku watakaoathirika ni wao.
 
Mimi sihitaji kusoma tafiti ya mtu wakati binafsi nina miaka zaidi ya thelathini nikiwa katika eneo husika.

Hao watafiti huja kuandika kwa kuhoji watu kwa kipindi fulani na kuondoka lakini mimi ninielewa eneo hilo kuanzia Loduare mpaka Wasso kule Loliondo.

Ninaijua milima yote na nimeipanda kwa miguu yangu ukiwemo huo wa Le Magurut

Nimezitembelea crater zote kuanzia Ngorongoro, Olmoti na Empakai.

Nimepanda mpaka kileleni mwa mlima pekee wenye volcano hai...Oldoinyo Lengai.

Nimetembelea na kufanya kazi katika ziwa pekee lenye mazalia ya flamingo Lake Natron.

Nimewatembelea mpaka machifu maarufu wa Ngorongoro akiwemo marehemu Birkaa na Ole Mereiya.

Utafiti gani zaidi nauhitaji #Lukubuzo ramsis!

Labda watafiti ndio wanitafute ili niwatafiti.
Mimi nimekaa siku tatu pale , naafiki masai waondolewe kwa kuwa wanazaana sana uwezi kudhibiti hali hiyo. Ila Tanzania nayo ipunguze idadi ya vipori uchwala watu wapate maeneo ya kuishi na kufuga. Mfano mkoa wa shinyanga na tabora kuna vipori vingi vya hovyo.
 
Uko sahihi kabisa. Kwa mfano hawa wafugaji wa kimasaai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Wangepewa mojawapo ya hayo mapori ya akiba na waendelee kuishi na wanyama kama kawaida yao.
Ili kuiokoa ikolojia ya Ngorongoro.
 
Nakubaliana na wewe!
Tunachopaswa kufanya ni kuitaka serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinusuru eneo hilo na viumbe wake.
Lakini ihakikishe katika uendeshaji wa zoezi hilo,haki itendeke bila kufanya uonevu wala upendeleo kutoka kaya moja kwenda nyingine.

Kusitokee upotevu wa mali za wananchi.

Ili kubalance na kubakiza idadi ya wafugaji wanaoendana na uhifadhi kusudiwa.
Kusema wabaki baadhi itakuwa ngumu,maana baada ya miaka kadhaa watu na mifugo vitaongezeka Tena ....

Wewe unaijua vizuri ngorongoro je kwa nn serikali isiongeze radius kuzunguka mbuga? Hata kilometer kadhaa?
 
.... Ngorongoro imezalisha mabilioni ya fedha kwenye uchumi wa nchi; wamasai wakiwa sehemu ya vivutio vya utalii. Badala ya matumizi ya nguvu, serikali iwape motisha ili wahame kwa hiari. Kwa mfano, serikali ijenge flats maeneo fulani kama zile za JWTZ zilizojengwa maeneo mbalimbali nje ya miji then wahusika wahamishiwe huko. Mbona vijiji vya ujamaa enzi za Nyerere na Kawawa (Simba wa Vita) iliwezekana?

Atakayegoma kuhama huyo sasa atakuwa na jambo lake na haitakii mema nchi yetu hapo sasa nguvu inaweza kutumika. Ila kuwafukuza bila kuwaandalia makazi ni kuwaonea; ni unyanyasaji wala sio haki hata kidogo!
Kumbuka Masai hawaka Ghorofani. Ukitaka kuwauwa basi walazimishe kukaa ghorofani mori ukiwapanda mtawakuta wote chini.
 
Wanabodi JF!,

Nawasalimia popote pale mlipo!
Naomba niende kwenye Mada hii kuhusu NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY.(NCAA).

Nimefuatilia mijadala mbalimbali ambayo imekuwa ikiendelea kwenye social platforms,takriban muda wa wiki moja na ushei sasa.

Kuna wachangiaji ambao wamegawanyika katika pande mbili tofauti.

Upande mmoja ni wale wanaoitetea jamii ya wamaasai kuendelea kuishi wao pamoja na shughuli zao za ufugaji.

Pamoja na kuendelea kuongezeka ndani ya eneo la hifadhi hiyo kama ilivyo kwa sasa.

