Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Ngome ya vijana Act-Wazalendo tumeendelea kuchukua hatua kadhaa wa kadhaa juu ya changamoto iliyopo katika marejesho ya mikopo elimu ya juu pamoja na sheria yake kuhusu viwango na masharti ya marejesho ya mikopo ya elimu ya juu.
Kama ambavyo mwenyekiti wa Vijana taifa Ndg Abdul Nondo alizungumza na vyombo vya habari kuhusu hili tarehe 14 /Januari/2021, akisema Ngome tumeazimia kuandika barua kwenda katika mamlaka za serikali ili serikali kuchukua hatua stahili.
Mnamo tarehe 20 Januari 202. Katibu wa Ngome ya vijana act wazalendo Ndg Mwanaisha Mndeme aliandika barua kwenda wizara ya Elimu-Dodoma yenye kichwa cha barua,
Serikali kufanya marejeo na tathimini mpya juu ya viwango na masharti ya marejesho ya mikopo elimu ya juu kupitia bodi ya mikopo na sheria yake
Nakala za barua hii zilipelekwa pia Ofisi ya Rais-Ikulu(kupitia Katibu mkuu kiongozi),Ofisi ya Waziri mkuu na Bodi ya mikopo elimu ya juu.Barua hizo zilipelekwa na viongozi wa Ngome ya vijana Petro Ndolezi Amir Khamis na Julius Massabo.
Mbali na barua hizo kupelekwa ofisini ,Ngome ya vijana ilizituma pia barua hizo kupitia email yake actwazalendovijana@gmail.com kwenda katika ofisi zote na kupokelewa.
Hizi ni hatua za awali tuu Ngome ya vijana tunafanya.Ikiwa hakuna hatua zozote zitakazo chukuliwa na serikali bado kuna njia ya ziada tutaifanya ya kufungua kesi mahakama kuu dhidi ya sheria ya bodi ya mikopo kuvunja mkataba wa msingi (Student's Loan Agreement) kati ya muombaji (Mwanafunzi) na Bodi ya mikopo kwa kushirikiana na wadau ,Azaki na wahanga wa sheria hii.
Tunaendelea kupongeza Azaki mbalimbali ikiwemo kituo cha sheria na haki za binadamu, Wanaharakiti ,wahanga na wanafunzi kwa pamoja wanavyoendelea kupaza sauti kwa pamoja dhidi ya sheria hii .
Ngome ya vijana Act wazalendo tutaendelea kupigania,maslahi ya msingi ya vijana na jamii kwa ujumla dhidi ya uonevu na hata kupokonywa haki.
Imetolewa Na
Idara Ya Habari Uenezi na Mawasiliano kwa Umma
Ngome ya Vijana Taifa.
22/01/2021.