M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Fatuma umesahau.... kuna kipindi (uchaguzi nadhani wa 2000) ngome ilikuwa CUF ya Lipumba!Katika hili ni lazima niwapongeze wanakaskazini kwa sababu wanajitambua tofauti na wanakusini.
Wengi waliamini baada ya Chadema kuishiwa " mipango " basi ACT wazalendo watakuwa chama kikuu cha upinzani, hata mimi awali niliamini hivyo kumbe siyo.
Ngome ya upinzani ni Kaskazini ndio maana wabunge wa Chadema mh Komu na Selasini wameaga kabisa kuwa wamehamia Nccr mageuzi na hawajachukuliwa hatua zozote.
Jana wabunge Silinde na Lijualikali wamehudhuria bungeni Chadema wanataka kuitisha kamati kuu kuwajadili kwanini wamekiuka maagizo ya chama ilhali inajulikana wazi mbunge anawakilisha wananchi wote bila kujali itikadi.
Selasini alikuwemo bungeni na ameiponda sana Chadema lakini hawamgusi.
Maendeleo hayana vyama!