Kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa 2015 CCM ilipata kura 8,882,935 za urais, karibu nusu ya kura zote zilitoka kanda ya Ziwa na kanda ya Kati.
CCM ilipata kura 3,638,623 kutoka mikoa 9 tu ya Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga, huku CHADEMA ikiambulia kura 1,724,569 kwenye kanda hizo kati ya kura 6,072,848 za urais walizopata 2015.
Pamoja na kuwa ngome kuu za CCM, lkn mwaka huu hadi sasa kupitia kampeni zake, CHADEMA imeonekana kufanya vizuri kwenye mikoa hiyo, huku ikiwa bado na uhakika wa kupata kura zaidi kwenye ngome zake za mikoa ya Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro, Arusha, na Manyara) na Mikoa ya nyanda ya juu Kusini (Mbeya, na Iringa).
Hadi sasa kimikakati bado CHADEMA inaongoza kwa kushambulia ngome za mpinzani wao wa karibu CCM kwa muda mrefu, nafikiri ‘strategist’ wao aliwashauri vizuri.
Nyanda zingine za Mashariki (DSM, Pwani, Morogoro na Tanga), Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara), Kanda ya Magharibi (Kigoma, Katavi) na Zanzibar ni kanda ambazo kura zake bado zimegawanyika kwa vyama vyote vikuu yaani CCM, CHADEMA na ACT.
Hii ni tathimini yangu kwa mikakati inayoonekana wazi ya awamu ya kwanza ya kampeni iliyofikisha mwezi mmoja tangu kuzinduliwa trh 26/8. Matarajio mabadiliko machache kutokea tunapokaribia siku ya uchaguzi.

DODOMA,
CCM (516,317); CHADEMA (157,623).
SINGIDA,
CCM (290,899); CHADEMA (112,342).
TABORA,
CCM (413,492); CHADEMA (181,213).
MWANZA,
CCM (584,184); CHADEMA (311,532).
KAGERA,
CCM (475,910); CHADEMA (287,538).
GEITA,
CCM (377,051); CHADEMA (157,440).
SIMIYU,
CCM (318,358); CHADEMA (163,319).
MARA,
CCM (335,476); CHADEMA (221,382).
SHINYANGA,
CCM (326,936); CHADEMA (132,180).