Kundi la pili ni wale ambao wanatetea uhifadhi maliasili ya wanyama pori na Ikolojia viumbe hai,vilivyo ndani ya eneo hilo muhimu na maarufu Duniani kwa utalii.

Mimi ninasimama upande wa watetezi wa Mazingira na Maliasili za wanyama pori na uoto wa asili,katika hifadhi ya Ngorongoro.

Ni ukweli usiopingika kwamba eneo hilo limekuwa likikaliwa na jamii ya kabila la kifugaji la wamaasai kwa asili.

Lakini inapokuja suala la uchumi wa kitaifa na pato la taifa kama nchi.
Eneo hilo na mengineyo mengi nchini yanayohusiana na utalii,yanabakia kuwa muhimu kwa upatikanaji wa fedha za kigeni.
Ambazo huingia na kuchangia maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na afya ya jamii.

Na hivyo kulifanya eneo hilo kutazamwa kwa maslahi mapana ya kitaifa na kimataifa.

Ikizihusu pia taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazojihusisha na utunzaji mazingira na viumbe hai Duniani.
Ikiwemo UNESCO.

Kuna kundi la watu wamechangia kwa kumshambulia Moja kwamoja #Maulidkitenge.
Kwa ile tu kunyoosha ukweli wake na kutoa maoni yake baada kile alichokishuhudia kule Ngorongoro.

Pia kuna waliochangia kwa kuwa wanatokana na jamii husika zinazokabiliwa na kadhia ya moja kwa moja ya kutakiwa kuhamishwa toka Ngorongoro hifadhini.

Lakini pia kuna wachangiaji ambao wameligeuza suala hili kuwa kama mtaji wao wa kisiasa zaidi.

Na hii niseme kuwa ni kwa maslahi binafsi ya wanasiasa hao.

Na hapa kuna wanasiasa wa pande zote mbili za kisiasa Toka upinzani na chama tawala CCM.

Mimi nachangia kama mtanzania ambaye nimefanyia kazi katika eneo hilo,kwa ukaribu na kwa muda mrefu sasa.

Nimeziona athari zinazoikumba hifadhi ya Ngorongoro katika kila hatua.

Kuongezeka kwa idadi ya wakazi na muingiliano wa shughuli za kiutalii.Ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa ujumla ni tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi au utatuzi wa mapema.kabla halijageuka na kuzaa mgogoro mkubwa baadae.
Endapo tu,halitachukuliwa maamuzi sahihi na kwa wakati stahiki.

Ebu tujiulize kwa kina!

Kama idadi ya wafugaji wa kimasaai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro inaongezeka kwa kasi.
Kama ilivyo kwa watanzania wote.

Je inakuwaje kuhusu upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii kama,Elimu, Zahanati na maji kwa matumizi ya binadamu na mifugo yao?

Katika eneo zima la Ngorongoro. Je kama wakipewa huduma zote na miji yao kutambulika kisheria...kutakuwa na kitu kinaitwa hifadhi ya Ngorongoro?

Ukizingatia kuwa jiografia ya eneo kubwa la Ngorongoro ni lenye kiwango cha chini cha mvua katika msimu wa mwaka mzima na hivyo suala la upatikanaji wa maji inakuwa moja ya changamoto kubwa kuwaathiri wakazi hao pamoja na mifugo yao.

Jambo linaloilazimu mamlaka ya hifadhi kuwasaidia ili kuwanusuru na maafa hayo.

Je, serikali inalo fungu la kuendelea kuwahudumia kwa muda woote,pamoja na idadi yao kuzidi kuongezeka kila uchao?

Je, watetezi wa wafugaji hao wanaelewa kwamba.

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na kupelekea kubadilika kwa mifumo ya maisha katika jamii nyingi.

Na jamii ya wamaasai wakiwa mojawapo ya wahanga wa mabadiliko hayo.
Kutokana na baadhi yao kupoteza kiasi kikubwa cha mifugo yao kutokana na maradhi au tabia nchi.

Imewalazimu pia kuanza kula vyakula ambavyo hapo awali havikukubalika kama chakula rasmi na ilikuwa ni marufuku kwao kuvila.
Ikiwemo Nyama Pori,Samaki na kuku.

Baada ya maisha kuwabadilikia na vijana wengi wa kimaasai kuingia mijini na kuchanganyika na jamii zingine katika jitihada za kutafutia maisha.

Leo hii wamekuwa walaji wakubwa wa vyakula vingi ambavyo hapo awali haikuwa kwenye orodha yao ikiwemo Chips Mayai nk.

Na ni katika mtindo huo,tabia hizi zinaambukizwa taratibu hadi huko kwenye asili zao.
Ngorongoro ikiwa muhanga mojawapo ya eneo husika.

Mifugo Tegemezi .

Tofauti na mifugo kama Ng'ombe,Punda,Mbuzi na kondoo inayofugwa na wamaasai hao wa Ngorongoro (na idadi yao pia ikiongezeka kwakasi).ambayo kiasili wanakula majani sambamba na wanyama wengine wa porini.

Kuna wanyama kama Mbwa ambao wafugaji wanawafuga na kuwategemea kama nyenzo muhimu kwa ulinzi wa mifugo yao,nyakati za usiku dhidi ya wanyama pori walao nyama kama Simba,Chui na Fisi.

Je! wao hao mbwa ambao kila kaya,lazima inawamiliki kwa idadi ya wastani usiopungua mbwa watano kila kaya.

Je, Wanakula nini kila siku ilhali chakula cha maasai wa asili ni mchanganyiko wa maziwa na mahindi almaarufu kama Roshoroo.?
Ambacho si chakula kinacholiwa na hao mbwa wa asili ya wamaasai.

Ikumbukwe kuwa nyama ya mbuzi ambayo huchinjwa na maasai hao mara chache katika maboma yao,huwa ni kidogo kuliko mahitaji rasmi ya kutosheleza jamii husika wakiwemo watoto wadogo.

Jambo ambalo hupelekea mgawanyo usio sawia kati ya wanaume
(Morani na wazee) na upande wa wanawake (kina mama,vikongwe na watoto wadogo).

Hapo humlazimu mbwa kujitafutia riziki zao na watoto wao.
Kwa mbinu asilia za kuwinda wanyama pori kama vile Sungura,Swala, watoto wa nyumbu na punda.

Na saa ingine hadi watoto wachanga wa Twiga.
Tukio ambalo mimi binafsi, niliwahi kulishuhudia na kulitolea taarifa pale Seneto gate kwa maaskari wa Ngorongoro.

Je, Hatujiulizi kwamba kuna idadi ngapi? au kiasi gani cha wanyamapori kinapotea kila mwaka kwa kuliwa na idadi kubwa ya mbwa wanaomilikiwa na wamaasai.?

Wakati tukiwatetea wamasai wa Ngorongoro,pia vema tuelewe kwamba,wao wanaishi pale ndiyo.
Lakini Ngorongoro inabeba maisha ya watanzania wengi kutokana na pato linaloingizwa kupitia sekta pekee ya utalii.

Na hivyo tunapotetea haki ya wamaasai wakaazi wa Ngorongoro kutohamishwa.

Pia ni vema tukumbuke na madhara yanayoweza kupatikana endapo jamii hiyo itaachwa kuzagaa na kuongezeka bila udhibiti sahihi kwa manufaa ya wengi nchini.

Na kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Hapo sijaongelea kero zinazowasibu wakazi hao kwa uduni wa maisha kutokana na kutoruhusiwa kulima mazao ya chakula kisheria.

Na hivyo kupelekea baadhi ya familia zinazoishi pembezoni mwa shughuli za kitalii,kugeuka omba omba mabarabarani jambo linaloiwekea Tanzania taswira mbaya kimataifa.

Pindi watalii hao wanaporudi makwao na kusimulia walichokiona ikiwemo pamoja na picha za video na mgando.

Tuacheni siasa na malumbano yasiyo na tija.

Watanzania tubadilike linapokuja suala la ukweli na tuache tabia ya kutanguliza maslahi binafsi mbele.

Maendeleo hayana chama.
Hivi vinavyoangamia Tanzania ni Ngorongoro tu? Deni la Taifa mbona pia linatuangamiza.
 
Nakubaliana na wewe!
Tunachopaswa kufanya ni kuitaka serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinusuru eneo hilo na viumbe wake.
Lakini ihakikishe katika uendeshaji wa zoezi hilo,haki itendeke bila kufanya uonevu wala upendeleo kutoka kaya moja kwenda nyingine.

Kusitokee upotevu wa mali za wananchi.

Ili kubalance na kubakiza idadi ya wafugaji wanaoendana na uhifadhi kusudiwa.
Voicer, kwanza nikiri hapa kuwa wewe ni 'voice of reason' hapa JF katika mjadala huu. Na wewe ni ama Mkazi wa Ngorongoro au unao ukaribu mkubwa na Ngorongoro.

Nimefuatilia yaliyozungumzwa Bungeni nikafahanu kuwa idadi kubwa ya Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliopo Ngorongoro wanamilikiwa na watu walio nje ya Ngorongoro.

Mifugo mingi ni mali ya Watu wenye Landcruiser VX wanaolala katika Nyumba za Maghorofa nje ya Hifadhi.
Wafugaji ndani ya Hifadhi wanamiliki Ng'ombe, Mbuzi, na Kondoo wachache sana.

Wingi wa Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliotoka nje ya Hifadhi ndicho kiini cha mgogoro huu.
Mamlaka ya Ngorongoro ni Watuhumiwa namba moja katika tuhuma hii.

Wameshiriki kuingiza mifugo toka nje ya Hifadhi kwa ama kulifumbia macho jambo hili, au kushiriki moja kwa moja.
Watuhumiwa namba 2 ni NGO zilizojaa Hifadhini ambazo zinaogopa kuwataja Wamiliki wa mifugo wakati wanawajua. Inawezekana Wamiliki wa hizo NGO na wao wameshiriki kuingiza mifugo yao ndani ya Hifadhi.

Watuhumiwa namba 3 ni Wafugaji wenyewe wa Kimasai waliokubali kutumiwa kuchunga mifugo ambayo siyo mali yao.
Inawezekana walipaza sauti zao lakini zikamezwa na Viongozi wa NGO na Mamlaka ya Ngorongoro ambao wanashirikiana kuiua Ngorongoro kwa kinachoonekana kuwa masilahi binafsi.
Tupe mwanga kuhusu hili tafadhali.
 
Kusema wabaki baadhi itakuwa ngumu,maana baada ya miaka kadhaa watu na mifugo vitaongezeka Tena ....

Wewe unaijua vizuri ngorongoro je kwa nn serikali isiongeze radius kuzunguka mbuga? Hata kilometer kadhaa?
Mkuu!

Tatizo kubwa hapa ni kwamba hata kama radius itaongezwa bado source kuu ya maji na malisho iko huku juu Ngorongoro Highlands.

Na hiki ndio kiini cha mgogoro,maana kila inapofika majira ya kiangazi,ukame unawalazimisha wafugaji kuileta na kuiingiza mifugo yao ndani msitu kwa malisho.kinyume na sheria.

Kwa hiyo eneo la square km 8200.
Sio dogo kwao.

Ila eneo lenye neema ni kama 30% ya eneo lote latarafa hiyo ya Ngorongoro.Na kila kundi lina uhitaji wa eneo hili.

Na ugomvi unaanzia hapo.
 
Voicer, kwanza nikiri hapa kuwa wewe ni 'voice of reason' hapa JF katika mjadala huu. Na wewe ni ama Mkazi wa Ngorongoro au unao ukaribu mkubwa na Ngorongoro.

Nimefuatilia yaliyozungumzwa Bungeni nikafahanu kuwa idadi kubwa ya Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliopo Ngorongoro wanamilikiwa na watu walio nje ya Ngorongoro.

Mifugo mingi ni mali ya Watu wenye Landcruiser VX wanaolala katika Nyumba za Maghorofa nje ya Hifadhi.
Wafugaji ndani ya Hifadhi wanamiliki Ng'ombe, Mbuzi, na Kondoo wachache sana.

Wingi wa Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo waliotoka nje ya Hifadhi ndicho kiini cha mgogoro huu.
Mamlaka ya Ngorongoro ni Watuhumiwa namba moja katika tuhuma hii.

Wameshiriki kuingiza mifugo toka nje ya Hifadhi kwa ama kulifumbia macho jambo hili, au kushiriki moja kwa moja.
Watuhumiwa namba 2 ni NGO zilizojaa Hifadhini ambazo zinaogopa kuwataja Wamiliki wa mifugo wakati wanawajua. Inawezekana Wamiliki wa hizo NGO na wao wameshiriki kuingiza mifugo yao ndani ya Hifadhi.

