Ng'ombe zaidi ya 5000 wafa Shinyanga kwa ukame

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,945
3,237
Sasa jamani Ng'ombe zaidi ya 5000 wamekufa Shinyanga Ukame sasa kama wanyama wamekufa, mazao yalipona?

Chakula kinatosha kweli bei ya sembe ni bei gani sukari?

Wananchi wana pesa?

======

Ofisa Mifugo mkoa wa Shinyanga, Beda Chamadata, akitoa taarifa ya hali ya mifugo jana alisema katika kipindi hicho ng'ombe waliokufa ni 5,855 na mbuzi ni 73.

Chamadata alisema wilaya ambayo inaongoza kwa idadi ya vifo vingi vya mifugo ni Kishapu 3,793, Kahama 2,112 na Shinyanga vijijini ni 23.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba, alisema kutokana na kuwepo kwa mabadiliko hayo ya tabia nchi amezungumza na wafugaji wilayani humo kupunguza idadi ya mifugo.

Chanzo: Nipashe
 
Sasa jamani Ng'ombe zaidi ya 5000 wamekufa Shinyanga

Ukame

Sasa kama wanyama wamekufa, mazao yalipona?

Chakula kinatosha kweli

bei ya sembe ni bei gani..sukari?

Wananchi wana pesa?

Source: Ng’ombe 5,000 wafa Shinyanga

Wapo bendera fuata upepo..eti wao wameshiba
Huo ni ujinga na upumbavu uliopitiliza yani hadi wanafika idadi hiyo wana waangalia tuu kwanini hawakwenda kuwauza? huu nao ni uzushi tuu... hebu weka picha ya hiyo mizoga
 
Tangu anavyodai hao wote walikufa, yeye alifanya nini kusaidia wasife!? au amesubiri tu kutoa taarifa bila kuwa na uhakika wa idadi ni kama vile ametunga tu kwa anayoyajua yeye.
 
na mvua zote hizi? ikifika august je?

Kuanzia November Mpaka February - Hakuna Mvua

Mvua Imeanza kunyesha February kati Kati

So Ng'ombe walishaanza kufa

--Elewa mvua za Vuli kukosekana (November/December/January) Mazao yalikauka na hivyo mavuno hakuna

Kuna shortage ya chakula nchini

Kwa mvua hizi, bado chakula kipo shambani
 
Tangu anavyodai hao wote walikufa, yeye alifanya nini kusaidia wasife!? au amesubiri tu kutoa taarifa bila kuwa na uhakika wa idadi ni kama vile ametunga tu kwa anayoyajua yeye.

Afisa Mifugo ulitaka Alishe Ng'ombe 5000? Una akili wewe au ni taahira?

Au ulitaka atengeneze mvua?
 
Huo ni ujinga na upumbavu uliopitiliza yani hadi wanafika idadi hiyo wana waangalia tuu kwanini hawakwenda kuwauza? huu nao ni uzushi tuu... hebu weka picha ya hiyo mizoga

Angalia gazeti la Nipashe, utaona picha

Wewe uliyeshiba..huwezi kumthamini mwenye njaa
 
Tangu anavyodai hao wote walikufa, yeye alifanya nini kusaidia wasife!? au amesubiri tu kutoa taarifa bila kuwa na uhakika wa idadi ni kama vile ametunga tu kwa anayoyajua yeye.
Tofauti na zamani,siku hizi kazi ya mtaalamu kama huyo,ni kuweka taarifa mezani kwa Mkuu (DC,RC,Waziri). Mkuu ndo atatangaza au kutoa maelekezo. Umesahau ya NIMR? Usimlaumu mtaalamu.
 
Tofauti na zamani,siku hizi kazi ya mtaalamu kama huyo,ni kuweka taarifa mezani kwa Mkuu (DC,RC,Waziri). Mkuu ndo atatangaza au kutoa maelekezo. Umesahau ya NIMR? Usimlaumu mtaalamu.

Huyo mtaalamu niambie basi alikuwa wapi tangu hao ng'ombe wanakufaa kufika labda 10, 20, 30.... 100, wengine wakiwa hoi, wakaendelea kufa hakujua hadi walipofika namba aliyoisema miezi yoteeeee hiyo!?
 
Jamani mm nimefanya kazi kanda ya ziwa. Wasukuma hawaendani na miti, wamekata miti mkoa wa Shinyanga hadi ajabu na wilaya ya Kishapu ni kama jangwa. Kwa hali hiyo lazima wakutwe na majanga hasa kama wafugaji na wakulima wenyewe hawatabadilika. Na kwao ng'ombe ndio utajiri, hata iweje hawauzi, wanaona bora afie nyumbani hapo hapo
 
Huyo mtaalamu niambie basi alikuwa wapi tangu hao ng'ombe wanakufaa kufika labda 10, 20, 30.... 100, wengine wakiwa hoi, wakaendelea kufa hakujua hadi walipofika namba aliyoisema miezi yoteeeee hiyo!?
Umejuaje hakuwa akitoa taarifa? Na mkubwa wa kutangaza akauchuna? Kwa nini RC hajamchukulia hatua? Ndugu yangu,things are not easy like that!
 
Back
Top Bottom