Ngorongoro: Fahamu maisha ya Faru Fausta; chakula na gharama za maisha yake

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kulima majani aina ya lusini ambayo ni chakula cha Faru
Fausta ili kupunguza gharama za kumtunza mnyama huyo.


Faru Fausta mwenye miaka 54 anahifadhiwa kwenye banda ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni hatua ya kumlinda asiliwe na wanyama wengine kutokana na jicho lake kutoona.


Amekuwa akitumia bandali 250 za majani kila baada ya miezi minne yanayoigharimu mamlaka hiyo Sh5 milioni. Majani hayo hununuliwa kutoka nchi jirani ya Kenya.


Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Idara ya Malisho na Usimamizi wa Wanyama NCAA, Hillary Mushi amesema mamlaka imeandaa shamba lenye ukubwa wa eka mbili na imepanda mbege za lusini. Amesema ndani ya miezi saba majani hayo yataanza kuvunwa.

pic%2Bfausta.jpg

Mushi amesema NCAA imechukua hatua hiyo ili kupunguza gharama za kumtunza faru huyo , ambaye amekuwa moja ya kivutio cha watalii na watafiti kutokana na kuwa ndiye faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani kati ya wanaoishi maeneo ya wazi hifadhini.
 
Rip Faru John umeondoka na kichwa cha Prof Magembe yuko bench now tunasubiri Faru Abdallah aondoke na Kigwa
 
Back
Top Bottom