Uchaguzi 2020 Ngome kuu za CCM (Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa) walizokuwa wakizitegemea zimetikiswa

Sio kweli Watu watatu ndio walikuwa mhimili wa hiyo kanda Lowasa, Slaa na Ndesamburo mtakiona cha mtema kuni tarehe 28 October

Dar es salaam wana Dar wameshawashia Taa za hazard na ving'ora kuwa chadema hamna chenu Dar

Uzinduzi wenu mliona ulivyodorora Dar hadi aibu
Dar bado haijaeleweka Nani anaekubalika
 
Kampeni za cdm zamani walikuwa wanapeleka chopa.Kwa sasa sana uhakika watu wanaenda kuangalia MTU kwenye vyuma mwilini.
Hakika wala hujakosea.
Screenshot_2020-09-28-15-31-51-1.jpg
 
Kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa 2015 CCM ilipata kura 8,882,935 za urais, karibu nusu ya kura zote zilitoka kanda ya Ziwa na kanda ya Kati.

CCM ilipata kura 3,638,623 kutoka mikoa 9 tu ya Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga, huku CHADEMA ikiambulia kura 1,724,569 kwenye kanda hizo kati ya kura 6,072,848 za urais walizopata 2015.

Pamoja na kuwa ngome kuu za CCM, lkn mwaka huu hadi sasa kupitia kampeni zake, CHADEMA imeonekana kufanya vizuri kwenye mikoa hiyo, huku ikiwa bado na uhakika wa kupata kura zaidi kwenye ngome zake za mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha, na Manyara) na Mikoa ya nyanda ya juu Kusini (Mbeya, na Iringa).

Hadi sasa kimikakati bado CHADEMA inaongoza kwa kushambulia ngome za mpinzani wao wa karibu CCM kwa muda mrefu, nafikiri ‘strategist’ wao aliwashauri vizuri.

Nyanda zingine za Mashariki (DSM, Pwani, Morogoro na Tanga), Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara), Kanda ya Magharibi (Kigoma, Katavi) na Zanzibar ni kanda ambazo kura zake bado zimegawanyika kwa vyama vyote vikuu yaani CCM, CHADEMA na ACT.

Hii ni tathimini yangu kwa mikakati inayoonekana wazi ya awamu ya kwanza ya kampeni iliyofikisha mwezi mmoja tangu kuzinduliwa trh 26/8. Matarajio mabadiliko machache kutokea tunapokaribia siku ya uchaguzi.
Porojo tupu. Katafute malimao kabisaaa, Magufuli JP ndio rais wako.
 
Kaskazini kwa sasa hawana Chao ilikuwa ngome ya Slaa,Lowasa na Ndesamburo ambao wote kwa sasa hawapo .Ndesamburo mwamba wa Kilimanjaro alifariki Lowasa na Slaa na makundi yao walisharudi CCM

Mbeya na Iringa unaongelea mbeya mjini na iringa mjini tu wilaya zingine hamna kitu
Wenzako wanapiga honi ya Treni kama vuvuzela Arusha....NI YEYE LEMA
 
Dodoma,
CCM (516,317); CHADEMA (157,623).
Singida,
CCM (290,899); CHADEMA (112,342).
Tabora,
CCM (413,492); CHADEMA (181,213).
Mwanza,
CCM (584,184); CHADEMA (311,532).
Kagera,
CCM (475,910); CHADEMA (287,538).
Geita,
CCM (377,051); CHADEMA (157,440).
Simiyu,
CCM (318,358); CHADEMA (163,319).
Mara,
CCM (335,476); CHADEMA (221,382).
Shinyanga,
CCM (326,936); CHADEMA (132,180).
Mapishi
 
Sio kweli Watu watatu ndio walikuwa mhimili wa hiyo kanda Lowasa, Slaa na Ndesamburo mtakiona cha mtema kuni tarehe 28 October

Dar es salaam wana Dar wameshawashia Taa za hazard na ving'ora kuwa chadema hamna chenu Dar

Uzinduzi wenu mliona ulivyodorora Dar hadi aibu
Subiri next round hiyo dar utanambia halafu mwaka huu lissu afungie kampeni dar tena!
 
Kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa 2015 CCM ilipata kura 8,882,935 za urais, karibu nusu ya kura zote zilitoka kanda ya Ziwa na kanda ya Kati.

CCM ilipata kura 3,638,623 kutoka mikoa 9 tu ya Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga, huku CHADEMA ikiambulia kura 1,724,569 kwenye kanda hizo kati ya kura 6,072,848 za urais walizopata 2015.

Pamoja na kuwa ngome kuu za CCM, lkn mwaka huu hadi sasa kupitia kampeni zake, CHADEMA imeonekana kufanya vizuri kwenye mikoa hiyo, huku ikiwa bado na uhakika wa kupata kura zaidi kwenye ngome zake za mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha, na Manyara) na Mikoa ya nyanda ya juu Kusini (Mbeya, na Iringa).

Hadi sasa kimikakati bado CHADEMA inaongoza kwa kushambulia ngome za mpinzani wao wa karibu CCM kwa muda mrefu, nafikiri ‘strategist’ wao aliwashauri vizuri.

Nyanda zingine za Mashariki (DSM, Pwani, Morogoro na Tanga), Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara), Kanda ya Magharibi (Kigoma, Katavi) na Zanzibar ni kanda ambazo kura zake bado zimegawanyika kwa vyama vyote vikuu yaani CCM, CHADEMA na ACT.

Hii ni tathimini yangu kwa mikakati inayoonekana wazi ya awamu ya kwanza ya kampeni iliyofikisha mwezi mmoja tangu kuzinduliwa trh 26/8. Matarajio mabadiliko machache kutokea tunapokaribia siku ya uchaguzi.
Porojo tu hizo.
 
Porojo tupu. Katafute malimao kabisaaa, Magufuli JP ndio rais wako.
Safari hii wizi hauta kuwepo kwani watu wamejipanga Hadi kufungua saver ya mtambo utakao tumika kurushia matokeo ili kubaini matokeo yanayo tangazwa na tume na Yale yaliyo halisi yaliyopigwa.
Wizi sasa Basi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom