Ngono mpaka aolewe?

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Jan 31, 2009
7,333
3,896
Ni haki kwa wasichana wasifanye ngono mpaka waolewe? Ndoa ngapi zinafungwa siku hizi? Je kuna uhakika kila msichana atapata wa kumuoa kabla hajafikia utu uzima? Naomba warasimu wanijibu.
 
Ni haki kwa wasichana wasifanye ngono mpaka waolewe? Ndoa ngapi zinafungwa siku hizi? Je kuna uhakika kila msichana atapata wa kumuoa kabla hajafikia utu uzima? Naomba warasimu wanijibu.
Ni haki na ni wajibu wajitunze, wasifanye ngono mpaka watakapoolewa kwani tendo hilo lina heshima yake na miiko inayolizunguka. Mwenyezi Mungu alitaka lifanywe na watu wa ndoa TU.Ndiyo kwa heshima linaitwa Tendo la Ndoa. Likifanywa nje ya ndoa linapata majina mengine kuonesha kwamba si mahali pake. Ndo mana utasikia: uzinzi, uzinifu, uasherati, nk.
Msichana akijitunza, akajithamini akaacha kupaparika atapata mchumba na kufunga ndoa safi. Na msichana anayejitunza jamii inamwona, na wanaume/ wavulana wanamwona.
Isitoshe wasichana wengi wanakuwa masomoni bado. Wamalize kwanza masomo. Wasichanganye masomo na ngono. Watashindwa mitihani.
 
Ni haki kwa wasichana wasifanye ngono mpaka waolewe? Ndoa ngapi zinafungwa siku hizi? Je kuna uhakika kila msichana atapata wa kumuoa kabla hajafikia utu uzima? Naomba warasimu wanijibu.

Na kwa nini ni wasichana tu?? Wanaume Je?

Wewe unayeuliza kama ni mwanaume, SWALI;

  1. umetenda tendo hilo (nje ya ndoa) na wanawali wangapi mpaka sasa?
  2. hao uliotenda nao wapo wapi?
  3. kwa nini unataka mwanamwali ambaye hajaingiliwa na hali wewe ushawaingilia wengi na hujawaoa???
Ukiwa mlafi usiwe mchoyo!!

Wewe ukiishi kwa maadili, utabajaliwa mwenye maadili na nyumba yako itakuwa na furaha, lakini endapo umechezea tu wabinti za watu na kuwaacha basi nawe utachezewa tu. Kama si wewe basi kizazi chako.

Hivyo panda mbegu njema ili uvune chema.
 
Ni haki kwa wote wawili msichana na mvulana, no sex till marriage.
 
No sex untill marriage is a good concept lakini ukweli ni kwamba watu wanao subiria mpaka ndoa ni wachache sana. Na ukiacha hiyo ya kusubiri mpaka ndoa ni wachache sana ambao mume/mke wake anakua the first and only person to have sex with. Hili swala ukiuliza mbele ya umati kama huu kila mmoja kuonekana "mwema" atakupa majibu mazuri sana mpaka uone jamii yetu takatifu lakini unakuta watu wanafanya the exact opposite. Watu wanatoa majibu ya "kisiasa".
 
Aghalabu si rahisi sana kupata bikra kwa wote wawili (mvulana na msichana). Tujaribu kuwa wakweli! ni nani hadi sasa kwa umri wa miaka 18 ambaye bado hajafanya ngono?
Achilia mbali siku hizi watoto wadogo kabisa wanajua ngono ni nini na inafanywaje.
Kimsingi ingependeza sana kama wote tungevumilia hadi kuoa/kuolewa, lakini pia si rahisi kijana wa sasa anunue mbuzi kwenye gunia. Hivi kweli wewe utakubali uolewe (kwa akina dada) na mtu ambaye hujui mziki wake ukoje? Kama jogoo hapandi mtungi si kesho yake tu mnaachana? Hali kadhalika kwa waoaji kweli utaletewa tu mamaa ndo huyu mara unaingia ndani kuna katundu ka mkojo tu kale ka shughuli hakapo!
Wengi walikuwa wanafanya hivyo zamani lakini si sasa, na kama wapo basi kuna sababu nzito sana zinawafanya wasifanye hivyo.
Mojawapo ya uhamasishaji wa kuolewa ni ngono kwa upendaye. Na manjonjo kama alivyowahi kusema kwenye thread moja MJ1,,,Wanawake wanaolia,,,,,,,,,,,,,,,,.
 
Back
Top Bottom