Ngono, Maadili, Rushwa, Haki na Polisi (Magomeni) Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngono, Maadili, Rushwa, Haki na Polisi (Magomeni) Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sophist, May 21, 2011.

 1. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Ndugu Waandishi wa habari na Wanaharakati.

  Pole na shughuli.

  Naleta kwenu malalamiko yetu, ili mtusaidie kufuatilia.

  Tuna mtoto wetu aitwae Solome Mahamud, anasoma Arusha. Mtoto huyo alikuja kututembelea hapa Dar Es salaam na alipofika hapa, Bwana Mickson Wallace Ndamugoba, ambaye ni shemeji yetu anayemuoa mamake mdogo wa huyo mtoto, Dada Lucy, akamtongoza na wakawa wanaenda kukutana kimapenzi kwenye guest house huko magomeni. baada ya kupata taarifa hizi, tuliripoti KITUO CHA POLISI MAGOMENI, na mtego ukapangwa na hatimaye akakamatwa tendoni. Hiyo ni wiki nne sasa.
  Alipelekwa kituoni Kufunguliwa jarada, lakini cha kushangaza ni wiki nne sasa hajapelekwa mahakamani, zaidi ya mkuu wa kituo kutushauri tuyamalize nje ya mahakama. Sisi tumekataa, lakini mkuu huyo amegoma kupeleka shauri hilo mahakani; tunajiuliza, je kituo cha polisi kimegeuka sehemu ya kunyanyasa wasiyo kuwa na uwezo kifedha?
  Imefikia hata ndugu wa huyo Mickson kutwambia kuwa hatuwezi kumfanya lolote. Je wenye uwezo watakuwa wanatembea na watoto wa shule au kufanya makosa, kwakujua kuwa wakipelekwa vituo vya polisi, watawaonga polisi na kuzima kesi hizo palepale vituoni? Tunaomba msaada wenu jamani.

  Mtuhumiwa anafanya kazi Amazon Pharmacy, iliyopo mtaa Lumumba kariakoo, namba zake za simu ya mkononi ni 0754880969 na 0716024238. Mkewake anapatikana kwenye ofisi za Mr. Clean, tawi la namanga ( kampuni inashughulika na ufuaji wa nguo), na namba ya simu yake ni 0713238433.

  Tuaomba msaada wenu kufuatilia suala hili.

  Tunatanguliza shukrani zetu kwa msaada tutakaoupata toka kwenu.


  Wasalaam.

  EDWIN MASSAWE
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  MZee Pole kwa yaliyokukuta, Lakini labda ufikiri upya juu wa aina hii ya kesi na ujiulize utawapeleka wangapi Mahakamani kabla huyo mtoto hajaolewa kwa sababu inaonekana hakubakwa na mda mwingi yuko Arusha sijui una hakika gani kuwa huko Arusha hafanyi mambo ya namna hiyo. Angalia mtoto asije akakuruka Mahakamani na ukaachwa kwenye mataa kiajabu kabisa.
  Nadhani huyo Askari anayekushauri hayo anaona mbali sana na unayo kazi ya kum-groom huyo mtoto ili ajenge tabia nzuri but hata ukienda mahakani ukashinda kesi je ndo mwisho wa huyo mtoto kufanya mapenzi?? Think twice man even though it huts
   
 3. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kukubwa hapa hujaeleza umri wa mtoto. Kwani kama yupo chini ya miaka 18 ni titizo lakini kama sio basi acha wale bata
   
 4. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapohujampa ushauri wa maaa uo ni uhuni umetoa,cha msini waone vituo vya wanasheria waeleze kesi yako for the way forward
   
 5. C

  Chamkoroma Senior Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kweli duniani tunayodhiki lakini tujipe moyo tutashinda kama Yesu alivyoshinda, jambo hili linaumiza kichwa kwasababu huyu mtoto hasomi hapa ila Arusha, japo hatujaambiwa umri wake lkn sidhani amebakwa kwasababu ya umri chini ya 18, naamini kabisa ni katabia alichoweka akilini mwake, naamini aempenda baba huyu, inawezekana kabisa baba huyu amemuanza au yeye amesababisha huyu baba amtongoze, kuna rafiki yangu aliisimlia kisa cha mtoto chini ya miaka 7 aliyekuwa akionyesha tabia yakumtekenya na kumkanyaga kila walipofika kuwasalimia hapo kwao, akaniambia kuwa mtoto huyo alikuwa akimkanyaga, nakumpapasa kwani jamaa alikuwa anenda kushonesha nguo kwamama ya mtoto, nakajiuliza ameona wapi na anajua nini maana ya jambo hili?
  kwahiyo inawezekana kabisa polisi ameona kupitia maelezo a mtoto.
  NAWASHAURI MSHIRIKIANE SI KUKOMOANA JAPO KUMETOKEA MATAIZO.
   
 6. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh watu hapa mnaona km vile kitendo hiki ni cha kawaida sn. Awe alishabakwa au ndo mara ya kwanza tendo la ubakaji halina justification km umri wake ni mdogo. Pia kwa maelezo hayo yaelekea ni mtoto ninahakika wazazi wa mtoto huyo si wajinga kupeleka polisi na polisi kushauri wakayamalize.
  Taarifa ya juzi ya PCCB inaonyesha polisi kuna matatizo makubwa sn. Tuwaokoe watoto hawa, tunajukumu la kuwasaidia. Hakuna justification ya kungonoka na mtoto eti kwa kisingiZio amekutungoza. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Badala ya kumuonyesha njia na wewe unaenda kuvua nguo kabisa. Hivi huoni aibu kuchunguliwa na katoto? Hebu wote wenye tabia hizi wakome.
   
 7. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Kisheria mwanafunzi wa shule ni minor, hakuna cha alinitongoza mwenyewe wala tulikubaliana. Ukitembea na mwanafunzi wa shule unakuwa umebaka, adhabu yake ni jela miaka 30 bila msamaha.
   
 8. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwakweli hicho kitendo alichokifanya Bwana Mackson si kizuri ukizingatia tayari ana mke, ila sasa inawezekana mlipompeleka kituo cha polisi hamkuelezea kesi yake ya msingi ni hipi:-
  Ni ubakaji, kufanya mapenzi na mwanafamilia au mtoto!!!!! Ukikosea kuelezea kesi ya msingi na upelelezi ukafanyika Polisi hawezi kupeleka kesi mahakamani bila kujilizisha, Hivyo basi kwa busara zaidi na kwa vile inaonekana walikubaliana kufanya kitendo hicho, Kaeni kama wanafamilia muangalie nini cha kufanya ili kunusuru maisha ya pande zote mbili; kumbuka Mackson anafamilia(mke na wototo) sasa akipigwa miaka 30 jera huyo Mke na watoto itakuaje?
   
 9. Tyta

  Tyta JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 12,846
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa maana ya kumuuchisha kiasi cha kutaja mpaka no. Zake na za mkewe...ila ushauri wangu kama binti ni under 18,tafuta msaada wa kisheria(attorney)...hivi hivi itakula kwako
   
 10. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Lakini huyo mtoto anasemaje? si yalishatukuta kwa mtoto wa dada yangu alikuwa ansoma form three with 16 yrs kipindi hicho, kweli kesi ilienda mahakamani ila huyo mtoto alichotufanya huko aibu tupu mara aseme sio kweli mara aongee maneno hayaeleweki mara akatae myaani mchanganyiko maalumu hadi kesi ilifutwa watoto wa siku hizi bwanaa acha tu
   
 11. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Ulitaka akaeleze kesi gani polisi? Kwani yeye ni mtaalamu wa sheria. Mbona ameeleza wazi kuwa mtego wa kumnasa mtuhumiwa ulipangwa na polisi? Wacheni kumdhihaki. Mwanafunzi analindwa na sheria. Kwa hiyo kwa vile jamaa ana mke na watoto ni ruksa kuvuruga watoto wa wasiojua wakifanyacho? Mbona hii forum inaanza kupotea mwelekeo?

  Ok. Mimi si mwanasheria, lakini hapa naona kuna tatizo la rushwa. Si jukumu la polisi kuamua kesi. Hivyo ushauri wangu nenda mapeema kwenye vituo vya wanasheria wa haki za binadamu. Hao watakupa ushauri mzuri na hata kuwashughulikia hao polisi. Naamini haki itatendeka. Ukishindwa hilo tinga kwenye vyombo vya habari upaaze sauti uone kivumbi chake.
   
Loading...