Watuhumiwa namba 3 ni Wafugaji wenyewe wa Kimasai waliokubali kutumiwa kuchunga mifugo ambayo siyo mali yao.
Inawezekana walipaza sauti zao lakini zikamezwa na Viongozi wa NGO na Mamlaka ya Ngorongoro ambao wanashirikiana kuiua Ngorongoro kwa kinachoonekana kuwa masilahi binafsi.
Tupe mwanga kuhusu hili tafadhali.
fundimchundo!

Umeongea mambo mengi kuihusu Ngorongoro kwa ujumla wake.
Ila nitofautishe hapa.....

Kuna migogoro miwili ya ardhi katika wilaya ya Ngorongoro.Nayo ni kama ifuatavyo.

Kuna mgogoro wa ardhi unaoihusu tarafa ya Ngorongoro yenye ukubwa wa Square kilometres 8200.

Ambapo wafugaji wanatakiwa kuhamishwa ili kupunguza idadi ya shughuli za kibinadamu na ongezeko kubwa la idadi ya mifugo.
Hali
inayotishia uwepo wa uhifadhi mseto baina ya Binadamu na mifugo yao,pamoja na wanyama pori asilia na ikolojia ya mimea.

Kuna mgogoro wa ardhi unaoihusu tarafa ya Loliondo yenye ukubwa wa square kilometres 1500.
Ambapo shughuli za makazi ya binadamu na mifugo yao inatakiwa kukoma.

Ili kuweza kubadili matumizi ya eneo hilo kuwa pori tengefu au Game reserved area.

Hapa tunajadili eneo moja kati ya hayo mawili.
Ambalo ni tarafa ya Ngorongoero.

Kuhusu umiliki wa mifugo kwa watu wasioishi ndani ya hifadhi au eneo la Ngorongoro,ni jambo lenye utata.

Sababu ni ukweli usiopingika kwamba,maisha ya kaya nyingi unazozikuta na idadi kubwa ya mifugo.
Bado haireflect maisha unayowakuta nayo kwenye maboma hayo.

Mimi binafsi sijalifanyia kazi suala hilo kwa sababu liko mbali tofauti na majukumu yangu ya kikazi yanayoniwezesha kufikia maeneo hayo.

Nimewahi kuona mfumo huu katika nchi ya Rwanda.

Kwamba!

Kuna eneo linaitwa #Kayonza.eneo hilo maarufu nchini #Rwanda.sababu ndiko mji wa nyumbani alikozaliwa rais #Kagame wa nchi hiyo.Kayonza pia inapakana na hifadhi maarufu ya wanyama nchini humo ya #Akagera National Park.

Lakini hapa nimelitaja kwa sababu niliona tukio linalofanana na hili la Ngorongoro.

Kuna idadi kubwa sana tena kupindukia ya mifugo inayotunzwa hapo ili kufaidi malisho katika bonde la Akagera. (Kagera).

Na ukiulizia wamiliki wa Ng'ombe wale utapewa jibu kwamba baadhi ni wa familia za mawaziri pamoja na matajiri walioko #Kigali.

Hivyo sintanshangaa mtindo huo kuwezekana ndani ya Ngorongoro.
 
Wewe ni mjinga kama Kitenge. Toka lini Ngorongoro inapata mvua kidogo mwaka mzima? Ngorongoro ni ukanda wa juu unaopata mvua sawia kila mwaka. Tena mvua nyingi kuliko sehemu nyingi nchini.

Hatua ya kwanza iwe ya kuivunja hiyo NCAA mnayoitumia kujitajirisha kwa kufisadi na kujilipa posho kubwa kubwa.
Eneo likabidhiwa kwa TANAPA ili iwe national park. Utalii wa utamaduni umekwisha. Eneo la NCA liwe mbuga ya Taifa chini ya Tanapa kama ilivyo Serengeti, Tarangire au lake Manyara.
Utalii wa utamaduni kwa namna unavofanyika sasa NCA ni greenwashing ya nguvu.
Watu wanaigiza maisha ya Maasai pale "Kanjiro" (staged cultural experience).
Kingine utitiri wa lodge na camps unaathiri biashara ya utalii!
 
Back
Top Bottom